Ushauri: Siyaelewi haya maisha ya ndoa

Kuishi na mtoto wa mtu bila Baraka za wazazi wake ni shida,hapo ukubali umekosea. Ila ishu ya tabia,unatakiwa ujilaumu mwenyewe,mwanamke kabla hujaanzanae mahusiano ni vyema kujua vitu muhimu ili visikuumize mbeleni.
Mfano
Tabia zake(mienendo yake)
Imani yake(hapa naanisha namna anavyoweza kudeal na mambo yake binafsi)
Ana malizaje mambo? Mkiwa kwenye ugomvi,akiwa na matatizo,akiwa na furaha iliyopitiliza nk.

Ushauri wangu kwako
Kuna vitu utakutana navyo Kwa kila mwanamke dunia hii,angalia uimara wake(her potential) jiulize akiondoka leo unaamini unaweza mpata mzuri kumzidi? Kubwa zaidi muombe MUNGU akuongoze katika njia iliyo salama kwako na Kwa mwenzi wako,hii ni baada ya kumuomba msamaha,maana unawaumiza wazazi binti,na unajiumiza mwenyewe kihisia na kiroho.
All the best
 
Back
Top Bottom