Ushauri: Siyaelewi haya maisha ya ndoa

Ushauri: Siyaelewi haya maisha ya ndoa

Habari.

Nimeamua kuja humu ndani kwa kuwa nadhani ninaweza kupata akili ya kufanya maamuzi kutokana na yale yanayonisibu.

Ilitokea nilikuwa kwenye mahusiano na mwanamke mmoja yeye alikuwa ametoka kumaliza kidato cha sita na mimi chuo tulikutana kwenye mizinguko ya kimaisha Mara baada ya kila mmoja kuamua kufanya issue nje na alichokisomea hasa mimi.

Nilikuwa nae kwa mahusiano kwa muda mfupi ila nilijiona Siko serious ilhali mwenzangh yuko seriously ilimuuma kwa upande wake lakini angefanyaje.

Baada ya miaka kupita alirudi katika circle yangu na mimi ikabidi nirudishe mahusiano upya na yalikuja kwa nguvu sana haikupita muda akapata ujauzito na niliupokea na nikalea hadi leo ninalea mtoto .

Kilichonileta hapa mwanzo nikiwa nae kwa mahusiano Kuna vitabia vingi alikuwa anavificha ila leo baada ya kuishi nae karibia mwaka nimeanza kuvigundua kama Dharau,kuzira zira,,gubu,kununa muda wote na mwenye kinyongo muda wote.

Mabadiliko mengine nadhani ni ya kawaida kama kuninyima penzi na kunipa anavyojisikia yeye.

Actually ndugu zangu karibia wote wamemkataa na hawanishauri nimuoe.

Ndugu upande wa kwao wamemzira mwaka wa pili sasa unaenda hawataki kumuona yeye na mtoto wake kisa tu sijatoa mahari na nilishawaeleza ukweli siko vizuri kiuchumi ila mambo yakikaa sawa Nitatoa maana nilishaenda ukweni kutoa posa.

Kwanini nimekuja kwenu.

1.Nimekuwa nikipata stress sana kama huyu mwanamke ananifanyia visa hivi naishi nae sijamua nikimuoa itakuaje atabadilika kweli au atakuwa mbogo tu ?

2.Je upande wa mwanamke wameniziria mtoto wao kisa sijatoa mahari je Siku nikitoa mahari Kuna undugu au ndo tumemalizana.

3.Kuna muda nawaza tuachane tu tulee watoto maana sioni future kwa huyu mwanamke na hata kama nitasema niforce nimuoe naona nitakuwa naparia makaa.

Ushauri wakuu.

Umri wangu sijafika 30.

Nina kazi ya kawaida.

Nimepanga.

Naishi mwanza.

Ahsante.
Kijana mbona wewe ndio una shida, huyo binti anataka utoe mahari anaishi kwa stress kwasababu yako, wazazi wamemtenga anahisi hata wewe hutakuja kumwacha, peleka mahari au posa utamwona anavyobadirika na kurudi hali yake ya awali.
 
Kuishi na mtoto wa mtu bila Baraka za wazazi wake ni shida,hapo ukubali umekosea. Ila ishu ya tabia,unatakiwa ujilaumu mwenyewe,mwanamke kabla hujaanzanae mahusiano ni vyema kujua vitu muhimu ili visikuumize mbeleni.
Mfano
Tabia zake(mienendo yake)
Imani yake(hapa naanisha namna anavyoweza kudeal na mambo yake binafsi)
Ana malizaje mambo? Mkiwa kwenye ugomvi,akiwa na matatizo,akiwa na furaha iliyopitiliza nk.

Ushauri wangu kwako
Kuna vitu utakutana navyo Kwa kila mwanamke dunia hii,angalia uimara wake(her potential) jiulize akiondoka leo unaamini unaweza mpata mzuri kumzidi? Kubwa zaidi muombe MUNGU akuongoze katika njia iliyo salama kwako na Kwa mwenzi wako,hii ni baada ya kumuomba msamaha,maana unawaumiza wazazi binti,na unajiumiza mwenyewe kihisia na kiroho.
All the best
Hela ya mahali nilipata million kadhaa nilipomwambia nikalipe mahari alikuwa mbogo na akanishauri nikafanye kitu kingine.

Kiuhalisia mimi hata nisingeweza kuishi nae nilitaka akakae kwao ila wamemkataa hawamtaki
 
Kijana mbona wewe ndio una shida, huyo binti anataka utoe mahari anaishi kwa stress kwasababu yako, wazazi wamemtenga anahisi hata wewe hutakuja kumwacha, peleka mahari au posa utamwona anavyobadirika na kurudi hali yake ya awali.
Posa nilishapeleka mahari ndo sina hela kwa sasa uchumi wangu umekuwa mbovu..

Mpaka juzi nimemwambia nataka niuze eneo nikalipe mahari kwao anakataa?
 
Kuishi na mtoto wa mtu bila Baraka za wazazi wake ni shida,hapo ukubali umekosea. Ila ishu ya tabia,unatakiwa ujilaumu mwenyewe,mwanamke kabla hujaanzanae mahusiano ni vyema kujua vitu muhimu ili visikuumize mbeleni.
Mfano
Tabia zake(mienendo yake)
Imani yake(hapa naanisha namna anavyoweza kudeal na mambo yake binafsi)
Ana malizaje mambo? Mkiwa kwenye ugomvi,akiwa na matatizo,akiwa na furaha iliyopitiliza nk.

Ushauri wangu kwako
Kuna vitu utakutana navyo Kwa kila mwanamke dunia hii,angalia uimara wake(her potential) jiulize akiondoka leo unaamini unaweza mpata mzuri kumzidi? Kubwa zaidi muombe MUNGU akuongoze katika njia iliyo salama kwako na Kwa mwenzi wako,hii ni baada ya kumuomba msamaha,maana unawaumiza wazazi binti,na unajiumiza mwenyewe kihisia na kiroho.
All the best
Mwanzoni anaondoka kiukweli alikuwa potential sana ndo maana nikamtafuta tena ila kwa sasa amerudi naona amekuwa mbogo na kuanza kunionesha makucha yake live hapa najiuliza siku akipata hela atakuaje ?

Ukimwambia issue za kuachana anakwambia poa tu.
 
In short huyo mwanamke hana afya kwa maisha ya ndoa no matter what! Utajuta sana maishani kuwa na mke km huyo. On the other hand kuishi na mtoto wa mtu bila kutoa chochote ni hatari kuliko hatari yenyewe, haiko direct ila utaona ugumu wake ukopatwa na tatizo upande wa mkeo, utaona nyota zote. Fanya maamuzi km unataka awe mkeo lipa mahari, km humtaki acha kikaa nae kabisa
 
Kwao wamemkataa hawamtaki yeye wala watoto wangu na hapo ndipo nilipoamua kuanza kuishi nae.
 
Tatizo lako ni hapo kwenye umri wa miaka 30 ila bado unajiona ni kijana mdogo,

Huwezi kupata mwanamke ambae yupo perfect 100% hata wewe hapo una mapungufu yako,

Uamuzi ni wako,hapa utapata kila aina ya ushauri ila at the end uamuzi ni wako,

Fanya kile ambacho nafsi yako inacho kitaka,

Good luck.
 
Kwao wamemkataa hawamtaki yeye wala watoto wangu na hapo ndipo nilipoamua kuanza kuishi nae.
Kwao wamemkataa coz inaonekana kabisa hakusikia ushauri wa wazazi wake na akaja kwako kwa mapenzi yake kwako,

Wazazi wake sio kwamba wanataka mahari coz ya hela bali mahari maana yake ni kua binti yao anaolewa na sio kuishi na mwanaume bila ndoa,

Familia ya huyo Mwanamke inaonekana wanajitambua sana na walimlea binti yao kwenye maadili mema ila mapenzi yake kwako yakamtia upofu.
 
Kwao wamemkataa coz inaonekana kabisa hakusilia ushauri wa wazazi wake na akaja kwako kwa mapenzi yako kwake,

Wazazi wake sio kwamba wanataka mahari coz ya hela bali mahari maana yake ni kua binti yao anaolewa na sio kuishi na mwanaume bila ndoa,

Familia ya huyo Mwanamke inaonekana wanajitambua sana na walimlea binti yao kwenye maadili mema ila mapenzi yake kwako yakamtia upofu.
Na jamaa anataka kumkacha.

Jamaa ajiangalie na yeye ni kipi anakosea, asimkosoe binti tu.
 
Back
Top Bottom