USHAURI: Serikali ifute kidato cha 5&6 watoto waende vyuo wakimaliza kidato cha 4

Ina maana tufuate mfumo wa Kenya? Ni umri mdogo sana kuingia chuo kikuu, ni mzigo kumaliza masomo yote ya sekondari kwa miaka minne. Ni Bora kujipanga kwa masomo 3 A level ili ujue utaingiaje chuoni.
 
Yan halo dawa ni
Kutoa mikopo kwa wingi vyuo vya kati
80 ya mikopo yote iende vyuo vya kati hasa technical collage
20 % ya mikopo iende universities kwa hasa course za science tu kwa waliofaulu vizur wenye one ya digit moja
 
Naomba utofauti wa formal education na self education
Self education ni Kama aliyojifunza Elon musk Mana haijafundishwa shuleni like Warren buffet. Ila formal education unakuwa daktari muhas,unakuwa mwalimu ama mhasibu serikalini unapokea mshahara.
Yaani Yale maarifa unayojifunza baada ya kutoka shule yaani umehitimu ama
 
Ni wazo zuri sana kaka, elimu yetu ya Sekondari kwa Tanzania iishi ngazi ya Form 4 kisha wanafunzi waende vyuo (college). Mfano hai ni nchi ya KENYA, imefanikiwa sana kwenye hili. Kwao kwa sasa Elimu ya msingi mwisho STANDARD 6, kisha wanafunzi wanaendelea ngazi ya Sekondari hadi Form 4 hapo hapo wanasoma mambo ya Advance kwa Tanzania wakiwa ngazi hiyo.

Baada ya hapo wale wenye ufaulu mzuri kwa Tanzania ninge shauri baada ya Sekondari waende UNIVERSITY na wale wenye ufaulu wa wastani waende COLLEGE na wengine VETA pamoja na vyuo vya MICHEZO. Hapa tukifanikiwa vjana wetu wanaotufuata watakuwa na ubunifu zaidi ya kuwaza kusoma muda mwingi bila ufanisi zaidi.

ASANTE
 
Kusema ukweli form.5 &6 ni kupoteza muda. Ili kujenga kizazi chenye ujuzi ni bora serikali ikawekeza zaidi kwenye vyuo vya kati vinavyo toa certificate na diploma katika fani mbalimbali.

Mtoto anamaliza form 6 hana ujuzi wowote wakati alitakiwa kuajiliwa kama technician kwenye viwanda na mashirika mbalimbali.

Kazi nyingi zinazo fanywa na wenye degree ni ndogo sana sehemu nyingi.

Mtu anajiita engineer lakini kazi yake ni kutengeneza coomputer kazi ambayo ingefanywa na mtu mwenye certificate.

Badala ya kupeleka Clinical officer kwenye zahanati mnapeleka doctor aliye soma miaka 6.. haya ni matimizi mabaya ya elimu.

Hili litasaidia pia kupata wafanyakazi wenye weledi na ndio sababu nyerere alianzisha advanced diploma ili kupata watu wasio na majivuno.

Nchi hii imejengwa na wenye diploma na full technician.

Wenye degree wanatakiwa kuwa wachache na degree iwe ngumu kuipata ili hao wachache wafanye na research makubwa makubwa huko na sio kufanya kazi za watu wenye certificate.



Faida

1. Serikali itapunguza vijana wasio na ajira kwa sababu vijana wengi watakua na ujuzi.

2. Serikali itapunguza matumizi ya fedha kwa sababu watendaji wengi watalipwa fedha kidogo ukilingajisha na wenye degree.

3. Nchi itapata cheap labor kwa ajili ya viwanda, leo wenye viwanda wanapata shida kwa sababu vijana wengi wana elimu ambayo sio ya level ya viwandani. Imagine ku aasemble simu- hii ni kazi ya technician mwemye elimu ya cheti na sio mwemye degree.


Na pia kuwe na connection kati ya veta na vyuo vya kati ambavyo vipo chini ya nacte hata kama inachukua muda lakini darasa la saba aliye pita veta awe na uwezo wa kupata hadi diploma.

Siku nyingine nitaleta uzi kwa nini nacte inatakiwa kufutwa na kuundwa upya.

Vyuo vya kati ndio msingi wa maendeleo..
Wenye degree wafanye risachi ( unatuonea hapa sie kaz yetu bodaboda, kuuza matunda, kulima, kuweka nyimbo za visingel kwa pc 🤕 na kufanya ujasiliamali ambao hauhusian hata na taaluma yetu) na masters na PHD holders wafanye nn sasa 😇😂 wale wakina ndalichako professor mwenye kingereza kimoja matata 🥳🤯👽nae afanye nn sasa??
 
Back
Top Bottom