Wanafunzi kukacha kidato cha 5 & 6 na kujiunga Vyuo vya Diploma, tatizo ni nini?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,119
49,840
Utafiti wa Wizara ya elimu unaonesha kwamba kumekuwa na Wimbi kubwa la Wanafunzi Kukacha Kidato Cha 5 na 6 badala yake Kujiunga Vyuo Vya Elimu vya kati ngazi ya Diploma.

Kwani Kuna nini huko Advance na huku Diploma Kuna nini wanakimbilia?

Je inaweka kuwa wanaona Elimu ya Kidato cha 5 na 6 haiwasaidii mtaani kulinganisha na Elimu ya ngazi ya Diploma?

Je, pengine ukijiunga A level unaenda Bachelor na Sokoni Bachelor haiziki kama Diploma?

Shida nini Wanafunzi mnakimbia Ugumu au?

20230328_092728.jpg
 
Njia fupi kivipi wakati Diploma ni miaka 3 na Chuo miaka 3 au zaidi ,Huoni aliyeenda Advance ana njia fupi Kwa kupungua mwaka mmja zaidi?
Narudia tena kwa herufi kubwa
NI NJIA FUPI YA KUPATA UJUZI
Miaka mitatu ya Diploma anaujuzi tayari, miaka miwili ya Advance una cheti kisichokusaidia chochote sijamaanisha njia fupi ya kupata Degree
 
Advance ni kwenda kukua na kama hujielewi unaenda kupotea. Advance inahitaji determination, Chuo cha kati ni kwenda kupata uhuru katika umri mdogo ila kinataka uwe unatambua career path inahitaji nini haswa.
Aidha, chuo cha kati kinajenga watendaji wa kiwango cha kati waliokomaa. Kwa mtoto atakayeelemewa kwa uhuru wa bila kuchungwa atageuka kuwa mzimu wa kolelo.
 
Said it all...
 
Back
Top Bottom