Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 515
- 2,875
Waziri wa @ortamisemi Mh.@angellah_kairuki na Waziri @wizara_elimutanzania Mh. @professoradolfmkenda . Tunaomba mlione suala hili malalamiko yanazidi kuwa mengi.
# Wengi wakilalamika wamepangiwa vyuo vya kati ikiwa hawakuchagua ,ila walichagua kwenda kidato cha 5 na 6 . Kama hoja ni CutPoint (Alama) ,Kuna waliopelekwa kidato cha 5 na 6 wamepata alama sawa na waliopelekwa vyuo vya kati ingawa wao hawakuomba vyuo vya kati.
Lakini pia suala lingine ni gharama vyuo vya kati , viongozi watanzania ni Maskini uwezo wao wa kifedha na kiuchumi ni mdogo sana kugharamia Elimu , ada ya kidato cha 1 hadi 4 elf 20 kwa Mwaka hawakuwa na uwezo wa kulipa ,Serikali ikaamua kutoa Elimu bure kidato cha 1 hadi cha 4 . Lakini pia ada ya kidato cha 5 na 6 elf 70 kwa Mwaka hawakuwa na uwezo wa kulipa serikali ikafuta ada ikaweka Elimu bure kidato cha 5 na 6.
Leo hii huyu mwanafunzi anatoka kidato cha nne akisomeshwa bure bila Ada akitarajia aendelee na mzunguko wa Elimu kidato cha 5 na 6 bure,ghafla ana chaguliwa vyuo vya kati DIT, DMl ,Mwalimu Nyererere na vyuo vingine akasome Certificate na Diploma ambapo Ada kwa Mwaka vyuo hivi ni zaidi ya laki 8 .Kweli huyu mwanafunzi ataweza kweli kuendelea na masomo ?.
Ushauri wangu , Serikali kupitia @ortamisemi na @wizara_elimutanzania wekeni utaratibu kwa ambao hawataki kwenda vyuo vya kati na wana sifa waombe kupangiwa shule kidato cha 5 na 6 na kuwe na awamu ya pili ya kupangiwa shule (Selection) kuwapa fursa hawa waende shule pathway ya kidato cha 5 na 6 . Tusilazimishi vijana kwenda vyuo vya kati ,lakini pia suala la gharama vyuo vya kati liangaliwe , wengine hawana uwezo tukiwalazimisha kusoma vyuo vya kati tumewapoteza na mzunguko wao wa Elimu utakuwa umeishia hapo ,jambo ambalo ni hasara pia kwa Taifa na serikali kumsomesha bure alafu anapotea kirahisi tuu namna hii.
Cc Mh. @samia_suluhu_hassan