USHAURI: Rais Samia safisha Polisi na vikosi vyote vya usalama vinavyotuhumiwa kuteka na kuua watu

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,753
Raisi Samia nakupa mawazo tu kusaidia nchi yetu. Pamoja na mazuri Mengi aliyofanya Hayati Magufuli **** jambo baya kubwa sana ambalo kwa wengi linafunika mazuri yake mengi. Jambo hili ni kuagiza na kuunda vikosi vya kisiri vya kushughulikia watu ambao yeye binafsi na wapambe wake walikuwa wakifikiri wanarudisha maendeleo nyuma.

Tatizo kubwa la hizi fikra zilienda mbali na Magufuli kwa kuelewa au kutoikuelewa kupewa list za wabaya wa nchi na viongizi wa hivi vikosi. Utekaji huu haukuacha mtu yeyote ambaye anasema lolote kuhusu serikali bila kujali ukweli kwamba watu wote waliokuwa wanasema serikali walisema kwa nia njema ya nchi na haki za raia na ndiyo maana kisheria hakuna hata mtu mmoja ameshitakiwa na kufungwa kwa makosa ya kusema serikali.

Mifano mitatu tu hapa msadizi wa Mbowe Ben Senare alitekwa na kupotea huyu ni kijana tu masikini, Roma Mkatoliki alitekwa kwa kuimba nyimbo tu! Mfanya biashara MO alitekwa kwa miradi yake na mashamba yake na Lissu alipigwa risasi. Hivyo kikosi hiki kilikuwa na list ya wasanii, wafanyabiashara, wanasiasa, na wana harakati.Hakuna Mtanzania wa kweli mzalendo ambaye anaelewa mambo ataumizwa na haya. Na kwa wale waliofikiri huu ulikuwa uzalendo walikuwa hawaelewi! tuwasamehe bure. Kuna wengine wafanyabiashara wengi sana wamechukuliwa pesa zao bila kufuata sheria yeyote!.

Ushauri wangu Kwa Raisi ni kubadilisha viongozi wote waliohusika na hivi vikosi na kutoa ushauri mbaya kwa Raisi. Lakini kibaya idara nyingine kama mahakama zimekuwa vichekesho kwa kesi za ajabu ajabu za upinzani. Usingate na kupuliza kwenye hili umekutana na Lissu na kuongea naye na kusema unataka arudi lakini wakati huohuo huwezi kwenda hadharani na kusema Lissu atakuwa salama. Unatumia kamati kutaka kumtoa Sirro badala ya kufanya maamuzi moja kwa moja. Katibu mkuu wa zamani na polepole bado unawapa kazi wakati wenyewe ndiyo wameharibu kabisa historia ya Magufuli kwa kununua wabunge na kuharibu uchaguzi wote! wametia nchi aibu sana na sasa unatumia muda kusafisha matapishi yao!

Kufanya vitu kwa kusitasita kutakuharibia kuliko kukujenga. Ukisema utafanya kitu kama ni kwa maslahi ya umma fanya. Kwenye miaka hii ya mitandao serikali haitaweza kuzuia maoni ya watu, vyama na hata wafanyakazi wa serikali. Dunia imekuwa ndogo na ni kupoteza muda na pesa kurekodi wanasiasa kama Mgufuli bila kufuata sheria. Bila kufanya haya hawa viongozi wa wahusika wa vikosi kazi watakuja kukugeuka wewe nashauri watoe wakati huu.

Kwa wale mnaotaka Raisi Magufuli awe kama Nyerere haitawezekana hasa miaka ijayo kwasababu ya haya mambo ambayo hayana majibu!







Mh. Tundu Lissu awataja waliohusika kumshambulia.

Tundu Lissu amesema Walionipiga risasi ni Kikosi kazi kilichopo chini ya Rais kikisimasimaiwa na Mkuu wa TISS Kipilimba. Kikosi kazi kimeua watanzania wengi sana.

Kimeua watu wengi sana, Kilijumuisha watu wa Usalam wa taifa, Watu wa Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi. Kinaitwa kikosi kazi cha kupambana na Ugaidi na madawa ya kulevya.

Watu wote waliouawa Maeneo ya Mkuranga, Kibiti Kilwa Rufiji zaidi ya watu 400. Wale waliokuwa wanatupwa mtoni maiti zinaokotwa kwenye beach, wote ni Wahanga wa Kikosi hicho.

Ndio waliomteka Ben Saanane, Azory Gwanda Mdude, Mo Dewji. Yote yalitekelezwa na hicho kikosi kazi hichi chiini ya Kipilimba ammbaye sasa ni Balozi.
 
Kuna kile Kimoja chenye Askari recruited ambao Wote ni Watoto Yatima tupu ni bora ukutane na MP wa JWTZ kuliko Kukutana nao na Shughuli yao.

Na hiki Kikosi ili ujue ni balaa Kwanza Trainers wake NI kutoka Kikosi Maalum cha Makomandoo Sanga Sanga Mkoani Morogoro. Naomba niishie hapa tafadhali.
 
.....MO alitekwa na watu wanaongea kwa lafudhi za SA

!eee Mungu tumepotea wapi kama nchi?ipi TISS yenye heshima na adabu ya president Nyerere (rip),halafu mashetani haya yaliyoua watanzania wenzetu wengi tu wanakwenda kwenye nyumba za ibada na kusali eti na wao wananwomba Mungu, mapadri na mashelkh wanawapa sit za mbele, wananyenyekewa kama watakatifu kumbe are cold 🥶 blood killing machines, siku zao zitafika na kutimia
 
.....MO alitekwa na watu wanaongea kwa lafudhi za SA!eee Mungu tumepotea wapi kama nchi?ipi TISS yenye heshima na adabu ya president Nyerere (rip),halafu mashetani haya yaliyoua watanzania wenzetu wengi tu wanakwenda kwenye nyumba za ibada na kusali eti na wao wananwomba Mungu, mapadri na mashelkh wanawapa sit za mbele, wananyenyekewa kama watakatifu kumbe are cold 🥶 blood killing machines, siku zao zitafika na kutimia

Jiulize mpaka leo kesi imeishia wapi ? yalikuwa maigizo tu
 
Makonda alitamkwa wazi na Marekani kuwa amekuwa akidhulumu haki za watu kuishi.
 
Back
Top Bottom