Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 52,367
- 24,082
Rwandair awajakua sababu ya brand name mkuu ukifwatiliia zipo njianyingi kufikia hapo mojawapo unajua mji wa goma??unakumbuka sebene la m20+ unajua walikuwa wanafanya nn Kyle..+ jiongeze utaelewa kwann wamarekan wanamwaga ndege ovyo Kyle bilakujua AMA kuangalia soko AMA biashara wanayofanya n profitable AMA lah....by the way wanaendeleankufanya kwa loss kubwa tu wakiamini profit aiji leowaala Kesho but rem wanaendeleankuongeza ndege hapo n tatizoWadau, amani iwe kwenu.
Nimetafakari sana juu ya hili shirika letu la ndege hasa baada ya madudu kibao yaliyoainishwa na CAG. Hakika nashawishika kusema kuwa Shirika hilo halina sababu ya kuwa hai mpaka sasa kwa sababu zifuatazo;
Kwa mantiki hiyo, nakushauri Rais wangu fanya maamuzi sahihi. Hata kama utatumbua majipu yote yaliyoota hapo ATCL, vijipu uchungu vitaendelea kujitokeza na hivyo utajikuta unafanya kazi ya kukamua majipu tu kwa miaka yako 10 bila ya ufanisi wa shirika hilo. Wastaafishe watumishi wote wa ATCL, Anzisha shirika jipya, Tangaza nafasi za Ajira utaona jinsi watu kutoka Kenya Airways, Ethiopian Airways, FastJet, Precission Air na hata Rwandan Air watakavyomiminika kuomba kazi na hapo ndipo tutakapokuwa na shirika bora kabisa la ndege.
- Linakula fedha za walipakodi ilhali production yake ni ziro.
- Imejenga taswira mbaya na hivyo hata kama tutakuwa na ndege 100, halitaaminika tena na wadau wa usafiri wa anga.
- Jina la ATCL halitoi utambulisho wa moja kwa moja kwa nchi yetu tofauti na wenzetu wanaotumia Kenya Airways ama Rwandan Air
- Siku zote kipya kinyemi. Kama tutakuwa na shirika jipya la ndege litakuwa na ufanisi zaidi tofauti na kuweka mvinyo mpya kwenye glas ya zamani.
- Mentality ya wafanyakazi wa shirika hilo imejengeka katika kubebwa na kudekezwa hivyo hata kama tutaongeza ndege mwisho wa siku watahujumu tu
- Hawajatueleza kwa nini ndege zimepungua kutoka 9 hadi 2 na hivyo kama tukiendelea kuwanunulia ndege, tutaishia kwenda kwenye negative.
- Madudu yaliyobainishwa na CAG haiwezekani kulikarabati shirika hilo badala yake tunapaswa kulisambaratisha na hapo Mheshimiwa Rais utakuwa umejiwekea rekodi ya kuharibu kibaya ili kuwa na kizuri
Nimalizie kwa kusema kuwa "KULINUNULIA NDEGE MPYA SHIRIKA LA ATCL NI SAWA NA KUPANDISHA GHOROFA KWENYE MSINGI WA NYUMBA ISIYO YA GHOROFA"
Huku kwetu n tofauti madeniyanawasha kilakonaa just for info usiojua MPAKA Kesho kuna nchi ikikanyaga ndege ikasoma airtanzania AMA Tanzania air ndio mwishowake MPAKA walipe deni la -2000 huamini peleka jinalako Tanzania airways Yemen uone saga lake.....