Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Nimetafakari sana juu ya hili shirika letu la ndege hasa baada ya madudu kibao yaliyoainishwa na CAG. Hakika nashawishika kusema kuwa Shirika hilo halina sababu ya kuwa hai mpaka sasa kwa sababu zifuatazo;
Nimalizie kwa kusema kuwa "KULINUNULIA NDEGE MPYA SHIRIKA LA ATCL NI SAWA NA KUPANDISHA GHOROFA KWENYE MSINGI WA NYUMBA ISIYO YA GHOROFA"

- Linakula fedha za walipakodi ilhali production yake ni ziro.
- Imejenga taswira mbaya na hivyo hata kama tutakuwa na ndege 100, halitaaminika tena na wadau wa usafiri wa anga.
- Jina la ATCL halitoi utambulisho wa moja kwa moja kwa nchi yetu tofauti na wenzetu wanaotumia Kenya Airways ama Rwandan Air
- Siku zote kipya kinyemi. Kama tutakuwa na shirika jipya la ndege litakuwa na ufanisi zaidi tofauti na kuweka mvinyo mpya kwenye glas ya zamani.
- Mentality ya wafanyakazi wa shirika hilo imejengeka katika kubebwa na kudekezwa hivyo hata kama tutaongeza ndege mwisho wa siku watahujumu tu
- Hawajatueleza kwa nini ndege zimepungua kutoka 9 hadi 2 na hivyo kama tukiendelea kuwanunulia ndege, tutaishia kwenda kwenye negative.
- Madudu yaliyobainishwa na CAG haiwezekani kulikarabati shirika hilo badala yake tunapaswa kulisambaratisha na hapo Mheshimiwa Rais utakuwa umejiwekea rekodi ya kuharibu kibaya ili kuwa na kizuri
Nimalizie kwa kusema kuwa "KULINUNULIA NDEGE MPYA SHIRIKA LA ATCL NI SAWA NA KUPANDISHA GHOROFA KWENYE MSINGI WA NYUMBA ISIYO YA GHOROFA"