USHAURI: Rais Magufuli vunja ATCL. Anzisha Tanzania Airways ama Kilimanjaro Airways

Kuna majina mengine huwa yana nuksi flani, naunga mkono hoja Air Tanzania au Tanzania airways ni best option
 
Ushauri mzuri sana......hata majina pendekezwa yote yanafaa Tanzania or Kilimanjaro airways tuachane na hayo majina ambayo yameshafeli:).
 
Kilimanjaro Airways sounds waaaaaaah, itatusaidia sana kuacha kugombania huu mlima na jirani zetu
 
Shirika linahitaji kubadilishwa watendaji wake wote then watangaze upya kazi watu wa apply ili competition na uweledi uingie kwenye shirika. Airline industry is very competitive and demands high level of professionalism. That's it
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Nimetafakari sana juu ya hili shirika letu la ndege hasa baada ya madudu kibao yaliyoainishwa na CAG. Hakika nashawishika kusema kuwa Shirika hilo halina sababu ya kuwa hai mpaka sasa kwa sababu zifuatazo;
  1. Linakula fedha za walipakodi ilhali production yake ni ziro.
  2. Imejenga taswira mbaya na hivyo hata kama tutakuwa na ndege 100, halitaaminika tena na wadau wa usafiri wa anga.
  3. Jina la ATCL halitoi utambulisho wa moja kwa moja kwa nchi yetu tofauti na wenzetu wanaotumia Kenya Airways ama Rwandan Air
  4. Siku zote kipya kinyemi. Kama tutakuwa na shirika jipya la ndege litakuwa na ufanisi zaidi tofauti na kuweka mvinyo mpya kwenye glas ya zamani.
  5. Mentality ya wafanyakazi wa shirika hilo imejengeka katika kubebwa na kudekezwa hivyo hata kama tutaongeza ndege mwisho wa siku watahujumu tu
  6. Hawajatueleza kwa nini ndege zimepungua kutoka 9 hadi 2 na hivyo kama tukiendelea kuwanunulia ndege, tutaishia kwenda kwenye negative.
  7. Madudu yaliyobainishwa na CAG haiwezekani kulikarabati shirika hilo badala yake tunapaswa kulisambaratisha na hapo Mheshimiwa Rais utakuwa umejiwekea rekodi ya kuharibu kibaya ili kuwa na kizuri
Kwa mantiki hiyo, nakushauri Rais wangu fanya maamuzi sahihi. Hata kama utatumbua majipu yote yaliyoota hapo ATCL, vijipu uchungu vitaendelea kujitokeza na hivyo utajikuta unafanya kazi ya kukamua majipu tu kwa miaka yako 10 bila ya ufanisi wa shirika hilo. Wastaafishe watumishi wote wa ATCL, Anzisha shirika jipya, Tangaza nafasi za Ajira utaona jinsi watu kutoka Kenya Airways, Ethiopian Airways, FastJet, Precission Air na hata Rwandan Air watakavyomiminika kuomba kazi na hapo ndipo tutakapokuwa na shirika bora kabisa la ndege.

Nimalizie kwa kusema kuwa "KULINUNULIA NDEGE MPYA SHIRIKA LA ATCL NI SAWA NA KUPANDISHA GHOROFA KWENYE MSINGI WA NYUMBA ISIYO YA GHOROFA"
Chuki yako na watu wa Kilimanjaro imeisha lini hadi utake ATCL iitwe Kilimanjaro Airways? Kwa nn liitwe Songea Airways
 
Back
Top Bottom