ushauri plzzz!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ushauri plzzz!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by 2my, Sep 5, 2010.

 1. 2my

  2my JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2010
  Joined: Jan 30, 2010
  Messages: 289
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hbr wapendwa!
  naombeni mchango wenu wa mawazo juu ya hili!
  kuna rafiki yangu aliniomba nimsaidie kimawazo nikaona c vibaya nikapata na mawazo yenu!
  ana mdogo wake wa kike kwa sasa yupo kidato cha nne mkoani na yy yupo dsm!jana kapigiwa cm kutoka mkoani kuwa huyo mdogo wake haonekani shule tangu j,5 na alikuwa akisoma bording!kufuatilia ikasemekana kaondoka na mwanafunzi mwenzie wa kiume naye kidato cha nne na hawajulikani walipo!hiyo shule ni ya bording na day na huyo mwanafunzi wa kiume alikuwa day na pia ikasemekana alikuwa akitoroka shule na kwenda kwa huyo mwenzie kulala na kuingia shule km mwanafunzi wa day!mbaya zaidi inasemekana ana mimba yake!ss wote hawajulikani walipo na mitihani inaanza trh 4 octoba!
  km ndo ww umeombwa ushauri juu ya hili utashauri nn?
  nadhamini sana ushauri wenu!
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ripoti kwenye taasisi husika kama vile polisi, ustawi wa jamii, na ndugu zao wengine
   
 3. 2my

  2my JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2010
  Joined: Jan 30, 2010
  Messages: 289
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  thanx acid!
   
 4. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2010
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  nakubaliana na ushauri wa acid, lkn pia mwabie huyo shost yako ahakikishe wanapaitika na wanfanya mitihani
  Ila vijana mnawapa pressure wazazi jamani!?
   
 5. D

  Dopas JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ushauri wa Acid bomba, ila pia watafutwe wakipatikana maamuzi mengine yafanyike. Kwa mfano kama mtihani ni okt, huyo mama atajifungua baada ya okt afanye mtihani ili aweke future yake. Hata huyo kijana afanye mtihani wake pia ili kuandaa maisha yake ya baadaye. Kupata mimba sio mwisho wa maisha, bali ni udhaifu tu wa kibinadamu ambao kila moja anaweza kuteleza kama si leo kesho. Ila hatua za kisheria zinaweza kufuata baada ya mtihani.

  Ushauri hao vijana wakipatikana wahakikishiwe usalama wao. Pia wahakikishiwe kuwa watafanya mtihani.
   
 6. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #6
  Sep 6, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,341
  Trophy Points: 280
  Lakini pia si mwanzo mzuri wa maisha.
  Taarifa zitolewe panapohusika kama acid alivyoshauri. Suala la kufanya mtihani litategemea hisani, kisheria kutoroka shuleni ni kosa la kufukuzwa hasa katika mazingira yaliyoelezwa! Kama akiruhusiwa kufanya mtihani ni kukamilisha 'ratiba'' maana serious student hawezi kuwa anahangaika na ngono wiki chache kabla ya mtihani tukategemea mazuri. Akipatikana suala la muhimu ni kujenga nidhamu yake kwa maisha ya baadaye na kichanga chake kama kipo.
   
 7. 2my

  2my JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 30, 2010
  Messages: 289
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sure Nguruvi si mwanzo mzuri kabisa ila ndo hivyo tena maji yameshamwagika hayazoleki!
  cha msingi na muhim hapa ni wao kupatikana na wafanye mitihani ili kukamilisha ratiba km ulivyosema!then mambo mengine yafuate after exams!!!!
   
 8. 2my

  2my JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 30, 2010
  Messages: 289
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mmmmh yani Lady N kwa hali hii hawa watoto watawatoa wazazi wao roho kwa pressure heb imagine its only few dayz zimebaki kumaliza shule!so sad
   
 9. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,430
  Likes Received: 2,009
  Trophy Points: 280
  mie natoa ushauri kwa uongozi wa shule anayosoma kuwa pindi watakapopatikana wafukuzwe shule mara moja na hakuna kufanya mitihani kwani ataharibu matokeo ya shule kwa kuongeza idadi ya zero ni bra matokeo yasome "absent" kuliko miswaki tupu

  kuwapa nafasi ya kufanya mitihani ni kosa kwani kosa lao ni kubwa na ni la kufukuzwa shule wafukuzwe mara moja ili iwe mfano kwa wanafunzi wengine na kukomesha tabia hiyo na kuendeleza nidhamu
   
 10. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #10
  Sep 6, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Duh...:confused2::confused2:
   
 11. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #11
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  mhhh wakati mwingine unakuwa kama sio mzazi vile.
   
 12. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #12
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,430
  Likes Received: 2,009
  Trophy Points: 280
  sio hivyo Nyamayao nidhamu lazima ishike mkondo wake ndio maana siku hizi maadili yameshuka sana mashuleni na kwa taifa zima kosa la kutoroka shule kipindi chote hicho na kufanya mapenzi na kupeana mimba ni kosa kubwa sana tena adhabu yake inatakiwa iwe zaidi ya kufukuzwa shule

  Hivi wenzangu mmesoma shule gani? mimi shule niliyosoma kama ukichelewa siku 3 tu baada ya kufungua inapigwa sansipesheni sasa hao waliotoroka kungonoka kumimbishana na kutega shule nadhani kwa ile shule yangu wangefukuzwa na kupelekwa polisi kabisa

  Nyamayao ukiwa kama mzazi hapo unapendekeza adhabu gani shule ichukue? kuwa mkweli
   
 13. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #13
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,430
  Likes Received: 2,009
  Trophy Points: 280
  mbona umeshangaa sana askofu au hujasoma seminari zenye adhabu kama hizo?
   
 14. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #14
  Sep 6, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mm nakubaliana na ushauri wa Acid kwakweli,lkn yule .......a liesema wafukuzwe duh,kweli akili ya mbayuwayu changanya na yako but angalia ratio unayotumia kuchangany,kwann wafukuzwe?kila mzazi hapa Duniani anataka misingi imara kwa mtoto wake tena maisha mazuri mno,lkn watu hatulingani kama ambavyo hatufanani,mwisho wa siku kila mtu anataka kuwa na Furaha,Upendo na Amani,kwa sasa hao wanaona Dunia yooooote yao lakini hatuwaombei mabaya ila kesho na kesho kutwa wataona walipita njia sio,ila pia kuna wengine wamepita njia hiyo hiyo lkn mpaka sasa wako pamoja na furaha tele,Yooooooote ni mipango tu ktk maisha,zaidi tuombee Mungu wawe salama maana si binti pekee na kijana pia,wapatikane na wafanye mtihani wao na vile vile wapass(Utavuna ulichopanda)
   
 15. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #15
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  ctetei kitendo cha vijana, wamefanya kitendo kibaya sana! na kumbuka kila mzazi anatamani mtoto wake akuwe kimaadili sema na huu utandawazi wa sasa watoto wanaharibikiwa mapema/vibaya sana.....kwangu mie hata wangepewa adhabu za viboko na kupewa onyo la mwisho kwamba wakirudia wanatimuliwa jumla...
   
 16. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #16
  Sep 6, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,957
  Likes Received: 23,635
  Trophy Points: 280
  Nyamayao hujambo dada? Nimejisikia kukumisi sana..:playball:
   
 17. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #17
  Sep 6, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Nimesoma FD, lakini kwa dunia ya sasa, ni bora waachwe wamalizie hiyo mitihani yao... afterall bado huyo dada atazaa tu na kuwa grounded for a looooooooooong tym... kumfukuza kwa muda huu sio suluhisho... Preventive measures ndo zinahitajika... ili kitu kama hicho kisitokee in future.
   
 18. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #18
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,430
  Likes Received: 2,009
  Trophy Points: 280
  wameshadungana mimba sasa hapo kuna kurudia kosa tena maana kinachofuata ni kuzaliwa mtoto hapo wafukuzwe tu watakuja kujipanga akili zikikomaa
   
 19. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #19
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,430
  Likes Received: 2,009
  Trophy Points: 280
  hapo ni kuweka mbele nidhamu ya shule kwa kuonyesha mfano kwa wengine ili wasije kuiga tabia kama hiyo na hiyo ni kwa mujibu wa sheria za wizara ya elimu tukiacha haya mambo utakuta wanafunzi wote wanaishia kuzaa wakiwa sekndari na njia ya kukomesha ni kuchukua hatua kali mojawapo ikiwa ni kufukuzwa shule na vilevile wakirudi nyumbani wazazi nao wawatimue wakajitegemee si wanajiona wakubwa
   
 20. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #20
  Sep 6, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,017
  Likes Received: 3,198
  Trophy Points: 280
  Sipendi jina la "mkoani" hata sie wa huku Mbeya mnatuitaka wa mkoani.
   
Loading...