Ushauri please:housegal wangu ananitisha!!!

Ushauri please:housegal wangu ananitisha!!!

Jamani wanajamvi naombeni ushauri.mimi ni mama wa familia japo bado sina mtoto naishi na mume wangu na dada anaenisaidia kazi nyumbani.ni mfanyakazi japo kwa muda sahivi nina likizo.nimepata dada wa kazi kama wiki tatu zimepita tatizo lake tangu nimeanza kukaa nae haongei,hali hata kwa siku nzima au anakula mlo mmoja then anagoma kula wakati mwingine.nikimtuma ua kumsemesha kanuna na hajibu chochote mpaka atakapotaka yeye kunisemesha.jana nikavunja ukimya kumuuliza nini tatizo mpaka anakuwa hivyo akaanza kulia.hakula akalala na njaa leo nimeamka nikakuta hayupo karudi muda huu kamm masaa mawili tangu nilipoaamka kumuuliza alikuwa wapi kaanza kulia na kunieleza mambo makubwa sijawahi dhani lama ni hayo.siku zote alikataa nieleza nini kinamsumbua mpaka leo nilipomwambia bora nimrudishe nyumbani naona kashindwa kukaa hapa.ananambia ana mashetani yanamkataza kuongea na mimi na yanamfanya anichukie hata nikimfanyia kitu gani kizuri.tatzo lake sahivi ananipigia magoti kuniomba nisimrudishe kwao jumla but nimpe kama likizo ya siku mbili akirudi atakuwa sawa.nahitaji mtu wa kunisaidia coz soon likizo yangu inaisha lakini kwa huyu nashindwa nichukue uamuzi gani.analia sana na anaomba msamaha kwa yote na anaahidi atabadilika baada ya kwenda kwao kutambikiwa kwa siku mbili.ananiogopesha na sijui nifanyaje.naombeni ushauri jamani.

Mrudishe nyumbani kwao leo, maana mashetani yangu yananionyesha kwamba atakuuwa wakati wowote tokea 'jana'
 
Mashetani haya bwana!kwanza yalimzuia kuongea na wewe lakini baada ya kumuambia kua unamrudisha kwao ndio yamemruhusu kuongea na wewe na misamaha mingi hapa kuna tatizo huyo hata kama hana mashetani hayo ana matatizo mengine mazito sana inaonekana! tahadhari chukua hatua!
 
Mi ningeshamrudisha kwao kitambo,before even seeking a piece of advice
 
hili tatizo la wasichana wa kazi wasiokula, wenye tabia za kushangaza naona linashka hatamu sahv. Wewe ni mtu kama wa 4 hivi naskia ukiongea. Huyo dada (japo sina uhakika kama ni mapepo kweli) cha kufanya mpeleke akaombewe huku akiwa keshaweka tayari kila kilichochake, akirud mrudshe kwao. Yako meng yanaweza kukupata ukiendelea kuwa nae 1. Yanaweza yakamkwida hadi kuondoa uhai wake. Kwao utaeleza nin? 2. Siku unaweza mkuta ktandan kwako na mumeo na akakwambia ni mashetani. FUMBUA MACHO.
 
hilo sio wewe mrudishe,kuna mtu yamemkuta karibuni na hawa watu wa majini,siwezi kusema zaidi,ila mrudishe tu kwao.
 
Hataki kwenda kokote,siku za nyuma alisema anaumwa nikamwambia nimpeleke hospital akakataa.nikimwambia tuende msikitini hataki coz yeye n i too ni waislamu.na sasa ananambia anashida sana nikimridisha kwao jumla maisha yake ni mabaya na ametafuta kazi ili ajisaidie.analia ukimuona hadi huruma itakuingia kweli ananiweka njia panda
Ukitaka kumuua nyani usimuangalie usoni mama! Vipi kesho mashetani yakimwambia akuwekee sumu unadhani atakwambia? Kama maisha kwao ni magumu kama anavyodai msaidie pesa kidogo akafanye biashara ndogondogo kwao.
Mrudishe tu huyo hakufai maana hata wewe utakosa amani.
 
Ukitaka kumuua nyani
usimuangalie usoni mama! Vipi kesho mashetani yakimwambia akuwekee sumu
unadhani atakwambia? Kama maisha kwao ni magumu kama anavyodai msaidie
pesa kidogo akafanye biashara ndogondogo kwao.
Mrudishe tu huyo hakufai maana hata wewe utakosa amani.

watu wako hopeless kweli yaani wanakushauri umuludishie nyumbani,hapana umuludishie
mpeleke kwa mzee wa upako au kwa kakobe akaombwe
issue yako mbona ndogo sana
 
Ni mjamzito sahivi na naanza kazi baada ya wiki

Hata kama mamy,mrudishe tu.
Nilipataga wa kuninunia nikiwa na ujauzito wa miezi 7,kuna siku alienda sokoni asubuhi akarudi baada ya sala ya adhuhuri akapitiliza kwenda kulala. Nikawapigia simu kwao wakaniambia ndivyo alivyo huwa ana ugonjwa wa akili. Kesho yake nilimpakia basi akaenda kwao sikujali hali yangu wala ukweli kuwa nafanya kazi.
Unaweza kuta kafungia mtoto kwenye freezer akakutafutia kesi ya kuua bure maana nawe hutamuacha salama
 
asante kwa ushauri,sababu iliyonifanya niwe na dada wa kazi ninafanya kazi za projectna mara nyingi nakuwa safarini nikirudi ni baada ya two to three weeks na niliishi kwa muda bila kuwa na msaidizi.tatizo niliweka msaidizi wa kiume baada ya kuona nyumba inakaa tupu muda mrefu na eneo hili usalama mdogo ut yule kaka alisubiri tisafiri wote kurudi tukakuta nyumba nyeupe.kakomba kila kitu tukaanza moja na kukaa muda kifogo bila mtu.tatzo lilijitokeza tena nyumba inakuwa chafu nahata usalama wa nje ni mdogo ndio tukaamua kuwe na housegal kwa kipindi hichi nilichoko likizo mpaka nikianza kazi ntamuacha mwenyewe atakuwa amezoea.ana wiki tatu now na matatzo ndio hayo.

kulia kwake anakuonea aibu na huruma jinsi unapokuwa umesafiri kwenye project zako yeye anavyokula mavituuuuuzi ya nguvu, ndani ya sita kwa sita, magoli tatu kwa tatu jumla sita
 
watu wako hopeless kweli yaani wanakushauri umuludishie nyumbani,hapana umuludishie
mpeleke kwa mzee wa upako au kwa kakobe akaombwe
issue yako mbona ndogo sana

Ndogo eeh!
Mi naona ungemsindikiza huko kwa mzee wa Upako au kwa Kakobe.
 
Mental problem zina namna nyingi ya kujitokeza, labda ni bi-polar.

Na ww huna hata mtoto dada wa nin? Kwani una ujauzito?
Na kama ni mashetani kweli si umpeleke kwao akatibiwe? Kuna siku yatamtaka alale na mmeo, utayakatalia?
 
Jamani wanajamvi naombeni ushauri.mimi ni mama wa familia japo bado sina mtoto naishi na mume wangu na dada anaenisaidia kazi nyumbani.ni mfanyakazi japo kwa muda sahivi nina likizo.nimepata dada wa kazi kama wiki tatu zimepita tatizo lake tangu nimeanza kukaa nae haongei,hali hata kwa siku nzima au anakula mlo mmoja then anagoma kula wakati mwingine.nikimtuma ua kumsemesha kanuna na hajibu chochote mpaka atakapotaka yeye kunisemesha.jana nikavunja ukimya kumuuliza nini tatizo mpaka anakuwa hivyo akaanza kulia.hakula akalala na njaa leo nimeamka nikakuta hayupo karudi muda huu kamm masaa mawili tangu nilipoaamka kumuuliza alikuwa wapi kaanza kulia na kunieleza mambo makubwa sijawahi dhani lama ni hayo.siku zote alikataa nieleza nini kinamsumbua mpaka leo nilipomwambia bora nimrudishe nyumbani naona kashindwa kukaa hapa.ananambia ana mashetani yanamkataza kuongea na mimi na yanamfanya anichukie hata nikimfanyia kitu gani kizuri.tatzo lake sahivi ananipigia magoti kuniomba nisimrudishe kwao jumla but nimpe kama likizo ya siku mbili akirudi atakuwa sawa.nahitaji mtu wa kunisaidia coz soon likizo yangu inaisha lakini kwa huyu nashindwa nichukue uamuzi gani.analia sana na anaomba msamaha kwa yote na anaahidi atabadilika baada ya kwenda kwao kutambikiwa kwa siku mbili.ananiogopesha na sijui nifanyaje.naombeni ushauri jamani.

Kiumbeya zaidi: 'Unayataka...yaani wewe na mumeo tu, no mtoto bado unahitaji housegirl!? Uvivu wako unakuponza'
 
Duh embu kwanza mrudishe kwao!!!!kama una imani mpeleke akaombewe ila sio kwa mama lwakatare wala mzee wa upako wa la mchungaji yeyote maarufu wa dar!!tafuta nyumba za maombi hizi ndogo ndogo au wale wamama au wababa wa mitaani wanafahamikaga mitaani kwetu kuwa fulani anakipawa cha kuombea!mpelike hapo akikataa rudisha kwao fasta!!!!usije ukatiwa utasa bure!!!! Na akiondoka ndani ukague kwelikweli na ndani kwako asiingie kwa kawaida labda aingie kichawi kuna vitu vingine kichawi lazima viwekwe fizikali na mhusika!!!!wanategaga vitu vya ajabu sana...fuata haya niliyokuambia mimi la sivyo hatabaki hata panya mmoja
 
Kiumbeya zaidi: 'Unayataka...yaani wewe na mumeo tu, no mtoto bado unahitaji housegirl!? Uvivu wako unakuponza'

Si uvivu ndugu yangu situation zote nimeeleza why nimeweka dada wa kazi.si mbaya lakini ulivyojibu post yangu sikulaumu sababu naona hujasoma maelezo yangu yote.asante
 
Nakuunga mkono Mamndenyi, hakuna sababu yoyote ya kupoteza muda adimu wa kumpeleka kwenye maombi. Muhusika anajua ana "mashetani" atafute muda wake mwenyewe akapambane nayo.

Wamama wengine kweli mnao ujasiri wa ajabu sana;
Mie ningempa chake na kumkabidhi kwa aliyeniletea leo hii hii.
 
Last edited by a moderator:
Ni mjamzito sahivi na naanza kazi baada ya wiki

Yaani mdogo wangu, watu karibu wote humu wanakushauri mrudishe kwao. mpaka hapa comments zilipofika wala sidhani kama unahitaji zaidi ya hapo, hata kama ni mjamzito tafuta mwingine tu, huyo MRUDISHE FULL STOP. Binafsi nimeshakaa na wasichana wengi sana nawafahamu kweli, wa dizain hiyo ya kwako hatakufaa kabisa, and you know what, mshukuru Mungu amekuonesha mapema. sikutishi lakini kitakachofuata baada ya hapo utakuja kusema humu sikumoja atakapokugeuka na mumeo, wabaya sana hao wala si wakucheka nao kihivyo, na utakuja kushangaa sasa ukigundua wala hutaomba ushauri utamrudisha mwenywe tu na utashangaa zaidi utakapo mrudisha ukajikuta unagombana na mumeo kwamba kwanini umemrudisha wakati ni msichana mzuri tu. Ushauri mwingine, kulingana na imani yako na dini yako embu uwe unaomba kwanza wakati unatafuta wasichana au wasaidizi maana mara nyingine huwa tunakaribisha mapepo na mashetani ndani ya nyumba zetu bila kujua.
 
Asanteb kwa ushauri wadau nadhani mpaka sahivi nimeshapata uamuzi nini cha kufanya kupitia ushauri wenu.wengi wamehoji kwanini nimetafuta ushauri while ningeweza chukua maamuzi ya kumuondoa mm mwenyewe lakini sikuweza fanya uamuzi wa haraka kwa kuwa nilikuwa njiapanda.binafsi maisha yangu mpaka kufika hapa nilipitia matatzo na kwa wakati ule sikupata mshauri.japo si ya aina hii lakini ni maisha ya kunung'unika,ukimya na hata kulia sikuwa na mtu wa kunishauri.nilihisi bila ya kumsaidia huyu binti inanikumbusha maisha niliyoishi.maisha ya kukimbiwa na mzazi(baba) nikahangaika na wadogo zangu nikimsaidia mama kufanya biashara ndogo ndogo huku nikiwa shule ya msingi.so muda mwingi nilikuwa mtu wa huzuni na masikitiko.asanteni kwa ushauri mbarikiwe!
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Similar Discussions

Back
Top Bottom