Ushauri please:housegal wangu ananitisha!!!

Pole sana, huyo si wa kumuamini kabisa. Achana naye utafute mwingine kabla likizo yako haijakatika. "Mashetani" yake yanaweza kumwambia akufanyie wewe au mwenzio kitu kibaya zaidi badala ya kuacha kuongea tu.
 
Pole sana, hapo "shetani" ni yeye mwenyewe mbona leo ameongea, asilimia kubwa ya dada wa kazi hufanya hivyo. mara nyingine inakua ni uoga wao tu na wengine ni kiburi au alitegemea kukuta mazingira tofauti na hayo.

jambo la msingi ni kumuacha tu aondoke moja kwa moja, ukimuacha kuna siku"mashetani " wake watamwambia akufanyie kitu kibaya zaidi ya hivyo anavyofanya.

halafu ungekuwa una mtoto sawa ila mpo wawili tu mbona unajipangia ratiba zako za home vizuri kila kitu kinaenda sawa bila kuwa housegirl na ofcn unawahi kama kawaida
 
Pole sana,asikuumize kichwa mpe nauli arudi kwao,kuna uhakika gani kama hayo mashetani yake yataondoka pindi utakapo mpa hizo siku 2?Kwanini akuchukie wewe tu na sio mmeo?chukua hatua sasa.
 
Anamtamani mumeo huyo,kama unabisha hebu mkabidhi mumeo hilo suala,wiki moja tu kwisha habari!
 
mh pole ndugu bt most of housegirls na houseboys hawaeleweki yan waaminifu wachache sana,

so kwanini usikae hata na ndugu mmoja either wa mume au wako
 
Yaani kwa issue kama hiyo unataka tukushauri nini jamani? Hayo mashetani kuna siku yatamfanya akuchinje.

Japo kwa upande mwingine sijamuamini. Hayakuweza kumzuia asikuambie ukweli? Mpeleke kwenye maombi then mrudishe kwao akalee imani ili mashetabi yasirudi.
 

Inamaana huna uwezo wa kupata mwingine. Tumia likizo hiyo kutafuta mwingine kwanini uumize kichwa kwa mtu wakati maisha yenyewe yanakaba. Kazini uumize kichwa tena home. Mrudishe kwao tena mlipe kila kitu ili akajute huko.
 
Pole sana bora nusu shari kuliko shari kamili,huyo siyo binadamu mrudishe kwao haraka vinginevyo utahatarisha nyumba yako hayo mashetani yanaweza kula hata watoto wako au wewe mwenyewe,hima mrudishe akagange yake mwenyewe huko kwao,hata kwenye maombi usimpeleke wewe aende mwenyewe kwani anaonekana anayafurahia unajua maombi kama imani yako ni haba yanaweza kurudi kwako tena kwa shari sasa ya nini kudhurika fanya maamuzi magumu ujiepeshe na hiyo kadhia.
 
pole lakini kame wewe si mjamzito mtoto wa kazi wa nini jamani! umrudishe tu kwao atakusumbua sana huyo
 
Bi dada achana na habari za kukaa na mabinti iwapo huna mtoto unless kama ni mjamzito ila kama bado ishi wewe na mumeo jaribu kuboresha maisha kwa kuweka vitendea kazi vya kukusaidia. ukianza kuhangaika na mabinti wenye mapepo leo hi hata kachanga huna ukija kupata si ndo upakatiwa mtoto na shetan lenyewe??

huo mshahara unaomlipa na kula anakokula nk ni bora ununue dishwasher, na washing mashine, pamoja na mopa na blower. siku ya j1 unafua na kusafisha nyumba yako na kupanga kama zinakuzidi tafuta kijana wa kiume ambaye atakuja akupasie iyo siku ya j1 na kukufagilia uwanja basi.
 
Tushaletewaga dada wakazi mmoja hivi, kwanza ni mbaya ukimwona unajua kabisa mtoto hatamkubali, tukashindwa kumfukuza kwa sababu hiyo.

Sasa wakati anaenda kuoga tukaona bonge la hirizi kajifunga mkononi kwa juu karibu na bega dah! Mwili ulinisisimka balaa, hatukulala mpaka kesho yake tulivyomrudisha kwao.

Sasa wewe ukitaka kucheza na mashetani kaa nayo, utapata bonge la fundisho ndo ujue shetani ni nani. Mtu kakurahisishia sababu za kumwondoa wewe unamlea?
 

Swtlady ​chukua huu ushauri kama ulivyo, usiongeze wala usipunguze kitu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…