Ushauri: Nimemkuta mpenzi wangu live ananisaliti

Habari za usiku huu wakuu.
Nimekuja kwenu kuomba ushauri juu ya mambo yaliyonitokea leo.Nilikua na mpenzi ambaye nilimpenda sana, tangu tuanze mahusiano tunamiezi minne mpaka muda huu ninaoandika hapa JF.

Nilikua simfuatilii mienendo yake kwasababu nilikua sitaki kuumiza moyo wangu, najifahamu hali ninayokua nayo kama nikijua mpenzi wangu anamtu mwingine.

Daaah!!Sasa leo nimemkuta na mtu mwingine wamekumbatiana huku anamkiss, kusema kweli nimeumia moyo. Hapa nilipo nina hali mbaya maana najikuta mwili unatetemeka kwa hasira kila nikikumbuka tukio. Kichwa nacho kinaniuma.

Sijui hata nifanye nini ili nirudi katika hali ya kawaida.

Nimekuja hapa mnisaidie jinsi ya kuondoa hii hali, kila nikijaribu kuiondoa nashindwa kwasababu kila nikisikia tu sauti yake hali inajirudia. Ieleweke nakaa nae mtaa mmoja, ni nyumba ya tatu kutoka ninapoishi.

Mnisamehe kama kuna makosa ya uandishi katika thread yangu, sipo vizuri kabisa now.
NAWASILISHA.
wanzinzi bhana
 
First,Calm yourself down n Relax.
Ni wazi hapo ulikosea kwa kumuamini kwa haraka sana "Trust no body even yo self".

SOLUTION: Usifikiri ku-react kwa namna ambayo itamfanya a-feel proud kwa alichokifanya (act normal kabisa ikiwezekana salimiana nae vizuri kabisa na Mpe hongera kwa maamuzi aliyoyafanya) kwa Sababu Ana expect ww u-react kwa hasira/ujichukulie hatua mkononi dhidi yako/yake ama jamaa yake huyo/Umchunie au uoneshe kusononeshwa ama kuumizwa kwa kitendo alichokifanya. "Don't grant her wish,bro" you deserve someone better than her n even best,pull yo self up n build yo future.

Who made for you will come to you, Have yo dreams intact n fulfill them N u shall surely have yo dream wife as a bonus.
So wise indeed [emoji122][emoji122]
[emoji9]
 
Nifikiri ni mwanamke/mke ambaye umekuwa naye kwa kipindi kirefu na kuzaa mtoto/watoto. Hapo pangehitajika ushauri unaotokana na tahadhari ya kina juu ya mambo mengi.

Kwa huyo wa uhusiano wa mwezi minne, ushauri wangu ni kwamba pia mwenyewe kwanza faida na hasira za kuendelea naye. Binafsi ningeachana naye kwa sababu ninapata "kichefuchefu sana" nikishajua anauhusiano na mtu mwingine.
 
First,Calm yourself down n Relax.
Ni wazi hapo ulikosea kwa kumuamini kwa haraka sana "Trust no body even yo self".

SOLUTION: Usifikiri ku-react kwa namna ambayo itamfanya a-feel proud kwa alichokifanya (act normal kabisa ikiwezekana salimiana nae vizuri kabisa na Mpe hongera kwa maamuzi aliyoyafanya) kwa Sababu Ana expect ww u-react kwa hasira/ujichukulie hatua mkononi dhidi yako/yake ama jamaa yake huyo/Umchunie au uoneshe kusononeshwa ama kuumizwa kwa kitendo alichokifanya. "Don't grant her wish,bro" you deserve someone better than her n even best,pull yo self up n build yo future.

Who made for you will come to you, Have yo dreams intact n fulfill them N u shall surely have yo dream wife as a bonus.
Hicho kidhungu kupata GPA 3.5 itakuwa ngumu sana!!!
 
mnyang'anye kila kitu ulichomhonga ili akili imkae sawa nyambafu zake huyo.
 
Habari za usiku huu wakuu.
Nimekuja kwenu kuomba ushauri juu ya mambo yaliyonitokea leo.Nilikua na mpenzi ambaye nilimpenda sana, tangu tuanze mahusiano tunamiezi minne mpaka muda huu ninaoandika hapa JF.

Nilikua simfuatilii mienendo yake kwasababu nilikua sitaki kuumiza moyo wangu, najifahamu hali ninayokua nayo kama nikijua mpenzi wangu anamtu mwingine.

Daaah!!Sasa leo nimemkuta na mtu mwingine wamekumbatiana huku anamkiss, kusema kweli nimeumia moyo. Hapa nilipo nina hali mbaya maana najikuta mwili unatetemeka kwa hasira kila nikikumbuka tukio. Kichwa nacho kinaniuma.

Sijui hata nifanye nini ili nirudi katika hali ya kawaida.

Nimekuja hapa mnisaidie jinsi ya kuondoa hii hali, kila nikijaribu kuiondoa nashindwa kwasababu kila nikisikia tu sauti yake hali inajirudia. Ieleweke nakaa nae mtaa mmoja, ni nyumba ya tatu kutoka ninapoishi.

Mnisamehe kama kuna makosa ya uandishi katika thread yangu, sipo vizuri kabisa now.
NAWASILISHA.

Sio mke? Songa mbele.
 
Nilifikiri uliwakuta uchi kitandani, kumbe wanakiss tu. Tena wamevaa nguo!!!!
wapotezee tu
 
kwani ndugu zake wote unawajua? walikua wanakumbatiana hadharani au?
Mnaishi dunia gani? Hamjawahi kusikia mtu na dada yake, mtoto wake wanakulana? Suala sio wakoje bali ni tendo la kimahaba waliouwa wanafanya.
 
Kataa kufinywa kwa demokrasia,ongeza juhudi katika utafutaji,jua ulichagua mfanya buashara na si mpenzi,kumbuka wanawake ni wengi kuliko wanaume,wekeza akili kwenye utafutaji,jenga maisha yako,kamata mwingine.
 
Habari za usiku huu wakuu.
Nimekuja kwenu kuomba ushauri juu ya mambo yaliyonitokea leo.Nilikua na mpenzi ambaye nilimpenda sana, tangu tuanze mahusiano tunamiezi minne mpaka muda huu ninaoandika hapa JF.

Nilikua simfuatilii mienendo yake kwasababu nilikua sitaki kuumiza moyo wangu, najifahamu hali ninayokua nayo kama nikijua mpenzi wangu anamtu mwingine.

Daaah!!Sasa leo nimemkuta na mtu mwingine wamekumbatiana huku anamkiss, kusema kweli nimeumia moyo. Hapa nilipo nina hali mbaya maana najikuta mwili unatetemeka kwa hasira kila nikikumbuka tukio. Kichwa nacho kinaniuma.

Sijui hata nifanye nini ili nirudi katika hali ya kawaida.

Nimekuja hapa mnisaidie jinsi ya kuondoa hii hali, kila nikijaribu kuiondoa nashindwa kwasababu kila nikisikia tu sauti yake hali inajirudia. Ieleweke nakaa nae mtaa mmoja, ni nyumba ya tatu kutoka ninapoishi.

Mnisamehe kama kuna makosa ya uandishi katika thread yangu, sipo vizuri kabisa now.
NAWASILISHA.
epuka mpenzi uliyenae
shule moja
mtaa mmoja
ofisi moja
.
.
.
.
matokeo yake yanakuwa hivi.
 
Kwanini unampa mwenzio ushauri wa hivi?kakukosea nini labda?unajua labda yuko katika hali gani?tujifunze kuheshimiana watanzania itatusaidia sana katika kujikomboa hata kifikra
mkuu huo ndo ushauri wangu,we unaweza kuuona sio mzuri lakini Mimi ndo nauona unafaa
 
Hilo tatizo limewatokea wengi sana na sio wewe mwenyewe tu..kikubwa wewe mshukuru Mungu umeyashuhudia mapema kabla hata hamjaoana...fikiria ingetokea hivyo wakati mko kwenye ndoa na mna watoto??? Huyo hakufai na Mungu kakuonyesha mapema...piga chini songa mbele.
 
Back
Top Bottom