Athed Jnr
Senior Member
- Jul 27, 2016
- 150
- 68
Habari za usiku huu wakuu,
Nimekuja kwenu kuomba ushauri juu ya mambo yaliyonitokea leo. Nilikuwa na mpenzi ambaye nilimpenda sana, tangu tuanze mahusiano tunamiezi minne mpaka muda huu ninaoandika hapa JF.
Nilikuwa simfuatilii mienendo yake kwasababu nilikua sitaki kuumiza moyo wangu, najifahamu hali ninayokua nayo kama nikijua mpenzi wangu anamtu mwingine.
Daaah! Sasa leo nimemkuta na mtu mwingine wamekumbatiana huku anamkiss, kusema kweli nimeumia moyo. Hapa nilipo nina hali mbaya maana najikuta mwili unatetemeka kwa hasira kila nikikumbuka tukio. Kichwa nacho kinaniuma.
Sijui hata nifanye nini ili nirudi katika hali ya kawaida. Nimekuja hapa mnisaidie jinsi ya kuondoa hii hali, kila nikijaribu kuiondoa nashindwa kwasababu kila nikisikia tu sauti yake hali inajirudia. Ieleweke nakaa nae mtaa mmoja, ni nyumba ya tatu kutoka ninapoishi. Mnisamehe kama kuna makosa ya uandishi katika thread yangu, sipo vizuri kabisa now.
NAWASILISHA.