Ushauri: Nimejenga nyumba lakini kabla haijaisha nikafukuzwa kazi

Hauna hata NSSF? FAO la kujitoa bado halijapamba moto, chukua pesa biashara nyiiingi sana ila usiwe mtu Wa aibu kama wasomi wetu. Kuna jamaa humu ana mashine za kutengeneza mkaa,hii ni biashara ya uhakika unatoboa Mara moja.

Naomba unielekeze hiyo mashine mkuu
 
Kwanza kujenga tu ukiwa una uhakika wa kipato cha moja kwa moja its risk sana na risk yake ndio hii hapa jumba linageuka guest house...madogo wanazaliwa humo hadi wanapata akili na wao wanagongea mademu zao humo wanazalisha watoto wakitokea kwenye jumba hilo hilo walilozaliwa wao awali.

Hii mistake waafrika wengi tunaifanya unakuta mtu kajenga Nyumba ya milion 70 kwa mkopo afu analipwa la laki mbili tu baada ya makato yote kwa mwezi....huyu anakuwa deserving poor...ulaya na nchi zilizoendelea watu wanapanga kwa muda sana hadi wajenge zao hiyo milion 70 hiyo..inaenda kuleta hela nyenzake huko nje.

Waafrika mbona hatujifunzi kutoka kwa wazungu, wahindi, na waarabu? Hawa hawawezi kujenga hadi wawe na kipato imara kwenda kuitupa milion 70 kwenye Nyumba ikae tu kijinga kwao ni msamiati wasiouelewa kabisa...huwa wanakomaa na Kazi na biashara hadi wawe na uhakika wa kujenga na kubakia na mtaji mkubwa wa kuendeleza biashara zao..ndio maana wengi wamepanga kwenye Nyumba za bei ndogo za msajili.

Bongo heshima ni kuwa na kajumba wakati unachoingiza hakieleweki...

imbecilic!
 
Usiuze hata kidogo,
Iache kwa muda,tafuta shughuri ya kufanya,harafu weka paa nusu(kitaa tunaita slopu),hamia,
Chonde chonde usiuze ndugu yangu!!
Ahsante sana tena sana kijana mwezangu kwa huu ushauri ambao umenipa na kunitia moyo kwa kunisisitiza pia
 
Nilianza ujenzi wa nyumba yangu ya vyumba 3, master bedroom 1, viwili vyoo vya ndani, jiko, sebule na choo. (nyumba bado sijaezeka)

Ila sasa nimekwama jinsi gani naweza kuimalizia na kwani sasa kazi nimefukuzwa.

Naomba ushauri nifanye nini ili niimalizie au Niiuze ili nifanye biashara kwa mtaa? Maana sioni njia ya kuweza kuimalizia kwa sasa na hata kwa baadae.View attachment 771252
Kauze upate mtaji acha maisha ya kutegemea binadamu jitegemee kwanza hiyo siyo nyumba ni kiwanja au tuite pagare sijawahi kuajiriwa sitegemei kuajiriawa nimejiajiri nakushauri ujiajiri
 
Kwanza kujenga tu ukiwa una uhakika wa kipato cha moja kwa moja its risk sana na risk yake ndio hii hapa jumba linageuka guest house...madogo wanazaliwa humo hadi wanajua jumba liko pale pale.

Hii mistake waafrika wengi tunaifanya unakuta mtu kajenga Nyumba ya milion 70 ya mkopo afu analipwa la laki mbili tu...huyu anakuwa deserving poor...ulaya na nchi zilizoendelea watu wanapanga kwa muda sana hadi wajenge zao hiyo milion 70..unaenda kuleta hela nyenzake.

Bongo heshima ni kuwa na kajumba wakati unachoingiza hakieleweki...imbecilic!
Mkuu kodi zinatia uchizi, Bongo ukikosa Kodi unarudi kijijini fasta,ukiwa na banda lako unakomaa kimjini mjini, unaezeka chumba kimoja maisha yanaendelea.
 
HUSIJARIBU KUFIKIRIA KUIUZA,CHA MSINGI PAMBANA KWA NAMNA NYINGINE SIKU UKIJALIWA UTAIMALIZIA TU,KUNA KIPINDI NAMI NILIKWAMA MWAKA 2011,WAKATI HUO NYUMBA ILIKUWA KWENYE MADIRISHA ILA NILIPAMBANA BADAE IKAISHA KABISA BILA MATATIZO,KAZA MOYO.
 
Usiuze aise.....pambana ,tunafanana tatizo ila nami kidogo niingie chaka kuuza kwa Jirani hatua kazaa ili nijikimu na vyuma kukaza ila nikatafakari nipambane kivingine ....Namimi tatizo lako kama langu....tupambane ki vingine tu
 
Hapa ndio utagundua akili ya wabongo ilivyodumaa, washauri wengi humu ni eti asiuze hilo gofu huku kazi hana na hana kipato chochote.FYI hilo gofu hapo lilipo kwa sasa ni liability kwa maana litakuchukulia vijisenti vyako kila uchao kwa kodi za jengo.
Ushauri wangu uza pata mtaji anza biashara maisha yanasonga utakuja pata utajenga au kununua ingine.usidumazwe na akili ya eti una nyumba ndio basi.. hilo ni gofu tu hapo halikuingizii chapaa yoyote hapo.
za kuambiwa changanya na za kwako.
 
Mkuu kodi zinatia uchizi, Bongo ukikosa Kodi unarudi kijijini fasta,ukiwa na banda lako unakomaa kimjini mjini, unaezeka chumba kimoja maisha yanaendelea.
Kodi siku hizi easy tu na serikali ishasisitiza kulipia kodi kwa mwezi mmoja hamna kulipa kwa miezi 6 tena.

Kwenye maisha kuna liability na asset.....hiyo nyumba sio asset tena Bali ni liability... Ni Mzigo kwako. Na hapa ndio inabidi uoneshe uanaume wako..usidhani kuwa na paipu pekee ndio uanaume. No..hapa ndipo mashujaa wakiume wanapimwa. Kila la kheri mkuu.

If you can't take risk how will you succeed?

Ningekuwa na muda ningekupa somo moja muhimu sana la "Comfort zone"

Then what's next?
 
Hauna hata NSSF? FAO la kujitoa bado halijapamba moto, chukua pesa biashara nyiiingi sana ila usiwe mtu Wa aibu kama wasomi wetu. Kuna jamaa humu ana mashine za kutengeneza mkaa,hii ni biashara ya uhakika unatoboa Mara moja.
unamaanisha nn ndugu, kwa "fao la kujitoa halipamba moto".
 
Sisi Wapemba tunasema "KUUZA NI KUGEA" (kutupa), usiuze mkuu, jaalia kama huna hilo jengo, fikiria njia nyengne ya kujikwamua
 
Back
Top Bottom