Ushauri: Nataka nikaishi Ulaya

Ushauri: Nataka nikaishi Ulaya

Msaada wakuu,

Bongo kwangu tafrani,

Nimetumia kila njia kufanikiwa na kujituma sana katika maisha ya hapa Tanzania na sijafanikiwa.

Kama kusoma nina Diploma IT,
Kama biashara nishafanya bila mafanikio.

Nimeona nitafute nchi nyingine nihamie,
Niko tayari kufanya kazi yoyote huko.

Ushauri wenu wakuu niende nchi gani Ulaya ambapo ndoto zangu nitazifanikisha.
Kama ni kazi yoyote mbona zipo nyingi tu hapa.....0713
 
Msaada wakuu,

Bongo kwangu tafrani,

Nimetumia kila njia kufanikiwa na kujituma sana katika maisha ya hapa Tanzania na sijafanikiwa.

Kama kusoma nina Diploma IT,
Kama biashara nishafanya bila mafanikio.

Nimeona nitafute nchi nyingine nihamie,
Niko tayari kufanya kazi yoyote huko.

Ushauri wenu wakuu niende nchi gani Ulaya ambapo ndoto zangu nitazifanikisha.
Ulaya ilikuwa zamani,siku hizi hali ni ngumu huko pia.
Kwenda ulaya kwasasa ni kupoteza muda.Komaa na maisha hapa hapa Tanzania utatoka tu.
 
Mkuu Ulaya takudaganya ingelikuwa Africa ningekushauri japo kidogo. Wala haihitaji ushauri kwa jambo kama hilo, anzia tu nchi za Africa then ukajikuta unaingia Ulaya kama unateleza tu. Labda nikuulize, una familia?
Nenda Libya kuna njia rahisi ya kukaza kwenda europe,mambo mengine yote utayapata unifika Libya.Kila pa kheri.
 
Umri ulionao si vibaya ukavumilia kidogo pia kuna nchi hapa hapa Africa unaweza kuishi vizuri tu kama uko Ulaya. Naheshimu mawazo yako maana ndiyo ilikuwa akili yangu tangu namaliza form four Geita (Geseco). Kwa sasa niko kusalimia familia yangu mwezi huu katikati nang'oka tena. Hebu jaribu kuingia Botswana na ukifika tu parangana kuoa demu wa huko harafu ulete mrejesho hapa, mie ndo teknic zilizonifikisha South Africa na sasa sijiiti mzamiaji tena. (sina chats za private for positive reasons)
1475437746270.jpg
 
Nenda Libya kuna njia rahisi ya kukaza kwenda europe,mambo mengine yote utayapata unifika Libya.Kila pa kheri.
Hiyo njia ya mauti, aingie tu Botswana harafu akapate mchumba ambaye asilimia kubwa wanafanya kazi mining na hapo nayeye ataunganishwa kufanya kazi baada ya kupata work permit au uraia baada ya kuoa hata kama kwa shingo upande. Baadae ataanza ku hustle kuingia Europe kama haridhiki na noti za pura
 
Nenda Libya kuna njia rahisi ya kukaza kwenda europe,mambo mengine yote utayapata unifika Libya.Kila pa kheri.
Ya nini akawe chakula cha samaki wa mediteranian sea?komaa bongo kijana ,ukiona wakimbizi wanavyokufa baharini kutoka libya kisa ulaya,utafikiri ulaya ni paradiso.
 
Dogo sepa usawa wa hapa bongo kwa sasa ni nomaa...mi mwenyewe nasepa soon
 
Usipokuwa na kinyaa,kuna kazi za kuosha kinyesi wakongwe,mshahara mzuri,tip za kumwaga,tofauti na hapo,utakuwa unawakimbia wabongo wenzio waliotoka kuja kutembea,maana utaishi miaka kumi na jeans moja na mia huna mfukoni,mwisho unakuwa mlowezi.
Bongo bado inalipa,changanya akili kama karata tu.
 
Ya nini akawe chakula cha samaki wa mediteranian sea?komaa bongo kijana ,ukiona wakimbizi wanavyokufa baharini kutoka libya kisa ulaya,utafikiri ulaya ni paradiso.
Hapa hapa ni ulaya,atoke jasho na atumie akili tu,huko ni Desemba kwenda kutembea tu.
 
Yaani miaka 22 ndio unasema umeshaangaika sana kutafuta maisha ikiwemo kufanya biashara mambo yakagoma.
Huo umri ni mdogo sana,,ninavyokuona kama vile unapenda shortcut kufikia mafanikio.

Yaani miaka 22 ndio unasema umeshaangaika sana kutafuta maisha ikiwemo kufanya biashara mambo yakagoma.
Huo umri ni mdogo sana,,ninavyokuona kama vile unapenda shortcut kufikia mafanikio.[/QUOTE]
Mafanikio hayana umri maalum wala formula mkuu,
kujaribu ni moja ya njia ya mafanikio.
shortcut ya maisha ni juhudi zako na maarifa katika kutafuta mafanikio.
[/QUOTE]

Hili jibu inaonyesha una AKILI kichwani acha wanaoponda waendelee kuponda
 
Hiyo njia ya mauti, aingie tu Botswana harafu akapate mchumba ambaye asilimia kubwa wanafanya kazi mining na hapo nayeye ataunganishwa kufanya kazi baada ya kupata work permit au uraia baada ya kuoa hata kama kwa shingo upande. Baadae ataanza ku hustle kuingia Europe kama haridhiki na noti za pura

kwani Lazima uoe mkuu ndo UTOKE life
 
Umri ulionao si vibaya ukavumilia kidogo pia kuna nchi hapa hapa Africa unaweza kuishi vizuri tu kama uko Ulaya. Naheshimu mawazo yako maana ndiyo ilikuwa akili yangu tangu namaliza form four Geita (Geseco). Kwa sasa niko kusalimia familia yangu mwezi huu katikati nang'oka tena. Hebu jaribu kuingia Botswana na ukifika tu parangana kuoa demu wa huko harafu ulete mrejesho hapa, mie ndo teknic zilizonifikisha South Africa na sasa sijiiti mzamiaji tena. (sina chats za private for positive reasons) View attachment 411100

ulifikia wapi? au ulipofika ulianzia mtaani tu
 
Back
Top Bottom