Ushauri: Nataka nikaishi Ulaya

Ushauri: Nataka nikaishi Ulaya

Pole sana.

Linapokuja suala la kupewa ushauri uende nchi gani/ipi ni ngumu sana, ujue kwanini?

Kila mtu (namaanisha wale wanaosema kweli wanapokuwa nje) atakujibu kutokana na Maisha yalivyo kwa upande wake.

Tunapokuja kwenye uhalisia ni kwamba, hakuna maisha rahisi popote hapa Ulimwenguni, nenda popote utakapoenda hapa Ulimwenguni changamoto za maisha/kimaisha ni zile zile na zinafanana.

Na ugumu unaongezeka zaidi pale linapokuja suala la Vibali, iwapo hukufanikiwa kupata Vibali vya kuishi hiyo Nchi husika.

Kitu cha kwanza utakapoingia Nchi yoyote ya Ugenini, changamoto kubwa ni Kibali kwanza.

Kwahiyo utakapofanikiwa kuingia popote hapa Ulimwenguni, kaa ukijua changamoto kubwa ni Kibali.

Maisha yamebadilika, Ulaya ya sasa tofauti na Ulaya ya zamani, Vibali vimekuwa vigumu, na machafuko yanayoendelea pande nyingine tofauti, tofauti za Ulimwengu yamechangia kwa kiasi kikubwa kufanya maisha ya Ulaya kuwa magumu, na Wahamiaji wamekuwa wengi sana.

Sikukatishi tamaa, wewe jaribu popote usiogope, kufanikiwa au kutokufanikiwa ugenini kupo, na ni sehemu ya maisha.

Muhimu wewe mwenyewe utakapofanikiwa kuingia Nchi yoyote jitahidi sana kuwa mpiganaji, mafanikio utayaona.

Kila la Kheri
 
kwani Lazima uoe mkuu ndo UTOKE life
Nafikiri kamaanisha Makaratasi.

Kuna zile ndoa za Mchongo, mnakubaliana na Demu umlipe kiasi kadhaa (mtakachokubaliana) cha Pesa, inakuwa ni Biashara sio ndoa, na mara nyingi kila mmoja anakuwa anaishi Nyumbani kwake, na hakuna mambo ya kuingiliana kimwili, labda itokee tu.

Na ukishapata Makaratasi mnafanya mpango wa kuachana kisheria, kila mmoja anaendelea na maisha yake
 
Msaada wakuu,

Bongo kwangu tafrani,

Nimetumia kila njia kufanikiwa na kujituma sana katika maisha ya hapa Tanzania na sijafanikiwa.

Kama kusoma nina Diploma IT,
Kama biashara nishafanya bila mafanikio.

Nimeona nitafute nchi nyingine nihamie,
Niko tayari kufanya kazi yoyote huko.

Ushauri wenu wakuu niende nchi gani Ulaya ambapo ndoto zangu nitazifanikisha.
Jichunguze kwanza ujue udhaifu wako!
Kama shida ni wewe na si system, hata huende mbinguni hutofanikiwa!
Taaluma yako bado ipo chini, Diploma ya IT hata kwa Tanzania bado haitoshi.
Kikubwa hapo utaishia kuwa mzamiaji tu nchi yeyote utakayoenda hata ikiwa Kenya!
Ushauri, kabla ya kufikiri ulaya, uliza opportunities kwa mtu wa IT hapa nchini!
itakuwa rahisi kwako na hutopoteza muda kama haya maandalizi yako ya kwenda Ulaya.
 
Nashukuru sana mkuu,
niko teyari kukabiliana na changamoto yoyote.
ushauri wako ntauzingatia sana.
 
kwani Lazima uoe mkuu ndo UTOKE life
Kwa mimi nisie na elimu ilikuwa njia simple sana kwangu. Ogopa sana life la South Africa kama huna uhakika wa kula na sehemu ya kulala hata kama una midegree kama Lipumba. Unapokuwa na sehemu ya kufikia ni rahisi sana kufuatilia mambo yako ukiwa umetuliza akili tofauti na hivyo utajiingiza katika biashara hatari ili mradi ule na kulala
 
ulifikia wapi? au ulipofika ulianzia mtaani tu
Mimi nilikuwa na uhusiano na raia wa nchi mbili mmoja Msouth na mwingine Mbotswana hivyo sikufikia mitaani. Botswana naendaga kupiga story tu weekend maana ni kama Dar na Moro vile
 
Nafikiri kamaanisha Makaratasi.

Kuna zile ndoa za Mchongo, mnakubaliana na Demu umlipe kiasi kadhaa (mtakachokubaliana) cha Pesa, inakuwa ni Biashara sio ndoa, na mara nyingi kila mmoja anakuwa anaishi Nyumbani kwake, na hakuna mambo ya kuingiliana kimwili, labda itokee tu.

Na ukishapata Makaratasi mnafanya mpango wa kuachana kisheria, kila mmoja anaendelea na maisha yake
Absolutely utafikiri na wewe ni mzamiaji. Mimi naweza kusema nilikuwa na bahati fulani hivi lkn ni sababu ya tabia yangu, mara ya kwanza kabisa nilikumbana na limama limoja likaniambia hilo jambo eti ili upate vibali sharti unioe then wewe utaamua aidha tuendelee ama la, sasa mkuu huyo mama hakufahamu kama hapo nilipo pia nalelewa na pia nikaona kuwa ananihadaa kwa faida yake lkn hii komenti yako imeshahibiana kabisa na hilo tukio. Tatizo kubwa sana katika hili ubahatishe maana wanawake wa South Africa hawaishi kwa kudra za mme hivyo kukufurusha ni kugusa tu na wengi wameachika sababu ya ku adopt tabia za makaburu.
Hiyo ndiyo njia pekee ya kupata makaratasi atake asitake
 
Mimi nilikuwa na uhusiano na raia wa nchi mbili mmoja Msouth na mwingine Mbotswana hivyo sikufikia mitaani. Botswana naendaga kupiga story tu weekend maana ni kama Dar na Moro vile
mkuu unakumbana na changamoto gani kubwa huko?
 
mkuu unakumbana na changamoto gani kubwa huko?
Changamoto zipo tu hasa ubaguzi kwa vile hawa jamaa hawapendelei Kiingereza isipokuwa lugha zao za asili sasa hata ukitaka kuvunga si mgeni utaumbuka tu kwa lugha ila nashkru mungu kuna wale wa Zimbabwe hawana nouma kivile lkn changamoto kubwa kabisa ni kuwa mbali na familia yangu harisi ndo sababu nikakuambia una mazigira mazuri sana ya kuzamia maana hujaoa
 
Inspector Harun..babuuuuu..hujawahi kusikia mtu kalala na njaa ndani ya Paris Ufaransaaa au sababu ni jiji la maraha ndo watu hawalambi garasaaa!!?
 
Msaada wakuu,

Bongo kwangu tafrani,

Nimetumia kila njia kufanikiwa na kujituma sana katika maisha ya hapa Tanzania na sijafanikiwa.

Kama kusoma nina Diploma IT,
Kama biashara nishafanya bila mafanikio.

Nimeona nitafute nchi nyingine nihamie,
Niko tayari kufanya kazi yoyote huko.

Ushauri wenu wakuu niende nchi gani Ulaya ambapo ndoto zangu nitazifanikisha.

Nenda sehemu moja inaitwa MAKING-LOSS {au Makongolosi};Ukifika pale kuna eneo LA makazi linaitwa "UGERMANI".Pale utawakuta watu wakijishughulisha na machimbo ya dhahabu na kilimo cha mahindi kama ukipenda. Vile vile ktk mji ule wa MAKING LOSS kuna eneo wanaliita "JAMAICA" Kule wanalima tumbaku kwa kwenda mbele.

Ukichagua kati ya maeneo tajwa hapo juu, Natumai utatoka kimaisha
 
Ingia you tube andika suprising europe utapata majibu yote nna uhakika
 
Jichunguze kwanza ujue udhaifu wako!
Kama shida ni wewe na si system, hata huende mbinguni hutofanikiwa!
Taaluma yako bado ipo chini, Diploma ya IT hata kwa Tanzania bado haitoshi.
Kikubwa hapo utaishia kuwa mzamiaji tu nchi yeyote utakayoenda hata ikiwa Kenya!
Ushauri, kabla ya kufikiri ulaya, uliza opportunities kwa mtu wa IT hapa nchini!
itakuwa rahisi kwako na hutopoteza muda kama haya maandalizi yako ya kwenda Ulaya.
Elimu kubwa ni kipaji cha mtu kusoma huko ni kuendeleza tu hicho kipaji ndio mana utaona watu wasio hata na cheti na wanafanakiwa sana.
Cheti au Astashahada mtu akipata hii ni kubwa na kama amepata elimu bora ni mtaji tosha sio haba kama unavyofikiri.

Wengi huona astashahada au stashahada ni elimu ndogo sababu mhitimu anakuwa amepata bora elimu na utata huanza hapo. Nina kaka yangu alisomea astashahada lakini ilikuwa ni elimu bora na sasa yupo abroad na ni fundi wa kutegemewa ana kipato kizuri.
Ukidharau hii nitakuonesha aliye na shahada za bora kusoma sample ya zile zitolewazo Tanzania na anasota naye utamwambiaje?

Mtoa mada nikuulize kwenye Information Technology umebase katika nini? Hata ukipata kazi unaeza fanya kwa ubora?
 
Back
Top Bottom