Ushauri: Nataka kuhamia Tanga

Ushauri: Nataka kuhamia Tanga

Habari wakuu na wadau wa jf,hope mko fine.

Mimi ni kijana mwenye miaka 38+ naishi mkoa wa Shinyanga kunakosifiwa kwa wingi wa madini japo mimi pesa ya madini siifaidi kabisa pamoja na kujihusisha kwa muda wa miaka mwingi.

Nina familia ya mke na watoto 3,sasa nimekaa nikafikiri nakuona nihamie moja ya mkoa ambao ni Tanga ila natamani kupata mengi zaidi kwa wenyeji au wanaojua hali,tamaduni na maisha ya huko kwa ujumla nijue pakuanzia.

Kwanini nimeichagua Tanga,ndugu zangu wengi walikimbilia Dare-ssalam japo na wao maisha yamewakaba yani hadi kuna muda naona bora hata mimi maana kuna muda inabidi mimi ndiyo niwapige tafu mambo yakiwagomea.

Naombeni msaada wa mawazo pia wenyeji mnisaidie kutambua fursa na uhalisia wa mkoa huo,binafsi ni mchapakazi na sichagui kazi labda iwe ya kushusha utu wa mtu tu🙏
IMG_20220225_230439.jpg
 
Ujiandae kuwa na mchepuko, hii ni kama formula.. korogwe kutakufaa, gharama za maisha zipo chini. Kila la Kheri mwanazengo
 
Ingekuwa vizuri Ukampata MTU ambaye ni mgeni mwenyeji ambaye yupo huko na anafanya biashara .

Hii itakupa picha kamili either uende au usiende.

Kuhusu kutoboa nafikiri is game of chance unaweza kwenda Wewe ukatoboa na wengine wakashindwa kabisa kutoboa .
 
ndg yangu nipo tanga mwaka wa kumi huu kikazi napambana sana kuhama .hakuna fursa huku usijaribu kuja tanga
 
Kama unapenda kilimo basi Korogwe na Lushoto patalufaa sana maana mvua ni nyingi huko, maji ni mengi... Muheza ukalime mazao ya biashara, Katani nk.. Tanga Jiji pale labda tukafanye biashara mabanda ya Papa mkagombaniane wateja.
Tanga sio pabaya kama una mishe za kufanya
 
Habari wakuu na wadau wa jf,hope mko fine.

Mimi ni kijana mwenye miaka 38+ naishi mkoa wa Shinyanga kunakosifiwa kwa wingi wa madini japo mimi pesa ya madini siifaidi kabisa pamoja na kujihusisha kwa muda wa miaka mwingi.

Nina familia ya mke na watoto 3,sasa nimekaa nikafikiri nakuona nihamie moja ya mkoa ambao ni Tanga ila natamani kupata mengi zaidi kwa wenyeji au wanaojua hali,tamaduni na maisha ya huko kwa ujumla nijue pakuanzia.

Kwanini nimeichagua Tanga,ndugu zangu wengi walikimbilia Dare-ssalam japo na wao maisha yamewakaba yani hadi kuna muda naona bora hata mimi maana kuna muda inabidi mimi ndiyo niwapige tafu mambo yakiwagomea.

Naombeni msaada wa mawazo pia wenyeji mnisaidie kutambua fursa na uhalisia wa mkoa huo,binafsi ni mchapakazi na sichagui kazi labda iwe ya kushusha utu wa mtu tu🙏
Usiende na mkeo kwani utampa shida sana utakapofichwa.
 
Kama unapenda kilimo basi Korogwe na Lushoto patalufaa sana maana mvua ni nyingi huko, maji ni mengi... Muheza ukalime mazao ya biashara, Katani nk.. Tanga Jiji pale labda tukafanye biashara mabanda ya Papa mkagombaniane wateja.
Tanga sio pabaya kama una mishe za kufanya
Mkuu kilimo gani lushoto kinafaa Kwa mazao ya chakula ukiondoa mazao ya biashara kama katani. je? mashamba yanapatikana Kwa bei gani?
 
Mkuu kilimo gani lushoto kinafaa ikiondoa mazao ya biashara kama katani. je? mashamba yanapatikana kirahisi?
Tanga bado pana fursa inategemea unataka kufanya nini, ardhi bado ni bei rahisi, kama wilaya ya mkinga inayokaliwa na Wadigo ambao kwa asili sio wakulima ardhi bikira ni nyingi tu, maeneo kama ya maramba kokoa inakubali na jkt walikuwa wanalima,lanzon mahindi yanakubali sana, mihogo na machungwa yanakubali sana tu kuanzia kibiboni mpaka duga. Nenda ukalime manga uwauzie wachina,wanahitaji sana unga wa muhogo.Manza bay kuna ardhi yenye rutuba sana, mbuluni kwa Warundi, Kilulu etc, upande wa kwenda Jesan kuanzia pale Mayomboni mpaka Jesani koroshi na katani inakubali sana, na wagerman walikuwa na estate kubwa sana, mpaka reli na kota za wafanyakazi enzi za mkoloni kabla mjeruma hajaondoka tz zilikuwepo na yamebaki magofu tu Totohovu pana visima walichimba wajeruman na mapaka leo vina maji, nenda kaanzishe mashamba huko mkuu, pwani za kutrngeneza majaruba ya chumvi zipo,ukitaka pia kalimwe mwani maeneo ya Kijiru na Moa mpaka kwale na Mongavyeru
 
Mkuu unga wa mhogo soko lipo wapi? Nionganishe ninamihogo ya kutosha
 
Habari wakuu na wadau wa jf,hope mko fine.

Mimi ni kijana mwenye miaka 38+ naishi mkoa wa Shinyanga kunakosifiwa kwa wingi wa madini japo mimi pesa ya madini siifaidi kabisa pamoja na kujihusisha kwa muda wa miaka mwingi.

Nina familia ya mke na watoto 3,sasa nimekaa nikafikiri nakuona nihamie moja ya mkoa ambao ni Tanga ila natamani kupata mengi zaidi kwa wenyeji au wanaojua hali,tamaduni na maisha ya huko kwa ujumla nijue pakuanzia.

Kwanini nimeichagua Tanga,ndugu zangu wengi walikimbilia Dare-ssalam japo na wao maisha yamewakaba yani hadi kuna muda naona bora hata mimi maana kuna muda inabidi mimi ndiyo niwapige tafu mambo yakiwagomea.

Naombeni msaada wa mawazo pia wenyeji mnisaidie kutambua fursa na uhalisia wa mkoa huo,binafsi ni mchapakazi na sichagui kazi labda iwe ya kushusha utu wa mtu tu🙏
Kama unaweza kilimo uje wilaya za Kilindi au Handeni, baada ya miaka 3 nauhakika utakua kutoa ushuhuda juu ya mafanikio hapa
 
Back
Top Bottom