Ushauri:-Nampenda ila hili linaniwia gumu.

Ushauri:-Nampenda ila hili linaniwia gumu.

.sikia si wote wanaopata watoto mapema huwa wamekosa utulivu au watakosa utulivu siku za usoni, ulimwengu huu una changamoto nyingi mkuu, kuna sehemu watu huteleza na ashukuriwe Mungu kwa wanaoweza kurejea hali zao za kawaida kama huyu dada uliyenaye, kwanza mkweli na ndo mana akakupa sababu ya we kubemebeleza mwaka mzima kuhusu suala la ndoa, na ndani ya huo mwaka ndo mana ukatambua wazi kuwa wampenda kweli. Nachofahamu ndoa/harusi itakuwa kati yako na huyo dada (hapa huoi mtoto wake) na zaidi ya yote mkiweka mikakati mizuri huyo mtoto nakwambia atakuja kuwa BARAKA kwako..

Duh aksante ngoja nlfanyie kazi.
 
angalia sana kuoa mtu mwenye motto kuna shida zake...uwe makini sana
 
Note hiyo
 

Attachments

  • 1392475435135.jpg
    1392475435135.jpg
    28.3 KB · Views: 143
namaanisha hivi usione ugumu wa kumuoa mwenye watoto/mtoto kuliko mwenye historia ya kutoa mimba zaidi ya moja,,tena wanawake wenye watoto wakiolewa wanadumu maana anaona ni chance pekee ya kuwaprv wrng watu waliokua wanadhani hata olewa NB:sina mtoto ila nimeona kitu kama hicho pia kama hajakuzidi umri hakuna gumu hapo kama ni mtot unnaweza ukaamua akae kwa bibi yake kwa muda baadae mkishazoea ndoa mnaweza mkamchukua

Kwan tunauhakika gani hajatoa?!
 
Mwambie mungu asante umepata anaesema ukweli. Wengine utamuoa hana mtoto lakn alishaharibu mimba za kutosha hata mimba hashiki tena, mayai yameisha. Huyo ndie mke sasa.

Well said mkuu... Kuna dada mmoja aliolewa lakini akaficha kuwa tayari ashazaa watoto 6. huwezi amini mwanaume alimuamini ila mwisho wa siku alipogundua it was too late ukizingatia washafunga ndoa ya kikristo. It was so painful na hii huwa inapunguza upendo na uaminifu katika ndoa!!!
 
kwa dunia ya sasa hakuna ambaye si used si mwanamke wala mwanaume ww mwenyewe huko ulikopita wangekuwa wanakubali kubeba mimba zako ungekuwa na watt wangapi? so usimuhukumu mwenzio kama vp chukua mzigo weka ndani
 
Asante mkuu,nampenda kweli naye pia ananpenda najua.
Una bahati kwa kua huyu kakueleza ukweli kua kazaa. Kama kweli unampenda, mtoto hawezi kuwa kikwazo. Kubalianeni namna ya kumlea. Unaweza kumwacha huyu na kuoa asie na mtoto, still akawa na upungufu mwingine ambao ni kikwazo kwako. Dunia ina mengi hii.
 
1. Mmekuwa katika mahusiano kwa muda gani?

2. Kwa nini suala la mtoto kachelewa kukujulisha?

3. Mtoto alimpata ndoani au alizaa tu na mwanaume baki?

4. Ni ipi nafasi ya baba wa mtoto kwa mtoto au mwanamke huyo?
 
  • Thanks
Reactions: Luv
Inaonekana wewe hujui hata maana ya mke ni nini

Mtoto sio kikwazo kama nyote mtaamua kuwa wawazi kwa kila mmoja wenu

Ni kitu gani kinakufanya unakufa moyo?

Kama ni majukumu unajuwa ili uwe mwanaume ni hadi iweje

Au ukiwa na 1200 tu unajiona ni mwanaume?

haaahaaaa!
umenikumbusha mbaaaali!
hata akiombwa hela anasema ana 1200 tu. mwombaji akiomba 200 hukataa kutoa, eti hana hela kabisa
 
Masai dada yakupata vzr,hebu fafanua kidogo.

Anachomaanisha ni kuwa kipi ni bora kati ya kuwa na mtoto au angekuambia aliwahi toa mimba(anamaanisha angetoa mimba ya huyo mtoto)chagua moja fanyia kazi
 
Ndo maana wadada wengine huamua kufanya siri kwa wachumba zao kuhusu watoto waliozaa na ma ex wao
kwa sababu wakisema huachika na wachumba zao.
ukishamwoa tu unaanza kusikia kuwa ana mtoto.
ukimuuliza anakuambia ukweli huku akijitetea kuwa aliogopa kusema mapema
kwa hofu ya kuachwa.

mtafute msiri atakufaa zaidi.huyu hakufai kabisaa.
angeacha uje kujua mwenyewe siku katoto kake(kalikofichwa kwa wazazi wake muda wote wa mahusiano yenu) kanapomwita mkeo MAMA mbele zako.
 
1. Mmekuwa katika mahusiano kwa muda gani?

2. Kwa nini suala la mtoto kachelewa kukujulisha?

3. Mtoto alimpata ndoani au alizaa tu na mwanaume baki?

4. Ni ipi nafasi ya baba wa mtoto kwa mtoto au mwanamke huyo?

1.Tokea nimfahamu ni miezi ni miezi nane ila kwenye mahusiano ni mi4. 3.Aliza na mwanaume tu sio kwenye ndoa na alikuwa na miaka 17 kipndi hcho. 4:Baba hanashuguli na mtoto sema ndugu zake ndo wanamjali mtoto pamoja na mama wa huyu mwanaume ila yeye hatoi chochote.
 
Ndo maana wadada wengine huamua kufanya siri kwa wachumba zao kuhusu watoto waliozaa na ma ex wao
kwa sababu wakisema huachika na wachumba zao.
ukishamwoa tu unaanza kusikia kuwa ana mtoto.
ukimuuliza anakuambia ukweli huku akijitetea kuwa aliogopa kusema mapema
kwa hofu ya kuachwa.

mtafute msiri atakufaa zaidi.huyu hakufai kabisaa.
angeacha uje kujua mwenyewe siku katoto kake(kalikofichwa kwa wazazi wake muda wote wa mahusiano yenu) kanapomwita mkeo MAMA mbele zako.

Hiyo ndio mbaya zaidi mkuu,bora amesema mapema.
 
Ndo maana wadada wengine huamua kufanya siri kwa wachumba zao kuhusu watoto waliozaa na ma ex wao
kwa sababu wakisema huachika na wachumba zao.
ukishamwoa tu unaanza kusikia kuwa ana mtoto.
ukimuuliza anakuambia ukweli huku akijitetea kuwa aliogopa kusema mapema
kwa hofu ya kuachwa.

mtafute msiri atakufaa zaidi.huyu hakufai kabisaa.
angeacha uje kujua mwenyewe siku katoto kake(kalikofichwa kwa wazazi wake muda wote wa mahusiano yenu) kanapomwita mkeo MAMA mbele zako.

Ushauri feki huu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom