Ushauri: Nahitaji kuanzisha biashara ya sigara

Ghadaf

JF-Expert Member
Oct 15, 2016
679
1,000
Waheshimiwa baada ya mapambano makali sana. nimefanikiwa kupata mtaji wa shilingi milioni nne. Sasa kutokana na mimi mwenyewe kuwa mvutaji wa sigara. Nimefikiria kufanya biashara ya sigara kwa jumla na reja reja. Naomba kama kuna mwenye ufahamu kuhusu biashara hii anipe muongozo .
  • Box moja la sigara kiwandani linauzwa bei gani?
  • Box moja la sigara kwenye maduka linauzwa bei gani?.
Pia nina kipikipiki changu ambacho nimepanga kukitumia kupeleka bidhaa kwenye maduka. Yaani nakua nawapelekea mwenyewe. Badala ya kusubiri wateja wanifate.

Msaada wenu wakuu kwa anaefahamu kuhusu biashara hii na changamoto zake.

Nimefikiria hii baada ya kuona watumiaji wa sigara huku mtaani tumekua wengi.

Naomba kuwasilisha.

1620386806319.png

 

Ghadaf

JF-Expert Member
Oct 15, 2016
679
1,000
Usifanye biashara inayohusiana na uraibu wakati wewe mwenyewe ni muhanga.

Kama ni mvuta sigara biashara ya sigara si ya kufanya na kama ni mnywaji wa Pombe usifanye biashara ya baa/ grosary nakuapia faida yote utaimaliza na mtaji utatetereka mkuu.
Mkuu mimi navuta sigara kali. Inauzwa shilingi mia. Na navuta nne tu kwa siku.
 

Johnny Impact

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
2,664
2,000
Kiukweli idadi ya wavuta sigara inaongezeka kila siku. Nilikuwa namsaidia jamaa yangu kuuza duka. Sigara zinanunuliwa kuliko Unga au mchele.
 

muddy1345

Member
May 21, 2015
67
125
Nahisi unaomba uwakala toka kampuni ya sigara. Wakuletee mzigo usambaze. Sasa kutakuwa na vigezo vyao unatakiwa uvijue kwanza
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom