Ushauri: Nahitaji kuanzisha biashara ya sigara

Uswiss

JF-Expert Member
Oct 15, 2016
842
2,159
Waheshimiwa baada ya mapambano makali sana. nimefanikiwa kupata mtaji wa shilingi milioni nne. Sasa kutokana na mimi mwenyewe kuwa mvutaji wa sigara. Nimefikiria kufanya biashara ya sigara kwa jumla na reja reja. Naomba kama kuna mwenye ufahamu kuhusu biashara hii anipe muongozo .
  • Box moja la sigara kiwandani linauzwa bei gani?
  • Box moja la sigara kwenye maduka linauzwa bei gani?.
Pia nina kipikipiki changu ambacho nimepanga kukitumia kupeleka bidhaa kwenye maduka. Yaani nakua nawapelekea mwenyewe. Badala ya kusubiri wateja wanifate.

Msaada wenu wakuu kwa anaefahamu kuhusu biashara hii na changamoto zake.

Nimefikiria hii baada ya kuona watumiaji wa sigara huku mtaani tumekua wengi.

Naomba kuwasilisha.

1620386806319.png

 
Usifanye biashara inayohusiana na uraibu wakati wewe mwenyewe ni muhanga.

Kama ni mvuta sigara biashara ya sigara si ya kufanya na kama ni mnywaji wa Pombe usifanye biashara ya baa/ grosary nakuapia faida yote utaimaliza na mtaji utatetereka mkuu.
 
Kiukweli idadi ya wavuta sigara inaongezeka kila siku. Nilikuwa namsaidia jamaa yangu kuuza duka. Sigara zinanunuliwa kuliko Unga au mchele.
 
Nahisi unaomba uwakala toka kampuni ya sigara. Wakuletee mzigo usambaze. Sasa kutakuwa na vigezo vyao unatakiwa uvijue kwanza
 
Sina uhakika km M4 kinatosha au hakitoshi kupewa uwakala. Km hakiwezekani, ongea na ambae amepewa uwakala mkubaliane wenyewe bila kampuni kuhusika
Sawa sawa mkuu. Ngoja niingie mtaani
 
Kweli kabisa afanye hiyo inayomuwahisha
Location niliyopo matunda ni mengi sana. So supply ni kubwa kuliko demand. Nilimjibu jamaa kutokana na mazingira niliyopo. Mawazo yako ni muhimu pia financial services karibu..
 
Nmecheka sana, ila hapo mkuu ongezea na pombe kali hizi za bei ndogo zilizowekwa kwenye chupa za plastic zinalipa sana uki mix na hii ya sigara

Nakuhakikishia hautachelewa kabisa
Ushauri wako nimeupokea mkuu. Ka mtaji kakikua inabidi nijiongeze. Hayo mambo ya matunda ni biashara za kina mama.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom