Ushauri: Mume wa mtu niliyezaa naye watoto watatu amefariki na ameacha mali nyingi, nifanyaje kudai haki za wanangu pasipo Mume wangu kujua?

Huko mlipo hakuna wauza mkaa,

Wanaume tunapachikwa jina la ukatili lakini niwaibie siri sisi ni watu wa utaratibu tu. Utaratibu usipofuatwa na kuzingatiwa ni kujiandaa kwa lolote.
 
Ana akili za kuchepuka kwa tamaa, ila hakuwa na akili za kuhakikisha mali zinakuwa zake hata kwa kuuziwa kiuongo na huyo mchepuko. Ndio dhambi yako imemtafuna kwa akili tangu mwanzo.

Pambana na khali yako labda binti yake akubali kufanya DNA. Hata kuweka savings account hukuweka. Ukome
 
Ndoa yangu ina miaka 12 mimi na mume wangu hatuna shdia, kabla ya mume wangu kuna mwanaume nilikua naye, alikua ni mume wa mtu, nilibeba mimba yake nilipomuambia akaikataa,

Kwakuwa kupindi hicho ndiyo nilikua nimeanza mahusiano na mume wangu nilibambikizia mimba na akanioa.

Baada ya kuolewa yule Baba alirudi akaomba msamaha na kusema yuko tayari kuhudumia mwanae hata kama atatumia jina la mume wangu.

Basi nilimkubalia na tangu kipindi hicho alikua anahudumia mwanae kwa kila kitu.

Kwakua alikua ananijali na kipato chake ni kikubwa basi nilijikuta narudiana naye, nikabeba mimba yake ya pili, nilimuambia mume wangu ni yake naye akawa anahudumia ila bado yule baba aleindelea kujali wanae mopaka kuwasomesha,

Mume wangu kipato ni cha kawaida ila mimi nafanya kazi pia, anajua nchukua mikopo kwaajili ya ada lakini ukweli Baba yao ndiyo anawasomesha.

Niliamua kumazalia mume wangu mtoto mmoja ambaye ndiyo mwanangu wa tatu, lakini mtoto wangu wa nne ni wa yule Baba.

Baadahi ya ndugu zake alishawatambulisha na wanajua watopto wao kwani nilishawapeleka kwa Dada yao.

Mwaka jana alianza kuumwa na mwezi huu mwanzoni alifariki dunia. Nilienda kwenye msiba kama watu wengine,

Sababu ya kuja kwako ni hivi, Baba wa wanangu kaacha mtoto mmoja tu na mke wake, lakini ana mali nyingi sana, ana nyumba 9, magari ya mizigo zaidi ya kumi na vitu vingi.

Nimefuatilia na kugundua kuwa hakuacha wosia inamaana mali zake nyingi zimebaki kwa mwanae aliyezaa na mke wake kwani ndugu nao wana mali zao hawhaangaiki naye.

Natamani kwenda kudai haki za wanangu kwani kwakua dada yao ananifahamu na anawafgahamu watoto wa Kaka yake naamini nitapata.

Hofu yangu ni kama huyo mke wake atakataa na kusema hanitambui, nahofia kama ikiwa kwenda mahakamani labda mume wangu atajua.

Kusema kweli nimechanganyikiwa, ndoa naitaka lakini mnikiwaza haki za wanangu natamani kwend ahata mahakamani, mimi ndiyo napaswa kupata kikubwa kwani nimemzalia watoto wa 3 wakati mke wake ana mmoja tu!

May be an image of 1 person and plaits

Utaishia kupoteza na ndoa. Hesabu hasara tu. Hiyo tamaa ya mali uliyonayo itakuua, mama ungekuwa mchepuko usiye na ndoa ingekuwa rahisi ila kwa hali yako hiyo, unataka kufa na watoto hao pia inaonekana huwapendi.

Huo mpango uta backfire vibaya mno na utakuja kujuta. Chukua hamsini zako tu.
 
Ukitoa mahala andika wapi umetoa, ilo ijulikane wewe sio mwandishi wa haya. Labda kama ni wewe muhusika humu Jamiiforums.
 
Wanaume wote wenye watoto wanne,mke mfanyakazi,mmoja wenu ndo huyo aliyepigwa
 
Tulia...unakoelekea utakosa vyote kwa pamoja, una mume tunza ndoa yako hayo mengine sahau.

Unataka kudai mali kama nani?

Tumia akili
Hivi unafikiri ataelewa na uroho wa mali ushamuingia.

Pia akifikiria majukumu yote yanamuangukia wakati mwanzo alikuwa anaishi bila stress sasa anatakiwa apambane watoto wasome tena ukute walikuwa wanasoma shule za gharama.

Ila pia alikuwa mzembe wewe unajua kabisa mtu ana mke wake wa ndoa kwanini hakumuomba awekeze kwa wanae yeye awe msimamizi.
Pagumu hapa.
Halafu hii story sidhani kama ina uhalisia

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Mm huwaga nasema nitaua mtu haya mambo nilelee mtoto afu nijue sio wangu ww mwanamke unakufa na mm nakufa
 
Duuh...! Kuna watu mna tamaa duniani. Nafikiri umesahau msemo usemao “MTAKA VYOTE KWA PUPA.............
 
Back
Top Bottom