Kila nikileta beki tatu mume wangu anatembea nao, nimechoka

george aloyce

JF-Expert Member
Aug 22, 2017
1,177
1,823
Mimi ni mama wa miaka 40, ninafanya kazi na nina kipato kizuri tu. Sababu ya kuja kwako kaka ni kwamba mume wangu ni malaya sana, ni mtu wa wanawake na hahudumii familia, kila kitu nafanya mimi. Nimejitahidi, nimekopa mpaka nimejenga mimi, ingawa kiwanja kina jina lake. Nilifanya kosa hilo kwa sababu nilikuwa sijakujuwa, hivyo nilinunua kiwanja kwa jina langu.

Lakini tuligombana, akaenda kushitaki nyumbani kwetu ambapo waliniambia kila kitu kinatakiwa kuwa kwa majina ya mume wangu kwa sababu mimi ni mke tu na yeye ndiyo baba, kichwa cha familia. Kila mtu alikuwa upande wake, akatishia kuniacha hivyo nikaamua kubadilisha majina, nikaandika majina yake ingawa hata katika ujenzi hakuchangia kitu chochote, kila kitu nilifanya mimi mwenyewe mpaka kukamilisha.

Wakati huo huo hahudumii familia. Nikimuuliza ananiambia kuwa kama nataka ahudumie familia basi niache kazi, niwe mke wake, nifanye kazi za nyumbani, atahudumia. Mimi nilikataa kuacha kazi, sababu ya kuja kwako ni hivi: Mume wangu anachepuka sana, ana watoto zaidi ya kumi nje, anazaa na wanawake na anawatelekeza. Kila mwanamke anayekutana naye anamuambia kuwa amegombana na mke wake na wanakaribia kuachana.

Anampeleka mpaka kwao na kumuahidi vitu vingi, wengi ni mabinti wa chuo, anawazalisha na kuwaacha, ila kuna baadhi ambao humtelekezea watoto ambao anakuja kuniachia mimi. Sasa hivi nina watoto wake sita nawalea, hatoi pesa yoyote, watoto wenyewe ni wadogo, kuna ambaye kaletwa juzi ana miezi sita, ananitaka nimlee. Nikimuambia atoe hata pesa ya mfanyakazi ananiambia kuwa hawezi kuoa mke na kutafuta mfanyakazi kwani mimi nafanya nini.

Nina wafanyakazi wawili ambao nawalipa mimi. Kaka, nimechoka na sijui cha kufanya. Tukigombana kidogo ananiambia kuwa kama nimechoka niondoke, lakini yeye hawezi kuacha kuzaa. Sababu ya kuja kwako kaka ni kwamba, nimegundua kuwa mume wangu anatembea na wafanyakazi wangu wote wawili, tena wananidharau.

Nikimuambia kwanini unafanya hivyo ananiambia ni mimi nimeleta wafanyakazi, kama nataka aniache kutembea nao basi niache kazi, nihudumie watoto wake, la sivyo kila nitakayemleta atatembea naye. Kaka, mimi nina watoto naye wawili tena wakubwa, ila kaniletea watoto sita wadogo. Yaani, nashindwa cha kufanya, ananiambia kama nimechoka niondoke, nimuachie nyumba ambayo nimejenga na pesa yangu. Mpaka sasa nina mikopo, kaka nisaidie nifanyeje? Naishi vipi na huyu mwanaume?
 
Mimi ni mama wa miaka 40, ninafanya kazi na nina kipato kizuri tu. Sababu ya kuja kwako kaka ni kwamba mume wangu ni malaya sana, ni mtu wa wanawake na hahudumii familia....
Kosa ulilofanya unamuendekeza anazaa nje anakuletea watoto ulee mbona utalea hao watoto hadi akili ikukae sawa.

Rudisha watoto kwa mama zao kaa bila wadada wa kazi uone atatembea na nani.
 
Mimi ni mama wa miaka 40, ninafanya kazi na nina kipato kizuri tu. Sababu ya kuja kwako kaka ni kwamba mume wangu ni malaya sana, ni mtu wa wanawake na hahudumii familia, kila kitu nafanya mimi. Nimejitahidi, nimekopa mpaka nimejenga mimi, ingawa kiwanja kina jina lake...
Wewe ni ke au me?

 
Mama nikuambie Kitu tunza risiti zako zote ulizokuwa unafanya manunuzi kipindi unafanya ujenzi wa nyumba Yako, na rekodi yote ya Mikopo ya Mabenki kwa ajili ya ujenzi, kuandikwa kwa jina la mmmeo kwenye Kiwanja siyo tija
Utakuja kunishukuru baadaye
 
Kwani ungeamua kuachika wakati ule alipodai kiwanja ulichonunua kiandikwe jina lake ingekuwa nini! Hayo umeyataka mwenyewe kwa kubembeleza ndoa na hayo ndiyo madhara yake endelea kupambana nayo mwenyewe.
 
Back
Top Bottom