Ushauri: Mume wa mtu ni mume wa mtu; keep out!

Money Penny

JF-Expert Member
Jun 20, 2016
15,758
14,687
Nilikutana na rafkiangu wa Primary, hukjooo Morena Hotel
Tukawa tunafanya catch up tangu Primary mpaka leo!

Nikagundua shogangu bado hajaolewa na bado ana akili kama chiu!

Primary School Friend: Best nakuona kwa mitandao, whatsapp, facebook, blog yako, instagrams, damn girl una instagram ngapi?!
Alafu sikuizi unaitwa Money Stars, hataree mimi nimekuzoea jina la ….?

Money Penny: hahahahha niacheeeee! Na wewe? Hubby na watoto hawajambo?

Primary School Friend: Sijaolewa best nipo tu

Money Penny: awkay, shemeji hajambo lkn?

Primary School Friend: Sina shemeji kama unavyodhani, nipo na mtu..

Money Penny: Mtu hajambo?
Primary School Friend: nadhani hajambo, sijaonana nae nina wiki 3

Money Penny: oh kwanini? Mmegombana?

Primary School Friend: Ameoa
Money Penny: ha?

Primary School Friend: It’s complicated! Lakini wamegombana na mkewake, ndoa yao haipo vizuri kivile wanataka kupeana talaka ila bado hawajapeana

Money Penny: Mume wa mtu umekuwa nae kwa muda gani ?
Primary School Friend: Miaka 3
Money Penny: Na amekuahidi ndoa?

Primary School Friend: Ndio lakini bado anafanya process ya talaka.
Money Penny: Miaka 3 ana process talaka?

Primary School Friend: I know right? Najua ni muda sasa ndio maana nagombana nae kila siku..

Money Penny: Mami una umri gani?

Primary School Friend: Nina 33

Money Penny: Huna bwana mwingine?

Primary School Friend: Sina, huyo ndio kila kitu kwangu, amenipangia nyumba, kaninunulia gari, kanitafutia kazi, naanzaje sasa kumsaliti na kumuacha?

Money Penny: ok kwahiyo wewe unatakaje au unataka kumzalia hupendi kuolewa au?!

Primary School Friend: siwezi kumzalia mpaka anioe! Kuolewa nataka sana. Nishauri unaonaje mami?

Money Penny: okay! Unataka nikushauri?

Primary School Friend: ndio best

Money Penny: Best ukinichukia sawa tu lakini Mume wa mtu ni Mume wa mtu, haijalishi wanagombana na mkewe au hawagombani, haijalishi kakununulia Mbingu au Dunia, haijalishi atampa mkewe talaka au la, haijalishi unambinukiaje kitandani au unampaje mechi za kichokoraa na mkewe hampi bado ni mume wa mtu

Tuchukulie mfano huyu mume wa mtu ndio mume wako, alafu ana mwanamke nje kamfanyia yote aliokufanyia wewe, na una watoto wanasoma kayumba, haachi hela ya msosi, ada, unapanda daladala na kimada amenunuliwa BMW, hujui misingi ya ndoa yao ilianzishwa kama ni kwa Mungu au shetani hujui! Utajuaje kama wewe sio Msukule wa huyo jamaa!? Maana sikuhizi vijana wengi wamejiunga free mason kupata pesa chap chap!

Primary School Friend: God forbid!

Money Penny: God hawezi kukusaidia hapo, huyo mwanaume anakupotezea muda, achana nae na umri wako unaenda, sawa kakuchuja ujana wako lakini malipo yako ni nyumba, gari, kazi na safari nyingi za ulaya kama ulivyosema, plz tafuta bwana mwingine usonge mbele hapo unapiga mark-time tu best unang’ang’ana na mwanaume alieshikilia hatima yako wa nini?

Primary School Friend: Kweli, lakini nampenda sana jamani sijui naondokaje?!

Money Penny: Uende kwa Kanisa wakakuombee kwanza, utashangaa Mungu atakutendea muujiza utaondoka mwenyewe bila yeye kukufukuza!

Nikamwangalia huyu shoga anajiuma uma kwenye mawazo nikaona huyu mbululaz wa mwisho, huenda kapuliziwa dawa!
Wadada naombeni tuwe wa kweli wa nafsi zetu tusipende kujifunga funga na kujifariji, tena hawa wwanaume wenye ndoa za Kikristo kuacha mke ni ngumu sanaaa, talaka ngumu jamaa – talaka maanake pasu kwa pasu ya mali na watoto hamna mwanaume anaetaka ku-rist hayo labda umloge!
Bora wale nduguzetu wanaooa wake 4 kidogo unaweza jipa matumaini ingawa nako pagumu!
Eti mimi nikavae Juba! Ahahahahha na umini akavae nini? Orijino Indian Hair avae nani? Gucci avae nani? Levi avae nani? Christian louboutin shoes avae nani?
Nyie mademu wa kiTanzania mnahitaji ku-chill, sijui ni trendy au wanajazana ujinga sijaelewa! Vitu vipo Obvious lakini watu wamo tu!
Akyanani, acha aendelee kutunyoosha tu wengine wamegoma kubadilika!
 
kuna baadhi yawanawake wa tanzania shida sana ....

wamegoma kutumia ubongo wao kwa asilimia 100%

matokeo yake wanatumia kwa asilimia 20% tu alafu hizi 80% zilizobaki wanatupa sisi wanaume ndio tuzitumie kwa niaba yao

yaani inshort wametupa power of attoney ya asilimia 80% ya ubongo wao

kama huyo hapo unayemsemea siyo kwamba akili hana ila tu amekubali kukabidhi akili zake kwa mume wa mtu matokeo yake maamuzi makubwa ya maisha yake yanafanywa na mume wa mtu

anashindwa hata kujiongeza kuwa hapo hakuna ndoa wala nini zaidi ya yeye kuwa kachumbari kwenye ndoa ya jamaa au kwa lugha nyingine yeye ni desert inayoliwa kabla ya mlo mkuu 😂😂😂

Money Penny embu waokoe wenzako asee
 
kuna baadhi yawanawake wa tanzania shida sana ....

wamegoma kutumia ubongo wao kwa asilimia 100%

matokeo yake wanatumia kwa asilimia 20% tu alafu hizi 80% zilizobaki wanatupa sisi wanaume ndio tuzitumie kwa niaba yao

yaani inshort wametupa power of attoney ya asilimia 80% ya ubongo wao

kama huyo hapo unayemsemea siyo kwamba akili hana ila tu amekubali kukabidhi akili zake kwa mume wa mtu matokeo yake maamuzi makubwa ya maisha yake yanafanywa na mume wa mtu

anashindwa hata kujiongeza kuwa hapo hakuna ndoa wala nini zaidi ya yeye kuwa kachumbari kwenye ndoa ya jamaa au kwa lugha nyingine yeye ni desert inayoliwa kabla ya mlo mkuu 😂😂😂

Money Penny embu waokoe wenzako asee
Hahahahha desert on fleet
Nimechekaje huku Dodoma mpaka wananishangaa uuuwi nimemiss Jamii forum like hell man.
Thank u wangu
 
Teh tatizo ni caring ndiyo inawachanganya hao wapenda waume za watu.

Hakuna mdada anayeng'ang'ania mme wa mtu kama huyo mme wa mtu hampi mahela ya kutosha mahitaji yake.

Hata hivyo watakuelewa japo ni wachache sana maana pesa imewatawala sana wadada wengi kiasi cha kufikiri kuwa hawawezi kuingia kwenye ndoa na mwanamme mwenye uwezo mdogo wa pesa.
 
Teh tatizo ni caring ndiyo inawachanganya hao wapenda waume za watu.

Hakuna mdada anayeng'ang'ania mme wa mtu kama huyo mme wa mtu hampi mahela ya kutosha mahitaji yake.

Hata hivyo watakuelewa japo ni wachache sana maana pesa imewatawala sana wadada wengi kiasi cha kufikiri kuwa hawawezi kuingia kwenye ndoa na mwanamme mwenye uwezo mdogo wa pesa.
Shikamoo Pesa Marahaba Mechi
 
Wanawake wa kibongo wastamilivu sana!!mwanamke wa kilami eti wiki 2 hujaonana nae siku ukikutana nae yuko na msela mwingine.anakujibu hawezi kuishi na mtu yupo mbali nae.wenzetu wanahitaji mapenzi zaidi kuliko materials.
Niko na dem wangu wa kitasha hapa maana toka alivyoniambia hivyo siendi tena kwa hadija mnato wa ngaleloo

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom