Ushauri mchumba wangu anatembea na lecturer wake

Ushauri mchumba wangu anatembea na lecturer wake

Best ishu sio lecturer kuwa na mke ishu ni huyo mke wako to be kuwa na mahusiano na lecturer,u know what?akina dada vyuoni hupenda sana vya mteremko kama vile soe offers,kufaulu vizuri na kuonekana kuwa wanatoka maisha bora ili hali ni wanatoka katika familia au koo ambazo ni choka mbaya kinoma,cha msingi huyo mwanamke hakufai kwani ndo tayari kwa lecturer,washwahili husema ukiona manyoya ujue ame.............,cha msingi achana nae na epuka uchumba wa vyuoni.:a s 20:
 
kuna siku nilikuwa nabishana sana humu ndani na C.T.U alileta habari kutoka hukohuko udaku special nikamwambia ungeedit au ungeirepresent tofauti tupate maudhui ila si kama unavyoleta wewe nakumbuka watu wakanishambulia sana walitokaje na povu hata Mamndenyi nae alikuwa mmojawapo.
Haya mambo yanaboa sana
mi nadhani humu ndani ni kwa ajili ya kupeana ushauri kwa mambo tunayokutana nayo au angalau basi waliyokutana nayo watu wetu wa karibu tunawaombea ushauri. na kama tunapiga stori kutaka kupeana mambo ya kufanya issue kama hiyo itakutokea basi tuambizane.
sasa mtu ana-present as if yeye ndo yamemtokea, watu wanachubuka vidole kutoa maushauri kumbe katoa udaku, lol!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mtani wewe ndio kama mimi, ukiona natoa vijembe na post fupi zenye kebehi ujue nisha-google kitambo na kujua source....
Wengine huwa hawanielewi kabisa wakidhani ndivyo nilivyo, kumbe mwenzao nishazoea ulimwengu wa ICT...
Kuna mijitu inayoleta mada humu ni waongo kupindukia...

nimezigundua nyingi sana ndo maana wala huwa sichangii serious, nikiingia ni kuchat tu na siyo kutoa ushauri
hii inaniudhi sana
 
Nahisi kulia, ningekuwa mm nadhan safari ya kigoma kwa bibi ingenihusu ili huyo lecturer anitambue, Lol! Mkuu, jali future yako, ndo mabinti wa Tanzania, ful kushobokea mijihela, na huyo lecturer akijua unaendelea kusalandia atakufanyia hila udisco bure, malizia miezi yako uende na huenda mchumba wako akavuna ka UKIMWI, kuna waschana wengi bwana, endelea kutafuta.
 
Habari za jioni wana JF!!
Mimi ni kijana wa kitanzania, najitokeza hapa mbele yenu kuomba ushauri kwa haya makubwa yaliyonikuta.

Nilianza chuo miaka mitatu iliyopita, nikimaanisha kwa sasa nipo mwaka wangu wa mwisho katika hii kozi ninayoichukua. Nilianza chuo bila kuwa na uhusiano wowote ule wa kimapenzi na msichana hapa chuoni kwa mwaka wote ule wa kwanza.

Hali hiyo ilibadilika baada ya kuingia mwaka wa pili, kwani kipindi hicho kukawa na mwaka wa kwanza wanaingia na bahati nzuri nikatokea kumpenda msichana mmoja mrembo wastani sema ni mstaarabu haswaa. Nilijaribu bahati yangu na mungu si athumani huyu msichana akanikubalia na tukaanza mahusiano yeye akiwa mwaka wa kwanza,mimi wa pili. Tuliishi kwa amani na  furaha kwa kipindi chote kile(nikimaanisha semester zote mbili za mwaka wangu wa pili).

Kinachonifanya kuandika hapa ni hiki sasa, mwanzoni mwa semester iliyopita nilianza kusikia tetesi kutoka kwa marafiki zangu ya kuwa huyu msichana niliye naye anatoka na mmoja wa ma-lecturer wanaomfundisha. Sikuliamini hilo, nikaamua kumuliza mwenzangu kwamba nimesikia hili na hili, je kuna ukweli wowote? Alikataa kata kata na kusema huo sio ukweli na nisiamini kila ninalolisikia, kwa kuwa ni mstaarabu sana na kwa jinsi alivyokuwa akiongea basi nikamuelewa kwa muda ule.

Ila sikuishia hapo nikaendelea na uchunguzi wa chini chini bahati mbaya sikuambulia lolote kuhusu uhusiano wake na  huyo lecturer zaidi ya yeye kuwa na ratiba ya  kwenda kwao kila baada ya wiki mbili kuanzia ijumaa jioni mpaka jumapili ambao ni utaratibu wake toka anaanza chuo. Na hiyo ijumaa mpaka jumapili akiwa nyumbani mawasiliano yalikuwa yakipungua sana kwa sababu alikuwa akisema anakuwa busy sana na shughuli za nyumbani kwao na hata usiku ukimpigia simu alikuwa hapokei kwa madai analala na ndugu yake na kwahiyo atakuwa anampigia kelele.

Leo mchana sasa, nilimpigia simu twende tukapate chakula cha mchana lakini alikataa na kuniambia kuna kazi anaifanya kwanza mpaka aimalize ndio ataenda kula, mimi nikatangulia kwenda kula ila wakati narudi nikakutana na rafiki yangu, akaniuliza mbona nimekutana na bibie(mchumba wangu) anakula na Mr. X (huyo lecturer niliyeambiwa anatembea naye ) sehemu flani(ma-lecturer wengi ndio wanapokula hapo na kama utakuta wanafunzi basi ni mmoja mmoja ambao wako vizuri sana kifedha)… sikuamini, nikaenda kuhakikisha… Nilichokiona aisee sikuamini macho yangu, wote wawili walikuwa wamekaa wakipata lunch tena wakionekana wenye furaha.

Nilimpigia simu lakini hakupokea, aliishia kuiangalia tu simu yake na kuirudisha kwenye meza… Nikamtumia meseji ya kwamba nimemuona na nimezima simu yangu mpaka sasa, hapa natafakari nimfanyaje huyu msichana kwa hili alilonifanyia??? It hurts kwa kweli ikizingatiwa huyu lecturer ana mke kabisa so what if ndio tabia yake hiyo kutemebea na wanafunzi? Si  ndio kuambukizana magonjwa huku??

Naombeni ushauri wenu wana  JF, nimfanyeje huyu kiumbe??
fanya yak0
 
Haha hivi wasoma saa ngapi?manake kutwa kuchwa uko jf afu ukifel test unakimbilia kujikomba kwa lecturer akupe marks za bure grow up, soma knowlegde haiji hivihivi
una hakiri sana!!!halafu yeye anayajua sana maisha ya malecturer utafikiri pekee ndo kapita huko chuo!!
 
Kwani kula chakula na lecturer ndo katembea naye?mbona kawaida saana,au kutopokea simu kwa muda huo akiwa na lecturer ndo ukahisi kuwa tayari anatembea naye?hacha wivu wa ajabu,kama anakupenda utaona outcomes
 
kuna mtu amei-share sijui ndo amei-copy thread yangu kule udaku na kuonekana kama ni story ya kutunga, naomba kuwaambia hii story ni ya kweli na naenda kuonana na huyu msichana muda si mrefu... nitawajuza nitakachoamua kutokana na majibu yake.... Ahsanteni so far kwa ushauri wenu
 
Lo! Mambo ya Udom hayo. Hiyo cafeteria si ndo ile ya jirani na madarasa ya social? Tena wanatoka wote class wanapitia hapo wanagonga menu then wanapanda gari wanaenda town kula menu yenye vinyweleo. Ulimkuta kachalazwa za kila aina we unataka umiliki mwenyewe???
Pole kaka, ndo ukubwa.
 
Kafany hiv test alafu soma shule wewe ukifikiria sana hutamaliza masomo yako
 
Angekuma mke wako ningekushauri uchukiwe hatua stahiki,ila kwa sa nakushauri mawili.(1).Kama huogopi ukimwi na upo tayari kufa tafuta mwingine then gonga kavu .(2).kama unaogopa ukimwi;Achana nae kabisa usimuongeleshe,usitafute mwengine,jichanganye na washkaji,piga sana zoezi,jiandae na UE upige GPA kali;then anza michongo ya ajira;wapo wengi sana hao tena wazuri na wenye tabia za ukweli
 
Back
Top Bottom