Ushauri mchumba wangu anatembea na lecturer wake

Ushauri mchumba wangu anatembea na lecturer wake

mdogo wangu, siku hizi nimeamua kabla sijatoka sugu kushauri watu niwe na-google kwanza vizi story, nakushauri na wewe uwe unafanya hivyo
Ushauri mchumba wangu anatembea na lecturer wake | Udaku Specially

cc. Ablessed, Nivea, Smile, BAK, Dark City. watu8, Jiwe Linaloishi, cacico, Mamndenyi, King'asti, mwaJ, Kaunga, gfsonwin, Nyani Ngabu, Preta, sweetlady, dada white, Kongosho, ...........

you are a genius and a half.
Halafu ujue nini, hii post mimi niliignore kwa sababu sikuona cha kuchangia; the guy (whoever he is) have all the facts, and he just have only two choices ambazo anapaswa kuchagua, anakuja kuomba ushauri; kweli huyu ndiye leader tunayemtegemea kwenye society kama anashindwa kufanya maamuzi ambayo facts zote ziko kwenye ground.

Simwambii jinsi ya kuishi maisha yake, kwani sio kilanja wa maisha yake!
 
POLE SANA KAKA

USHAURI

1.MUOMBE MUNGU AKUPE MKE NA SIYO DEMU.

2.MUNGU HAWEZI KUKUPA MCHUMABA HALAFU MR.X.. AJE KILAINI NA KUMCHUKUWA kwa MAANA HIYO HUYO HAJAKUPA
MUNGU.

3.CHUONI NI MAHALI PA KUSOMA SI PA KUPATIA WANAWAKE.WACHACHE SANA WANAPATA WAKE CHUONI NA
WAKADUMU NAO.

4.MUNGU AKIKUPA MKE HATA KAMA SHETANI/LECTURER AJE NA SUMAKU HAMPATI.
 
kwani katika kanuni zako za adhabu zinasemaje kwa kitendo kama hicho anachofanya mchumba wako?
akili ku mkichwa
 
Ha ha ha azoteee muulize mumeo kama amenidump,hana ubavu huo ndo kwanza kanipitia mida hii job tukatumbue,nimemwonyesha post yako kacheeekaaaa
yule mme wa mtu mekudamp?
 
Eti agonge GPA kali,hana uwezo kutwa anawaza mademu ilhal ukoo mzima unasubiria agraduate aanze kuzurura na bahasha ya khaki mtaani ha ha ha
Angekuma mke wako ningekushauri uchukiwe hatua stahiki,ila kwa sa nakushauri mawili.(1).Kama huogopi ukimwi na upo tayari kufa tafuta mwingine then gonga kavu .(2).kama unaogopa ukimwi;Achana nae kabisa usimuongeleshe,usitafute mwengine,jichanganye na washkaji,piga sana zoezi,jiandae na UE upige GPA kali;then anza michongo ya ajira;wapo wengi sana hao tena wazuri na wenye tabia za ukweli
 
now days si mnasemaga jino kwa jino?? na ww mtafute professor wako umgegede...
 
kaka wala usiwaze mwanaume hana nafasi ya kumkumbuka mwanamke aliyekuacha ila mwanamke anayonafasi ya kumkumbuka mwanaume aliyemwacha tulia piga shule wapo wanawake wastaarabu sana utapata mwingine wala usimuwaze kabisa huyo dada atakukumbuka.
 
Ha ha ha azoteee muulize mumeo kama amenidump,hana ubavu huo ndo kwanza kanipitia mida hii job tukatumbue,nimemwonyesha post yako kacheeekaaaa
ndoto za mchana hizo,mme wangu yuko zake seminar huko kwenye state moja ndani ya USA,hata kama angekuwepo hana tabia ya kuchapa nje,mme wangu ana hofu ya MUNGU
 
Ha ha chill am just joking siwezi toka na men mchovu ka mumeo mpenzi wangu ukimwona lazima ujitongozeshe,usiku mwema shosti kesho kibaruani alfajiri tutaonana mida ka hii
ndoto za mchana hizo,mme wangu yuko zake seminar huko kwenye state moja ndani ya USA,hata kama angekuwepo hana tabia ya kuchapa nje,mme wangu ana hofu ya MUNGU
 
Ha ha chill am just joking siwezi toka na men mchovu ka mumeo mpenzi wangu ukimwona lazima ujitongozeshe,usiku mwema shosti kesho kibaruani alfajiri tutaonana mida ka hii
sitakinataka,usiku mwema pia nawe.kazi njema best
 
Wivu mwingine bwana, kumkuta mtu anakula na mwingine imekuwa bonge la issue??
alaf chunga sana matetesi, japo mara nyingi zinakuwa za kweli!
NB. ukimpata mwingine jitahidi kujituma...vinginevyo wataendelea kukudonolea!:ballchain:
 
Sasa wewe hapo unataka ushauri gani, ulimuuliza akakataa, kakudanganya umemuona ukapiga simu kaingalia hakupokea na bila shaka kuna mengine mengi tuuu. imekuuma na umezima simu inamaana hutaki mawasiliano nae tena.

Endelea hivyo hivyo kukata mawasiliano nae, angalia mambo yako, soma kwa bidii na bila shaka wewe ni first born kwa hiyou unamajukumu mengi, utapata akupendae.

Achana nae
 
Mambo mengine bwana yanafurahisha,kuwa ww umegekwa? sasa unasubiri nini bro achana naye hayo yamekukuta wengi leo yalishakutawengi,wakaachana nayo leo hao ni wakurugenzi wanawakimbia wanawake kwani ni wengi ,achana, naye huyo soma haowako wengi utajawakimbia dogo take care

Searching...100%
Loading...100%
Network Connected !

Near by Philip & Friends Academy Mbeya.
 
Kwa hiyo story za udaku special zinahamishiwa jf siku hizi??

Nadhani mods inabidi wajaribu kuangalia hili, story ikitokea udaku special wawe wanazifunga au zinapelekwa jukwaa la jokes

Watu tunatoka povu vichwani kushauri kumbe jamaa natuenjoi tu

Mtoa mada - Mafi yako

Hahahahaaaaa...... Nimejikuta natoa bonge moja la kicheko..! Yaani weweeee...!
 
Hakuna raha ninayosikia kama kumpora demu mwanafunzi wa chuo kisha kumuangalia anavyotapa tapa.
Uwa nawa-enjoy sana awa watoto wa shule na nafanya ivyo ili waache tabia zao za mapenzi shuleni kama me nilivyoacha na sasa naona matunda yake.

Acheni ngono vyuoni

Kote ulikwenda vema,
hapo ulipokuja na hizo habari za kupora mademu ndo umeharibu mantiki na uwezo wako kifikira!
Kweli elimu uuliyopata haijakukomboa,
Unadhani unawakomesha kupora mademu, jamani kweli binadamu tupo tofauti, huyo demu akitoka kwako anaosha tu tu hiyo pachuchu anahamia kwa mwingine zaidi, mwingine Mademu wa vyuo wana wanaume kulingana na mahitaji yao, yupo mwanaume anayepewa dudu kwa ajili ya academic affairs, wenyewe wanaitaga academic husband, yupo wa club, yupo wa shopping, yupo wa nyumbani so jiche kaka inawezekana wewe ni wa shopping lkn hujajigundua
Funguka kaka, Elimu uliyopata iwe imekukomboa
 
umfanye nini ?
unataka apigwe disco...kaamua kupata degree ya ngono muache
Baada ya hapo, ataona kumbe maisha yanaenda simpo hivi....hatimae anakuja pata kibarua kwa njia ile ile ya mkato!
 
Habari za jioni wana JF!!
Mimi ni kijana wa kitanzania, najitokeza hapa mbele yenu kuomba ushauri
kwa haya makubwa yaliyonikuta.

Nilianza chuo miaka mitatu iliyopita, nikimaanisha kwa sasa nipo mwaka
wangu wa mwisho katika hii kozi ninayoichukua. Nilianza chuo bila kuwa
na uhusiano wowote ule wa kimapenzi na msichana hapa chuoni kwa mwaka
wote ule wa kwanza.

Hali hiyo ilibadilika baada ya kuingia mwaka wa pili, kwani kipindi
hicho kukawa na mwaka wa kwanza wanaingia na bahati nzuri nikatokea
kumpenda msichana mmoja mrembo wastani sema ni mstaarabu haswaa.
Nilijaribu bahati yangu na mungu si athumani huyu msichana akanikubalia
na tukaanza mahusiano yeye akiwa mwaka wa kwanza,mimi wa pili. Tuliishi
kwa amani na  furaha kwa kipindi chote kile(nikimaanisha
semester zote mbili za mwaka wangu wa pili).

Kinachonifanya kuandika hapa ni hiki sasa, mwanzoni mwa semester
iliyopita nilianza kusikia tetesi kutoka kwa marafiki zangu ya kuwa huyu
msichana niliye naye anatoka na mmoja wa ma-lecturer wanaomfundisha.
Sikuliamini hilo, nikaamua kumuliza mwenzangu kwamba nimesikia hili na
hili, je kuna ukweli wowote? Alikataa kata kata na kusema huo sio ukweli
na nisiamini kila ninalolisikia, kwa kuwa ni mstaarabu sana na kwa
jinsi alivyokuwa akiongea basi nikamuelewa kwa muda ule.

Ila sikuishia hapo nikaendelea na uchunguzi wa chini chini bahati mbaya
sikuambulia lolote kuhusu uhusiano wake na  huyo lecturer zaidi
ya yeye kuwa na ratiba ya  kwenda kwao kila baada ya wiki
mbili kuanzia ijumaa jioni mpaka jumapili ambao ni utaratibu wake toka
anaanza chuo. Na hiyo ijumaa mpaka jumapili akiwa nyumbani mawasiliano
yalikuwa yakipungua sana kwa sababu alikuwa akisema anakuwa busy sana na
shughuli za nyumbani kwao na hata usiku ukimpigia simu alikuwa hapokei
kwa madai analala na ndugu yake na kwahiyo atakuwa anampigia kelele.

Leo mchana sasa, nilimpigia simu twende tukapate chakula cha mchana
lakini alikataa na kuniambia kuna kazi anaifanya kwanza mpaka aimalize
ndio ataenda kula, mimi nikatangulia kwenda kula ila wakati narudi
nikakutana na rafiki yangu, akaniuliza mbona nimekutana na bibie(mchumba
wangu) anakula na Mr. X (huyo lecturer niliyeambiwa anatembea naye )
sehemu flani(ma-lecturer wengi ndio wanapokula hapo na kama utakuta
wanafunzi basi ni mmoja mmoja ambao wako vizuri sana kifedha)…
sikuamini, nikaenda kuhakikisha… Nilichokiona aisee sikuamini macho
yangu, wote wawili walikuwa wamekaa wakipata lunch tena wakionekana
wenye furaha.

Nilimpigia simu lakini hakupokea, aliishia kuiangalia tu simu yake na
kuirudisha kwenye meza… Nikamtumia meseji ya kwamba nimemuona na
nimezima simu yangu mpaka sasa, hapa natafakari nimfanyaje huyu msichana
kwa hili alilonifanyia??? It hurts kwa kweli ikizingatiwa huyu lecturer
ana mke kabisa so what if ndio tabia yake hiyo kutemebea na wanafunzi?
Si  ndio kuambukizana magonjwa huku??

Naombeni ushauri wenu wana  JF, nimfanyeje huyu
kiumbe??

Mtafute huyo Lecturer, mwambie tabia yake siyo nzuri.
 
Uyo lecturer achana nae ,acje fanya mambo na lecturers wenzake ufaulu wako ukawa at stake..
Uyo binti we ushaona live anachukuliwa,muulze akueleze ukwel,dnt lose ur concetration ya shule for a woman who betrays u,chuo mbna girls wengi tu,opoa kifaa kingne wen u get over her
 
Back
Top Bottom