Ushauri: Maafisa uajiri wa taasisi binafsi waajiriwe au wasimamiwe na Serikali

Jul 21, 2013
13
12
Baada ya kuwaza kwa muda mrefu ningependa kushauri baadhi ya taasisi binafsi hasa zenye wafanyakazi zaidi ya 200+ zisimamiwe na Serikali direct kwa kuajiri HRs au HR waripoti Serikalini na sio kwa waajiri binafsi kama ilivo sasa.

Sababu za kufanya ivyo na faida zake:
1. Kumwezesha HR kusimamia moja kwa moja sheria, kanuni na miongozo ya serikali.
Kwa sasa ni rahisi kushindwa kusimamia moja kwa kwa moja kwa hofu ya kupoteza kibarua chake Boss akikasirika.

2. Kampuni nyingi zenye wafanyakazi 200+ zina wageni (Expatriates ) ,inawezekana kutokana na wasi wasi wa kupoteza ajira hawa HRs hawezi kutoa taarifa au kusimamia pale mambo yanavyoenda tofauti na vibali vyao vya Ukaazi na Kazi pia.

3. Mapato, Kodi, Michango na Ada mbali mbali za lazima kwa serikali - kutokana na taarifa mbali mbali kutoka vyombo vya habari na mashirika , zipo baadhi ya Taasisi zimekua zikichelewesha malipo au kutolipa kabisa michango ya wafanyakazi kama NSSF, WCF na ada nyinginezo kwa njia wanazojua wao. Kama hawa HRs wangekua wanaripot moja kwa moja Serikalini nadhani hii pia ingesadia.

4. Usawa katika soko la ajira,
Yapo baadhii ya makampuni na taasisi binafsi hazina muundo maalumu wa mishaara na kuajiri bila kufata Sifa stahiki.

5.
6.

Ni mawazo tu wajumbe mnaweza kuongeza na nyie pia viwafikie watunga sheria

CC. J.Mhagama,
 
Mkuu utakuwa na hoja kama Kingai, Jumanne, Mahita, Sirro, Goodluck, Sabaya, kondakta na wenzao hawaripoti serikalini.

Ila kama hao wana ripoti serikalini, mbona bora kazi (status quo) na iendelee?
 
Mkuu utakuwa na hoja kama Kingai, Jumanne, Mahita, Sirro, Goodluck, Sabaya, kondakta na wenzao hawaripoti serikalini.

Ila kama hao wana ripoti serikalini, mbona bora kazi (status quo) na iendelee?
Angalia wanapoenda kinyume na utaratibu nini kinatokea mkuu ,
 
Back
Top Bottom