Kuna watu watafariki kwa mgongano huu wa NHIF na hospitali binafsi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,014
9,883
Kwa wateja wengi wa Bima hospitali binafsi ni kimbilio kwa ubora wa huduma zao ukifananisha na hospitali za serikali. Nakumbuka ndugu yangu mmoja alilazwa Temeke kwa dharura, hospitali ilikuwa inaomba kutumia vifaa vyetu kuwapima wagonjwa wengine wa pale. (Kwa ugonjwa uliotulaza kipimo chake kiko shared, hakihusishi damu)

Watu wenye ugonjwa ule wengi wakawa wanafariki pale, na wahudumu wala hawana muda ni kama wanasubiri watu wafariki. Tulienda pale kwa dharura tu kwa kuwa hospitali tuliyozoea ilikuwa mbali kwa usiku ule na baada ya kuwa admitted pale ilikuwa ngumu kuruhusiwa kwenda kwingine. Hata hivyo tukafanya mafekeche tukaenda Agha Khan.

Agha Khan wanapokea bima ambazo ni supplimentary (kifurushi kikubwa). Pale tulipata huduma nzuri sana ndugu akapata kwa muda mfupi akarejea nyumbani.

Sasa nawaza watu wenye maradhi ambao wamelazwa hospitali nzuri za binafsi kama Agha Khan, Saifee, Kairuki na kwingineko, kwa haya matangazo yao maana yake wateja walipe cash ambapo ni gharama sana ao waondoke kwenye hospitali.

Fikiria maradhi yanayohitaji extra care. Fikiria mtu ambaye amepata majanga sasa hivi, ila haezi kwenda hospitali binafsi wakati huu anapaswa kwenda serikalini ambapo kuna balaa kama tulivuozoea. Ni wangapi watafariki.

Busara inahitajika.
 
Tatzo la Serikali Ni ubabe hata pasipo stahili
Sababu kubwa na ya msingi, kwenye sector ya umma wanaajiriwa university na college wasio cream, ndio maana wanalipwa less na wapo ready, cream yote ya vyuo ipo sector binafsi kwa kuzingatia mishahara na delivery, huwezi tegemea ubunifu public zaidi ya wizi na kuforce increments na posho bila uzalishaji.

Unaona wakistaafu wanakufa mapema hata maprofesa wa ujasiliamali hawana biashara bunifu zaidi ya kufuga nguruwe na guest houses. Matokeo ya haraka ndio hayo walikoajiriwa.

Hawazuii tatizo kama sukari, mfumuko wa bei na umeme, vikitokea wanajifanya kuhangaika kutatua.

Je ni kwa nini hawana mifumo imara ya kuzuia na kubaini wizi wa pesa kwenye mifumo hadi waziri mkuu anakuja kubaini miezi kumi baadae?. Je asingekuwepo?,Mbona mabenki yenye watumishi cream (from recruitment) wizi wa kipuuzi ni mdogo?
 
Back
Top Bottom