Ushauri: Long Distance marriage

Ushauri: Long Distance marriage

Habari wakuu,

Mimi ni mdada natamani kuingia katika ndoa hivi karibuni,nina mtu wangu lakini hatujatambulishana bado kwasababu bado natafakari niamue kipi. Kinachonisumbua ni kuwa tunakaa mikoa tofauti yeye anafanya kazi huko Mwanza na mimi nipo Dodoma.

Kwa namna kazi yake ilivyo hawezi kuhama na kuja nilipo mimi na mimi pia ni hivyo hivyo. Sasa nikitafakari hali hii nashindwa kufanya maamuzi, kiukweli napenda sana na I always pray nipate ndoa ambayo tutakaa pamoja sehemu moja sio hizo za mbalimbali, pia nikifikiria na changamoto ya uaminifu katika hizi ndoa za siku hizi napata hofu na vile wanaume wenyewe ndio shetani huwa anawapitia sana! Akili yangu inakosa utulivu kabisa.

Nikikubali kuolewa na huyu mwanume maana yake tutaishi mbalimbali sijui kwa muda gani, kuanzia ndoa ikiwa changa hadi muda usiojulikana.

Naomba ushauri ndugu zangu ndani ya nafsi yangu nikifikiria kukaa mbalimbali nakosa amani kabisa!
Olewa tu Kama man pendana Mungu atawasaidia.
 
Mara nyingi mwanamke ndo anatakiwa kuhama! Kwa mda huu jaribu kitafuta kazi alipo akati bado upon hapohapo kazini kwako. Muombe ata akusaidie kutafuta. Ukipata endeleeni na process ya ndoa. Long distance marriage hua hazi work kwakweli. Lazima mmoja wenu a sacrifise kuhama.
 
dada suala la ndoa ni la milele, ila suala la kazi waweza pata pengine...cha kufanya
1: kama kampuni/taasisi unayofanya kazi ina tawi mwanza ongea na boss wako uombe uhamisho wa kikazi kwenda mwanza/mikoa ya kanda ya ziwa, na state clearly kwamba nakaribia kufunga ndoa na mwenza ngu yupo mwanza.
2: kama haiwezekani kupata uhamisho huo aidha kwa kuwa kampuni/taasisi hiyo haina ofisi mwanza /mikoa ya kanda ya ziwa basi acha kazi nenda mwanza kakae na mwenzako, kwakuwa ye anayokazi ataweza kukutafutia kazi au mkafungua kitu ukawa unasimamia.
hapo ni suala la kuthaminisha tu maana utaokoa kazi ila utampoteza ambapo kupata uonaye anafaa kama huyo ni ghali sana na itakugharimu pengine usipate atakayejaa nafsini mwako kama huyo.
ni kweli kuwa mbali hivyo ni rahisi kutekwa maana hali ya sasa waname ikijulikana una kazi afu wadada hawakuoni na mtu watakutafuta kwa nguvu zote hadi utadondoka kwa mmoja wapo.
mwambie mwenzako msimamo huo na anza utekelezaji mara moja ysipoteze tena mda kukaa unawaza
 
Situesheni ngumu sn,hapa sasa ni kuangalia nini cha thamani zaidi kwako...
Fanyeni juhudi wote wawili upate walau kazi hata ya kujishkiza huko aliko
Naamini family mnapaswa kuishi wote mambo ya distance basi ziwe zile za safari labda lakini throughout the year mhhhh...
 
Habari wakuu,

Mimi ni mdada natamani kuingia katika ndoa hivi karibuni,nina mtu wangu lakini hatujatambulishana bado kwasababu bado natafakari niamue kipi. Kinachonisumbua ni kuwa tunakaa mikoa tofauti yeye anafanya kazi huko Mwanza na mimi nipo Dodoma.

Kwa namna kazi yake ilivyo hawezi kuhama na kuja nilipo mimi na mimi pia ni hivyo hivyo. Sasa nikitafakari hali hii nashindwa kufanya maamuzi, kiukweli napenda sana na I always pray nipate ndoa ambayo tutakaa pamoja sehemu moja sio hizo za mbalimbali, pia nikifikiria na changamoto ya uaminifu katika hizi ndoa za siku hizi napata hofu na vile wanaume wenyewe ndio shetani huwa anawapitia sana! Akili yangu inakosa utulivu kabisa.

Nikikubali kuolewa na huyu mwanume maana yake tutaishi mbalimbali sijui kwa muda gani, kuanzia ndoa ikiwa changa hadi muda usiojulikana.

Naomba ushauri ndugu zangu ndani ya nafsi yangu nikifikiria kukaa mbalimbali nakosa amani kabisa!

usidhubutu kabisa long distance marriage....shetani atakupitia ata wewew pia sio mume tuu. au wewe hupendi mgegedo? hahaha
lah msingi dada hamia mwanza au waogopa wazazi watasema tumekusomesha kwa nini uaacha kazi na kumfuata mwanaume
 
OLEWA ENDELEA NA KAZI,HUKU UKITAFUTA KAZI ALIPO MMEO.Distance marriage mnaishi,mkishindwa si mnapena talaka tu;olewa tu ila kama mnapendana kwa dhati ,distance is nothing at all

wee wacha kumuingiza akili za ujinga mwenzio...sasa unataka awaze talaka ata kabala ya kuingia kwenye ndoa....sii sawa na kumwambia wee endeleea kugegedana tuu na jamaa ndoa ya nini
 
its a norm kwetu waafrika kwamba baada ya ndoa ni lazima mke na mume wakae nyumba moja...moving italeta matatizo mapema sanaaaa,kwanza utaanza is his job better than mine na kama utakuwa hujapata kazi huko mwanza ndio shida kabisaaa, cause unahela yako ndio, what happens pale umetumia wee,hela inaanza kuisha, kazi hujapata so you now have to ask for money kila mara...sacrifices hufanyika sana, mi nakushauri kuanza kutafuta kazi au mradi wa kufanya mapemaaa huko Mwanza kabla hujaamua kuolewa. Tena pale uanze kufanyiwa visa vya maneno baada ya kuomba hela heheeheee...alafu watu wanasemaga money sio ishu, love is what matters...nyooooooo

kudadadeki mwanamke umeongea point....uluguruni huku tunasema " hilo nalo neno"
 
hizi long distance marriage ni shida asee!, mimi mkewng kaenda kusoma mwanza, now ndo yuko mwaka wa pili na maisha ya chuo ninavoyafahamu kuchapiwa dakika tu! na nikimcheki wife bado mteke, nikaamu kumbandika mimba aendenayo huko chuo moyowangu angalau umetulia sasa.

ila dada nakushauri usije acha kazi na kama mnapendana owaneni tu.
Aliye kwambia wenye mimba awagongwi nani? nawanavyokuwaga na hamu.....na kale kajoto kao duuh nowmaaa.
 
Mwanzoni story ilitaka kunigusa nkadhani mama watoto katupia nyuzi uku hehe
 
Kwa mwanamke kitu muhim ndoa kuliko kazi, we uwaoni kina profesa ndalichako, sijui mama tibaijuka, sijui Anne makinda au rose migiro , SAA nyingine wanaona madegree na mavyeo yao si kitu kama hawana Mme full stop, shauri yako utazeekea nyumban
 
OLEWA ENDELEA NA KAZI,HUKU UKITAFUTA KAZI ALIPO MMEO.Distance marriage mnaishi,mkishindwa si mnapena talaka tu;olewa tu ila kama mnapendana kwa dhati ,distance is nothing at all
Wewe kadada au kwa kuwa si wewe, ndoa ya mbali matatizo
 
Distance relationship ni hatari sana asikudanganye mtu sio kwa mwanamke wala mwanaume, mie mwenyewe nilikuwa na msichana niliyempenda sana naye alionyesha kunipenda kwa dhati, nikamaliza masomo nikapata kazi dar yeye akiwa Mwanza and all the time nikiwa dar tulikuwa tunawasiliana na akipata shida nilikuwa najitahidi nimtimizie, lakini ndan ya mwaka akabeba ujauzito wa mwanaume mwingine na akawa ananificha mpaka nilipomkuta nilipoamua kwenda Mwanza na kumkuta akiwa mjamzito, kiliniumiza sana na sijui kama nitaoa tena kwasababu kila nikijaribu kuwa na uhusiano feelings zinatoweka unkwongly. Yaani nakushauri kama utakubali distance marriage itabidi mpange ratiba after two weeks muwe mnaonana. Zamani nilikuwa naamini sana kuwa distance in love make love stronger than before ila vice versa is true
 
Back
Top Bottom