overblessing
Member
- Apr 2, 2016
- 18
- 40
Habari wakuu,
Mimi ni mdada natamani kuingia katika ndoa hivi karibuni,nina mtu wangu lakini hatujatambulishana bado kwasababu bado natafakari niamue kipi. Kinachonisumbua ni kuwa tunakaa mikoa tofauti yeye anafanya kazi huko Mwanza na mimi nipo Dodoma.
Kwa namna kazi yake ilivyo hawezi kuhama na kuja nilipo mimi na mimi pia ni hivyo hivyo. Sasa nikitafakari hali hii nashindwa kufanya maamuzi, kiukweli napenda sana na I always pray nipate ndoa ambayo tutakaa pamoja sehemu moja sio hizo za mbalimbali, pia nikifikiria na changamoto ya uaminifu katika hizi ndoa za siku hizi napata hofu na vile wanaume wenyewe ndio shetani huwa anawapitia sana! Akili yangu inakosa utulivu kabisa.
Nikikubali kuolewa na huyu mwanume maana yake tutaishi mbalimbali sijui kwa muda gani, kuanzia ndoa ikiwa changa hadi muda usiojulikana.
Naomba ushauri ndugu zangu ndani ya nafsi yangu nikifikiria kukaa mbalimbali nakosa amani kabisa!