Habari yako kk!
Kwanza nikupongeze kwa kuchaguliwa kwenda kusoma Iran.
BINAFSI mm ni mwanafunzi nasoma Biomedical engineering huku Russia.Mara ya kwanza nilipopata chua watu wakaanza kunishauri vitu vingi ambavyo vilikuwa negative kama mambo ya ubaguzi,usalama na baridi.nikisikiliza ushauri wao na baada ya muda nikaamua kwenda kusoma russia mji mmoja unaitwa Tambov.nikisoma lugha huko tambov na baada ya mwaka nikamaliza.nikiwa tambov sikuwai kupata tatizo lolote la ubaguzi,usalama au hata michongo ya baridi.nilipo maliza lugha Tambov nikaamua kuama mji kwenda kusoma mji mwingine unaitwa Vladivostok.mjii huu wa Vladivostok ni mji ulipo mbali sana KUTOKA mji mkuu wa urusi moscow na mji ambao nilikuwa nasoma mwanzo.watu wakaanza kunishauri mambo kibao kuhusu kuama kwangu kwani mji huu wa Vladivostok haukua na mwafrika hata mmoja na mi ndo nikikuwa wakwaza kwanza.lakini nikaamua kwenda na nilipofika huko nikakutana na mambo ambayo sikutegemea maana nilikuta watu wa huko ni wakarim sana na maisha ya huko yalikuwa mazuri kuliko sehemu yoyote ile niliopata kushi ndani ya urusi japo mwafrika nilikuwa peke yangu.
Hoja yangu ni kuwa ni vizuri kuomba ushauri but unapofanya maamuzi jalibu kuangalia ni kipi moyo wako unataka mana wao wanaokupa ushauri wanasema ivyo labda kwa kusikia sikia tu au kwa jinsi walivyo jionea japo kila mtu anastail tofauti za kuishi so haimaanishi jinsi alivyoishi au yaliyomtokea fulani na ww yatakutokea.
Ushauri wangu nenda kasome mana KUTOKA tu nje ni faida sana hasa kama unajitambua mana licha ya masomo utajifunza mengi sana