biarakeyz
Senior Member
- Jan 19, 2016
- 183
- 47
- Thread starter
- #101
kaka chige chuo chenyewe ni Tehran university of medical sciences(TUMS)
Anyway, kv sikifahamu chuo chako labda niseme kitu kimoja. Mwaka jana nilifanya utafiti kuhusu credibility and acceptability ya institutions zinazofanya university ranking duniani... moja ya hizo institutions ipo hiyo webometric; nayo inakuwa referenced mara kwa mara. Ingekuwa ni ranking ya 4iuc ningekuambia achana nayo coz' ingawaje wao wenyewe wanasema wazi kwamba ranking yao sio by academic performance, lakini Wabongo ndio ranking tunayopenda kuitumia kv ndio the only ranking inayoweka vyuo vyetu juu!!!! Nilikuja kushituka siku ambayo hata Profesa Mkandara alii-reference ranking yao 4icu... nikajua, siasa at work!
Hata hivyo, ranking zinazoheshimika sana duniani na kuwa hata referenced na watu wenye dunia yao ni Times Higher Education and Shanghai Ranking! Itoshe tu kusema kwamba, kwa kutumia Times Higher Education hakuna chuo chochote cha Tanzania kinachotokea hata among 1000 best universities duniani... HAKUNA! Lakini wakati Tanzania hatuna ubavu wa kuingiza japo chuo kikuu kimoja kwenye list, ranking ambayo ilitoka mwaka jana Iran iliingiza vyuo vikuu 8 among Top 800 Universities duniani! Na kv chuo chako kimetokeza kwenye webometric, basi nacho kitakuwa ni moja ya hivyo vyuo. Hivyo basi, hiyo peke yake unaweza kupata picha ya kiwango cha elimu kati ya Tanzania na Iran... they are very far compared na sisi!!! Unaweza ku-opt kuachana nao kwa sababu zingine lakini sio ubora wa elimu!