Ushauri kwa Wanyarwanda: Sioni kosa la Kikwete!

Ushauri kwa Wanyarwanda: Sioni kosa la Kikwete!

Mbona hujasema kwanini Marekani hawakai na Al Qaeda meza moja,Never negotiate with terrorists.


Kumbe Alqaeda walikuwa ni miongoni mwa jamii ya wamarekani?Sikuwa nalijua hili? Kwahiyo waliwaua wamarekani wazungu na weusi halafu baadae wamarekani wazungu na weusi wakaichukua nchi na wamarekani waarabu (Alqaeda) wakabaki kuwa waasi?

Acha kutoa mifano ya kiabunuasi pompompoo wewe, wahutu ni miongoni wa wanyarwanda na wanachokipigania ni madaraka/usawa ndani ya nchi yao. Sasa hayo Alqaeda na Marekani yanatokea wapi? Hivi unajua wahutu wanavyonyanyasika ndani ya nchi yao kwasasa chini ya utawala wa kitutsi wa Kagame? Bora ufunge tu bakuli lako kuliko kupenda kushabikia usiyoyajua.
 
Waliwaua tena wengi na mbaya zaidi wakawafuata tena kwenye makambi yao waliyokimbilia DRC mwaka 1997 kipindi kile wanasaidia kumuondoa Mobutu inasemekana watusi waliua wahutu milioni mbili mashariki mwa DRC.Kwa hiyokwa kifupi kama watusi waliokufa kipindi cha genocide mwaka 1994 walikuwa laki 8 then watusi wakarevange kwa kuua wahutu milioni 2 kwenye makambi yao DRC so who is a genocider? haya soma mwenyewe hii link hapa chini
Second Rwanda genocide is revealed in Congo - World news - Africa | NBC News

Nashukuru sana mkuu, na mimi nimeuliza swali kama la kwako - hakuna anaye toa jibu la kuridhisha! As far as they are concern GENOCIDERS ni kabila moja tu, kabila jingine alihusiki!! Binafsi si support mauuaji yote - iwe nchini Rwanda au kwenye makambi ya wakimbizi nchini Congo - mauuaji by any name ni mauuaji TU.
 
Hata wale wakimbizi waliohifadhiwa ngara na kigoma ambao aliwazuga kuwa warudi rwanda kuwa vita vimekwisha na hakuna visasi, aliwapiga risasi wote. Jamaa ni chinjachinja ambaye anajifanya mtu mwema.

We acha tu ndugu yangu, inasikitisha sana lkn dunia yote imekaa kimya na kila siku wanaokumbukwa ni watusi tu kana kwamba wahutu waliokufa walikuwa kuku
 
Kumbe Alqaeda walikuwa ni miongoni mwa jamii ya wamarekani?Sikuwa nalijua hili? Kwahiyo waliwaua wamarekani wazungu na weusi halafu baadae wamarekani wazungu na weusi wakaichukua nchi na wamarekani waarabu (Alqaeda) wakabaki kuwa waasi?

Acha kutoa mifano ya kiabunuasi pompompoo wewe, wahutu ni miongoni wa wanyarwanda na wanachokipigania ni madaraka/usawa ndani ya nchi yao. Sasa hayo Alqaeda na Marekani yanatokea wapi? Hivi unajua wahutu wanavyonyanyasika ndani ya nchi yao kwasasa chini ya utawala wa kitutsi wa Kagame? Bora ufunge tu bakuli lako kuliko kupenda kushabikia usiyoyajua.

Hivi anajua kuwa Karzai anazungumza na TALIBAN kila siku na kikwazo ni marekani tu!
 
Mbona hujasema kwanini Marekani hawakai na Al Qaeda meza moja,Never negotiate with terrorists.

Hawezi kusema hivyo! USA inatoa misaada mingi tu hapa TZ! Endapo atayasema haya mbele ya Wamarekani, basi atakuwa amejifutia mwenyewe misaada anayoomba na atakuwa amewapa Njia FBI na CIA kuichunguza vizuri TZ na pengine kugundua mambo mengi juu yake na utawala wake! Kwa hiyo sio rahisi kwa JK kuishauri hivyo US!
 
Hivi anajua kuwa Karzai anazungumza na TALIBAN kila siku na kikwazo ni marekani tu!


Sijakupata vizuri mkuu wangu, Are we still talking about Hutu and Tutsi in Rwanda au unanifahamisha tu kuhusu ubabe wa wamarekani? Nifafanulie kidogo mkuu.
 
Waliwaua tena wengi na mbaya zaidi wakawafuata tena kwenye makambi yao waliyokimbilia DRC mwaka 1997 kipindi kile wanasaidia kumuondoa Mobutu inasemekana watusi waliua wahutu milioni mbili mashariki mwa DRC.Kwa hiyokwa kifupi kama watusi waliokufa kipindi cha genocide mwaka 1994 walikuwa laki 8 then watusi wakarevange kwa kuua wahutu milioni 2 kwenye makambi yao DRC so who is a genocider? haya soma mwenyewe hii link hapa chini
Second Rwanda genocide is revealed in Congo - World news - Africa | NBC News

Na hilo ni mojawapo wa jambo linalomgombanisha Kagame na Utawala wa France........
 
Hawezi kusema hivyo! USA inatoa misaada mingi tu hapa TZ! Endapo atayasema haya mbele ya Wamarekani, basi atakuwa amejifutia mwenyewe misaada anayoomba na atakuwa amewapa Njia FBI na CIA kuichunguza vizuri TZ na pengine kugundua mambo mengi juu yake na utawala wake! Kwa hiyo sio rahisi kwa JK kuishauri hivyo US!

Hauwezi kamwe kulinganisha Al qaida na waasi wa kihutu au waasi wa m23!. Al qaida ni raia wa nchi gani specificaly?. Lakini wahutu ni raia wa Rwanda na m23 ni raia wa congo wenye asili ya Rwanda. Kikwete asingeongelea kuhusu al qaida sababu analijua hilo.Cha muhimu watutsi muache ujeuri wa kujiona nyie ni bora zaidi ya wahutu mkae muongee mmalize matatizo yenu. Mbona hao wahutu nao waliwahi kuuawa kwa wingi lakini siku zote hamuongelei hilo?.Ni ushauri mzuri wa Kikwete,Rwanda iongee na waasi wa ki hutu,congo iongee na waasi wa m23na uganda iongee na waasi wao?Tunachotaka ni amani na usawa katika ukanda huu na si kundi moja kujiona bora na kutawala kundi lingine milele. Hata mkuu wa majeshi mstaafu wa Rwanda ndugu Kayumba Nyamwasa amempongeza Kikwete kwa kauli yake!
 
Museven and Kagame: These two Tutsi-Hima junta military leaders ndiyo kikwazo kikubwa cha amani katika eneo hili la maziwa makuu. Were key figures in plotting and perpetrating 1994 Rwandan genocide wakishirikiana na raisi wa taifa moja kubwa duniani. Lengo lao kuu likiwa ni kufaidi rasilimali zilizopo mashariki mwa DRC. Mkuu wa kwanza wa mahakama ya Kimataifa ya kimbari ya Rwanda (ICTR) katika uchunguzi aliofanya kuhusu chanzo cha Rwandan genocide aligundua kwamba aliyekuwa Rais wa taifa moja kubwa duniani wakati huo walishirikiana na M7 na Kagame kuitungua ndege iliyobeba maraisi wawili wa Rwanda na Burundi na kuwaua huku waki-underestimate idadi ya watu ipatayo 50,0000 (elfu hamsini tu) watakao kufa kutokana na ulipizaji kisasi. Huku wakisema idadi hiyo ni reasonable na jambo la kawaida la number ya watu kutolewa kafara linapokuja suala la kutimiza lengo kuu na muhimu. Ili kudhibiti (kuzuia) uchunguzi huo kuendelea na matokeo yake kuwekwa hadharani, raisi wa taifa kubwa alimshinikiza Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa Koffi Annan kumuondoa raisi wa ICTR kwenye wadhifa wake na vile vile kupiga stop uchunguzi huo. Kuanzisha mauaji ya Rwanda ilikuwa ni siri ya wachache ndani na nje ya RPF hivyo ili kuzuia uvujaji wa siri hiyo baada ya kuanza kwa uchunguzi wa chanzo cha mauaji hayo na mkuu wa ICTR na baadaye kuachishwa kazi na Koffi Annan, raisi wa taifa kubwa alimlazimsha Kagame kuhakikisha kuua kila mtu ndani ya RPF anayejua siri hiyo. Ndiyo sababu ya mauaji ya waliokuwa washirika wa karibu wa Kagame waliokimbilia nje ya nchi (mfano Seth Sendashonga) na wengine kunusurika (mfano Jenerali Kayumba Nyamwasa). Pia kilichomponza mkuu wa kwanza wa ICTR kuondolewa ilikuwa ni nia yake ya kutaka kumfungulia mashitaka raisi Kagame na washirika wake katika kuhusika na Rwandan genocide. Sasa jiulize kwa nini wanatoka povu jingi wanapoambiwa ukweli wa-negotiate na FDLR? Ni kwa sababu truce itafikiwa kwanza kwa kuwekwa wazi chanzo cha genocide, sasa Kagame hapo anaona hawezi kuchomoka! Kagame hataki ukweli ujulikane! Kwakuwa Kagame alisababisha kutokea kwa genocide kwa hiyo wote ni wahalifu hivyo wote wakae chini wazungumze wamalize tofauti zao kwa kusameheana kisha wajenge nchi yao na ndiyo maana raisi JK kamwambia wazi Kagame negotiate please na FDLR! Kagame huo ndiyo ukweli wenyewe ulioambiwa na mkuu mwenzio, ni ushauri wa bure PLEASE NEGOTIATE WITH FDLR!
 
huyu waziri wa rwanda wa mambo ya nje aliropoka mashudu ganii????
 
raisi alikuwa sahisi katika hili na wala hajakkosea mtu yeyote mwenye reference za comment mabya amabzo wanyarwanda walizitoa kwa raisi wetu please ningependa kuziipata hata kama ni katka social netwoks za kwao
 
Tatizo la uchambuzi wako ni kukosa hisoria ya FDLR na kilichotokea kipindi na hata baada ya mauaji ya 1994. Sio mambo yote yanatatuliwa kwa kukaa chini na kuongea. Mbona hatoi ushauri huu kwa Marekani na kuwaambia wakae chini na Al qaida waongee? Rwanda iongee nini na FDLR? Hata baada ya kupatikana kwa amani Rwanda wakimbizi wakaambiwa warudi, hawa jamaa hawakurudi, kwanini hawakurudi wakati wakimbizi wengine walirudi. Kwanini kama mtu kakosea msimwambie tu kuwa kakosea? Angeongela mambo mengine bwana, alikuwa na mambo mengi ya kuongea hili kachemsha kwa wale ambeo wanajua historia ya Rwanda
....jamaa wa FDLR ni sehemu ya rwanda..ni wanyarwanda walioikimbia nchi yao na kuishi uhamishoni kwa sababu ambazo zinaeleweka zaidi kwao..!usichanganye mambo..? we si gt? beahave ki gt..!
 
Ushauri wa Kikwete ni mzuri sana kwa wanyarwanda wasikivu na wanaoona mbali mstakabali wa nchi yao. Lakini kwa kuwa viongozi wao ni watu wanaojidanganya kwamba watutsi ni watu maalum wa kuwatawala wahutu daima hawawezi hata siku moja kufikiri vinginevyo maana wamezaliwa na kukuwa wakiwa na taswira hiyo ya kipuuzi kwamba ni watawala daima. Ni vyema wakafanya mazungumzo kama walivyofanya wenzao wa Burundi. Watutsi wa Burundi walizindukana mapema wakaona ukweli kwamba hawawezi kutawala milele bila kuwashirikisha wahutu. Wanyarwanda wasipozinduka si muda mrefu watachunjana tena na labda ndio kitakuwa kipindi cha wahutu kutawala kwa chuki! Zungumzeni mpate amani la sivyo mtamalizana kwa visingizio visivyo na tija kwa watu wenu.
 
Rais ajishughulishe zaidi na Mambo ya Ndani ya Nchi yake.Mbona humu Nchini Kero bado ni nyingi sana hazijapatiwa Ufumbuzi?.Kingine ni kwamba tusilazimishe Ushauri wa Kikwete ukubaliwe na Rwanda eti kwa sababu tu umetolewa na Rais.Wao wana vigezo vyao vya kupima shauri mbalimbali.Kama hatujafikia vigezo vyao wataona Kikwete kapendekeza Pumba tupu.Na kwa kuwa sisi ndio tumewaanza wana kila sababu ya kureact.
 
Rais Kagame amekoseha sana,,,kutoa kauli kama hizo za kumfedhehesha Rais wetu,,,,KWANI UNAPOSHAURIWA LAZIMA UKUBALI??,,,,angekaaa kimya kuliko kutukana,,,,,i hate HIM 😛arty:😛arty:,,,,,,RAIS WETU YUPO SAHIHI
 
mimi nadhani kuna mengine zaidi nyuma ya pazia,nikiangalia ushirika wa JK na Zuma sioni kama kuna mkakati wowote wa maana kama sibaada ya siku chache kusikia jeshi letu ktk,scandal za biashara ya madini na silaha huko DRC! Watu wanatafuta pesa za uchaguzi! Sioni tofauti kubwa anachofanya Kagame na tutakayo sikia hivi karibuni yakifanywa na watu wetu DRC!
 
Watanzania tusichokijuwa ni nia ya Rais kagame na Rais Museven kutaka kuitawala Afrika mashariki na kati. chini ya mission yao ya kuuda HIMA EMPIRE .huu ni mpango wa WATUTSI kuwatawala watu wote wa Afrika mashariki na kati.na mpaka sasa wamefanikiwa sana Wanaogoza nchi za uganda,congo na burundi. Tanzania walianxa kutuma makachelo wao ambai wakati wa mkapa tayari kulikuwa na watutsi jeshini tena wenye vyeo vya juu lkn wilipo gundulika haraka waliondoshwa na kurudishwa Rwanda.
Hata baadhi ya watu waliojifanya wanaharakati kama vile general ulimwengu ni mawakala wa wstutsi wiokuja Tanzania kwa kazi maalum. nae alishtukiwa na kutakiwa kuondoka nchini mara moja na sasa anauraia wa kununua.
Vurugu za Congo ni mipango ya makusudi ya inayoratibiwa na kagame na museven ili waendelee kuvuna rasilimali za huko congi DRC ,wameigeuza kongo kuwa shamba la bibi.na wako tayari mupambana na yeyote atakaetaka Congo patulie.
Kitendo cha Tanzania kupeleka jeshi la kulinda amani kongo ni tatizo kubwa kwa maslahi ya Rwanda na Uganda.maana wanaujua mziki wa jeshi la tanzania na bamna walivyo pania kuimarisha amani nchini congo hivyo hawatakaa kimya mpaka Tanzania iondie majeshi yaje nchini Congo.
Watanzani tuweke vyama pembeni katika hili na tusimame pamoja kama Taifa kuwapinga wote wenye nia mbaya na nchi yetu.wapo watakaochangia hoja hii kwa matusi na kejeli hawa ni miongoni mwa wanamtandao wa Kagane na Museven wala sio Watanzania ila wanajifanya watanzania. tuwapuhze tutetee maslahi wa watu wa congo ambao hawana mtetezi kwa miaka mingi tagu mzalendo wa jweli ws congo alipo uawa PATRICE LUMUMBA.

nakubaliana na wewe moja kwa moja....

halafu wale watu wanaongea lugha gani? ukikutana nao wanasema kinaitwa kinyarwanda...hiki kina tofauti na kihutu au kitutsi? au ndo kitusi kimegeuka kuwa kinyarwanda..by virtual
 
very well said. Kikwete is right...

Sana sana Kagame anataka kuharibu mahusiano mazuri yaliyojengeka baina yetu na watakaoumia ni wananchi wa Rwanda....
 
Back
Top Bottom