Ushauri kwa Wanyarwanda: Sioni kosa la Kikwete!

Ushauri kwa Wanyarwanda: Sioni kosa la Kikwete!

Kama yeye Kikwete ameshindwa kukaa meza moja na WANANCHI wake wa Mtwara kutatua mgogoro wa gesi asilia, kwanini basi aishauri Rwanda kukaa meza moja na maadui zake?

Kwanini Kikwete ana preach what he is not practicing?
 
Matatizo ya Rwanda yatadumu milele kama hawatakubali ushauri wa Rais Kikwete kwa kuwa mvutano wa watutsi na wahutu umekuwa kama jadi yao. Watutsi wanaamini ndio pekee wenye uwezo wa kutawala ingawa ndio wachache lakini kwa wingi wao wahutu nao hawakubali kuwa watawaliwa maisha dumu. Ni vyema wakae pamoja wakubaliane mambo ya msingi ya jinsi ya kuendesha nchi yao kwa pamoja la sivyo watakuwa wanaviziana na kunyang'anyana utawala kwa vipindi tofauti. Ubaguzi wao kati yao wenyewe utawamaliza kwa ujinga wa kutotaka kuzungumza na kudharauliana wao kwa wao. Wamshukuru Kikwete kwa kuwaambia ukweli na wamwombe msamaha kwa fikra finyu kuhusu mambo yao.
 
Watanzania tusichokijuwa ni nia ya Rais kagame na Rais Museven kutaka kuitawala Afrika mashariki na kati. chini ya mission yao ya kuuda HIMA EMPIRE .huu ni mpango wa WATUTSI kuwatawala watu wote wa Afrika mashariki na kati.na mpaka sasa wamefanikiwa sana Wanaogoza nchi za uganda,congo na burundi. Tanzania walianxa kutuma makachelo wao ambai wakati wa mkapa tayari kulikuwa na watutsi jeshini tena wenye vyeo vya juu lkn wilipo gundulika haraka waliondoshwa na kurudishwa Rwanda.
Hata baadhi ya watu waliojifanya wanaharakati kama vile general ulimwengu ni mawakala wa wstutsi wiokuja Tanzania kwa kazi maalum. nae alishtukiwa na kutakiwa kuondoka nchini mara moja na sasa anauraia wa kununua.
Vurugu za Congo ni mipango ya makusudi ya inayoratibiwa na kagame na museven ili waendelee kuvuna rasilimali za huko congi DRC ,wameigeuza kongo kuwa shamba la bibi.na wako tayari mupambana na yeyote atakaetaka Congo patulie.
Kitendo cha Tanzania kupeleka jeshi la kulinda amani kongo ni tatizo kubwa kwa maslahi ya Rwanda na Uganda.maana wanaujua mziki wa jeshi la tanzania na bamna walivyo pania kuimarisha amani nchini congo hivyo hawatakaa kimya mpaka Tanzania iondie majeshi yaje nchini Congo.
Watanzani tuweke vyama pembeni katika hili na tusimame pamoja kama Taifa kuwapinga wote wenye nia mbaya na nchi yetu.wapo watakaochangia hoja hii kwa matusi na kejeli hawa ni miongoni mwa wanamtandao wa Kagane na Museven wala sio Watanzania ila wanajifanya watanzania. tuwapuhze tutetee maslahi wa watu wa congo ambao hawana mtetezi kwa miaka mingi tagu mzalendo wa jweli ws congo alipo uawa PATRICE LUMUMBA.
nimekuunga mkono hoja yako kwa nguvu zote mkuumkuu baba! Hata Ben Ki Moo katibu mkuu wa umoja wa mataifa nalijua hilo ndio maana kamwambia museven na Kagame awache kuwasapoti M 23. Mtusi mi mtu hatari sana na kuwapo kwake africa mashariki na kati ni kero kupia hata kuishi na majambazi sabini karibu na Bank. matusi yote wnayotukana ni sio kwa sababu kikwete kabonga kuhusu mazungumzo bali ile chuki ya sisi kupeleka majeshi pale Congo.

Ila umeniuzi kwa neno moja tuu nalo ni kumsifia Lumbumba . Huyu Lumumba ni lilikuwa Comunisti lililokubuhu. Lingepata kutawala nchi ile tuu , zaira isingekuwa na heshima ya kimataifa na kuwa kipenzi kwa utalaamu wa sanaa wake unaovuma duniani kote.
angefuta haki miliki za wanamuziki na kuwafanya wawe masikini kama ilivyokuwa kwa wanmuziki wa kitanzania na zaire isingekuwa na viwanda vya santuli!
angepelka migogoro ya soka vilabuni ili kuzorotesha soka
angefuta makanisa yote na kuwabana kuwa na uhuru wa kuabudu
angefuta ziara ya pele mwaka 1967 kama sisi tulivofuta mwaka 1975
wazaire wangekuwa waimba kwaya sana kuliko kupiga muziki wa danci!

hivyo kifo chale lumumba ni sahihi kabisaaa kuwawa kwa tindikali!
 


Alichokisema Rais Jakaya Kikwete kwenye mkutano wa kutafuta amani nchini DRC hakina ubaya wowote. Pengine kwa kuanza nielezee kwa ufupi alichosema Rais Kikwete ambacho kimesababisha Wanyarwanda wanatahamaki kiasi hiki.


Ajenda ya mkutano ilikuwa ni juhudi za kutafuta amani nchini DRC. Inaeleweka kwamba vikundi vingi vya waasi kutoka nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu vinafanya shughuli zake kutokea DRC. Vikundi hivyo kwa miaka mingi vimekuwa viki destabilize DRC kwakuwa muda mwingi vimekuwa vikiendesha mapigano ndani ya Congo. Juhudi za kuvisambaratisha vikundi hivyo kwa njia za mapigano hazijazaa matunda kwa zaidi ya miaka 19 sasa.


Miaka yote, Tanzania imekuwa ni kimbilio la wanyonge Barani Afrika. harakati za ukombozi wa nchi zote kusini mwa Afrika zimefanyikia Tanzania. Aidha, Tanzania kwa miaka mingi imefanya juhudi za kutafuta amani sio nchini Congo peke yake, bali katika eneo lote la ukanda wa maziwa makuu. Mengi yamefanywa ikiwa ni pamoja na:


1) kuwa msuluhishi katika mazungumzo ya kutafuta amani Rwanda, Burundi
2) Kuwa mwenyeji wa wakimbizi kutoka Rwanda, Burundi, DRC
3) Kupeleka majeshi ya kulinda amani


Kitu kumoja ambacho Tanzania imejifunza katika miaka yote hii, ni kwamba mapigano/vita mara nyingi sio suluhu ya kudumu ya kumaliza uhasama. Mazungumzo ndio njia bora yenye kuweza kuleta maridhiano.


Ipo mifano mingi ya matunda ya mazungumzo. Leo hii kikundi kilichokuwa kinajulikana kuwa ni cha kigaidi nchini Burundi FNL, ni sehemu ya Serikali ya Burundi kwasababu, wote walitoa nafasi ya mazungumzo.


Vikundi vingi vya kigaidi vya DRC, viligeuka kuwa vyama vya siasa na kushiriki kwenye uchaguzi, kwasababu vilikubali mazungumzo.


Leo hii DRC inafanya mazungumzo na vikundi vya waasi na vya kigaidi nchini Uganda ili kutafuta suluhu. Mazungumzo haya yametokana na juhudi za wakuu wa nchi za maziwa makuu ambayo Rwanda ni mjumbe. Hivi nani asiyejua jinsi gani vikundi hivyo vilivyofanya vitendo vya unyama na mauaji kwa wananchi wasio na hatia? Wameua, wamebaka, wameiba.....wamefanya kila jambo hovu, lakini bado imeonekana busara ya kukaa mezani kuzungumza.


Ukiachilia mifano ya kwenye ukanda huu, ipo mifano mingine mingi tu nje ya ukanda.


Nothern Ireland
Yaliyotokea Ireland ya kaskazini kila mtu anafahamu. Maelfu ya watu waliuawa kutokana na vitendo vya kigaidi vya IRA. Lakini mwisho wa yote, Serikali ilikaa nao meza moja, matokeo yake ni amani kupatikana Nothern Irrland.


Msumbiji na Angola
Huko Msumbiji nani asiyekumbuka magaidi wa Renamo walivyoua maelfu ya watu nchini humo. Lakini mwishowe walikaa mezani na Frelimo, amani ikapatokana. Hata Angola, nani asiyekumbuka Jonas Savimbi alivyoua mamia ya wananchi wasio na hatia.


ANC na apartheid
Huko Afrika ya kusini nani asiyejua kwamba maelfu ya watu walipoteza maisha yao kutokana na sera za ubaguzi na manyanyaso ya serikali ya makaburu. Lakini baada ya kuitikia wito wa kuzungumza, leo hii wanaendelea kuishi kama taifa moja.


Jews na wajerumani
Pengine mifano niliyoitoa waweza kusema haifanani na Rwanda,kwakuwa nchi zile haziku experience mauaji ya kimbari. Lakini huko Ujerumani, mauaji makubwa yalifanyika dhidi ya wayaudi. Kila mtu anafahamu hilo. Lakini leo hii ndugu wale hawaendelezi uhasama....


Baada ya mifano hiyo, ni dhahiri kabisa kwamba alichoshauri Rais Kikwete ni sahihi kabisa. Nchi zote za maziwa makuu ambazo zina vikundi vinavyohasimiana navyo, watumie njia ya mazungumzo kama njia bora ya kumaliza uhasama na kutoa fursa kwa wahusika waondoke Congo na kurejea nchini mwao.


Kwa kesi ya Rwanda...sio kweli kwamba kila mwanachama wa FDLR alihusika na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994. Wapo wana FDRL ambao walizaliwa baada ya 1994 na wanaishi exile ikiwa ni pamoja na DRC.


Hivi ni haki kuwajumisha hao kwenye kundi la magaidi waliofanya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994?


Je hatuoni kutoa fursa ya mazungumzo itawawezesha wana FDLR ambao hawakuwa na hatia na wala hawakuwepo mwaka 1994 kupata fursa ya kurejea nchini mwao?


Na je Rwanda haioni busara ya kutumia njia ya mazungumzo itawezesha kufikia makubaliano na waasi hao wawatoe waliohusika na mauaji ya kimbari wakashitakiwe?


Kufanya mazungumzo hakumaanishi ni kutoa msamaha, la hasha. Kufanya mazungumzo ni kuweka mazingira ya kutafuta suluhu ikiwa ni pamoja na kuweka misingi ya kuchukua hatua mbalimbali kwa wahusika.


Wanyarwanda wame overreact na kuwa emotional pasipo kuwa na sababu ya msingi. Rais Kikwete na watanzania kwa ujumla, ni watu wa mwisho kuwa sympathiser wa wanachama wa FDLR waliohusika na mauaji ya kimbari mwaka 1994 na wale wanaoendeleza mapigano hivi sasa huko DRC kwani athari za vitendo vyao vilitugharimu sana.... kwani sio tu vilikiuka misingi ya utu ambayo Tanzania inaiheshimu na kuipigania siku zote, bali pia ilitugharimu kwa kupokea wakimbizi katika vipindi tofauti. Vitendo vyao bado vinaendelea kutugharimu hadi leo. Uwepo wa majeshi ya Tz kulinda amani nchini DRC ni matokeo ya vikundi vya aina ya FDLR kuvuruga amani nchini DRC.

ikumbukwe pia Kitendo cha Tanzamia kuwa Mwenyeji wa Mahakama ya Kimataifa ya Kimbari ICTR, ni ushahidi tosha wa namna ambavyo Tanzania haiungi mkono mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda, haina huruma kwa wale wote walooshiriki katika mauaji ya kimbari. Hivyo, hapa kama kuna mtu wa kuomba radhi, ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda na wanyarwanda wengine wote walio over-react na kumshambulia Rais Kikwete.
Umetoa maelezo sahihi kabisa mkuu. Watawala wa Rwanda na m23 waache kupotosha walimwengu na waongee na FDLR. Kwa asili ya mbari ya hawa wapenda utawala wanajiamini kupita kiasi na kudharau wengine jambo ambalo linaweza kuwaletea tena maafa. Lazima waache kutumia yaliyotokea kama kisingizio cha kuhodhi madaraka. Mifano ipo kama ulivyobainisha wa maadui wa kuuana kufanya mazungumzo na kupata amani ya kudumu. Kagame na wenzake hawawezi kuhodhi madaraka kibabe na kutegemea kuwepo amani ya kudumu. Sisi watanzania tumedhurika sana kwa wakimbizi, kuzagaa kwa silaha na amani kuanza kupotea nchini kwetu tusikubali huu mchezo wa kuchezea shilingi kwenye tundu la choo.
 
Watu hawapendi kuambiwa ukweli...kikwete amewaambia ukweli wanaanza mbwembwe...vita sio suluhisho la matatizo
kweli kabisa nadhani rwanda wanatambuwa duniani hakuna inchi kama tanzania ambayo uzalendo ni asilimia 100% licha ya matatizo yanayo tukabili leo jk aseme piga rwanda ata wasiyo kuwa wanajeshi watatoka na magobere yao nikiwa mmoja wao wakaye mbali kabisa na Tz wacheze na wake zao na siyo watanzania Tz taifa teule
 
Mbona hujasema kwanini Marekani hawakai na Al Qaeda meza moja,Never negotiate with terrorists.

Al Qaeda hawana origin ya nchi moja; ni muungano wa magaidi na wanaojitolea kufanya ugaidi na raia wa nchi mbalimbali; sio nchi moja kama issue ya Rwanda....big difference !
 
Waliwaua tena wengi na mbaya zaidi wakawafuata tena kwenye makambi yao waliyokimbilia DRC mwaka 1997 kipindi kile wanasaidia kumuondoa Mobutu inasemekana watusi waliua wahutu milioni mbili mashariki mwa DRC.Kwa hiyokwa kifupi kama watusi waliokufa kipindi cha genocide mwaka 1994 walikuwa laki 8 then watusi wakarevange kwa kuua wahutu milioni 2 kwenye makambi yao DRC so who is a genocider? haya soma mwenyewe hii link hapa chini
Second Rwanda genocide is revealed in Congo - World news - Africa | NBC News

mkuu ni kweli kabisa,kuna rafik yangu ni mcongo yeye na wazazi wake walikimbilia uganda,walikuwa wanauliwa sana kwa sababu jamii yao imefanana sana na watutsi .alinipa story ilivyokuwa kwa kweli inasikitisha walikuwa wanavamiwa mtaan na majumban wanamiminiwa risasi na mabomu kwa sababu tu wamefanana na watutsi
 


I have to say that I have been taken aback by our neighbors' over-reaction to what is a completely innocuous statement by President Kikwete. What he said could (and should) have been said by other leaders a long time ago. What he said is a no-brainer! It is commonsensical! Negotiations have a much better chance of resulting into durable peace than the use of force. Thus, I find these reactions not only disturbing but also distasteful and utterly impudent! What is even more shocking is the discourteous behavior shown by the Rwanda's Foreign Minister. She seems to be getting too much big for her boots as to suggest that President Kikwete's statement was absurd. She even has the audacity to ask that he should retract it. Ebo! By the same token I think Tanzania's Foreign Ministry should summon the Ambassador of Rwanda in Dar and ask him to clarify these utterances.


For far too long now the international community has adopted a softly softly approach with respect to Rwanda and this has meant that this tiny country gets away with literally everything, even murder. Rwanda has become like a spoiled child - untouchable and overly sensitive to everything even the slightest suggestion of censure. Rwanda has a tendency of not taking kindly any form of criticism whether from within or without. And its leadership comes across as snobbish and delusional. May be the western countries' plaudits have finally got into the heads of Rwandan leaders so much that they think they know it all.


For Rwanda to say that they cannot engage in talks with FDLR rebels because of their role in 1994 genocide is to allow themselves to be the captives of the past. History is replete with numerous instances of former sworn enemies burying their hatchets and extending an olive branch to one another for the sake of peaceful coexistence and future prosperity. This happened in South Africa where ANC and other progressive movements sat down with the perpetrators of one of the most brutal and inhumane policies in the history of mankind (apartheid ) and agreed to work together in an inclusive and democratic society. Similarly, after many decades of committing some of the most heinous crimes against the people of Angola, UNITA is now part of the democratic government of that country. In 2011 US and its allies initiated direct talks with some elements of the Taliban in Doha (Qatar).


Rwanda should wake up and smell the coffee! Being delusional has not worked and won't work. It is now close to 20 yrs since the 1994 genocide and during all that time Rwanda has not been able to achieve its objectives visa vis FDLR rebels through the use of force. Any sane person in Kigali should see the wisdom of changing the tactic/strategy which is, for all purposes and intents, what our President said in the Statement.


But talking of genocide, am I wrong in recalling that even President Kagame himself was once found to be complicit in this crime by a French magistrate? I recall that Rwanda's reaction to this finding was, as we have come to expect, fast and furious to the extent of severing its diplomatic relations with France. Again, this goes to show that this "spoiled child" can't stand any sort of censure or straight talking. I also recall that as recent as last year a UN report revealed that Rwanda's Kagame had committed or assisted in committing genocide in DRC! Despite all this compelling evidence, neighbors of Rwanda are still ready to engage that country in talks. Why can't Rwanda show the same attitude?


Finally, I have a gut feeling that it is not in Rwanda's interest to have the FDLR rebels go away. The perpetual presence of FDLR rebels in DRC gives Rwanda a convenient excuse to interfere into the DRC's affairs thereby making the country ungovernable for its own economic and geopolitical interests. I read somewhere that Rwanda's army – which is one of the biggest for a country of that economy and size - is mainly sustained by the exploitation of DRC's natural resources. So, Rwanda goes into the DRC on the pretext that it is in hot pursuit of the FDLR rebels but in actual fact what it does is to plunder the resources.


And Rwanda is particularly angry with Tanzania because by being part of MONUSCO in DRC, its misdeeds will be curtailed and exposed by our forces. So the over-reaction to President Kikwete's innocuous statement should not be seen in isolation. It is part of the frustration born out of the uneasy situation which Rwanda finds itself in as a result of our troops being part of the UN/SADC intervention force in DRC.
 
Anayefadhili vita ya kongo ni kagame na anafaidika kwa kuondoka na zahabu ..hapa tatizo kuwepo kwa jwtz mana siku chache zilizopita kagame kupitia bbc,cctv alieleza wazi kuwa haungi mkono majeshi ya tz kwenda kongo.. Jiulize kwa nini hataki hata kidogo sbb anajua wazi kabisa jwtz ni jeshi bora katika afrika kwa hiyo ni wazi kabisa masilahi anayoyapata kongo sasa yanakwenda potea..tena nashauri un,jwtz wapeleke jeshi kwenye mipaka yote ya rwanda na uganda ambako kongo inamipaka..yani mtasikia kelele za kagame kutoka shimoni... Tumuunge mkono rais wetu kwa hili mimi nawambia kama jirani yako hana amani kumbuka siku moja lazima wewe utapata mazara yake..angalia wakimbizi walivyokuwa wamejaa tz wameondoka wametuachia jangwa leo mpumbavu wa aina gani anakuja pinga ushauri wa rais jk......
 
Mbona hujasema kwanini Marekani hawakai na Al Qaeda meza moja,Never negotiate with terrorists.
huwezi kufananisha na Al Qaeda, hao ni wapinzani wa serikali ya Rwanda kama walivyo kuwa wapinzani kabla hawajaichukua nchi. Kwani serikali ya Kagame haijaua. Aliye itungua ndege ya rais ndiye aliye sababisha mauaji na anatakiwa ashitakiwe, Kagame hawezi kulikwepa hilo.
 
Mbona hatoi ushauri huu kwa Marekani na kuwaambia wakae chini na Al qaida waongee? Rwanda iongee nini na FDLR?

Usiwe mvivu wa kufikiria, mleta mada ameainisha athari za moja kwa moja ambazo Tanzania inazipata kutokana unrest ya mashariki mwa Congo; sasa Tanzania inapata athari gani za moja kwa moja na mapambano ya ugaidi baina ya Marekani na Al-qaeda. Aidha, kwani alqaeda ni nini? unadhani Al-qaeda ingelikuwa kama FDLR ingeendelea kuwepo? "Mtandao wa Al-qaeda" kwamba hauna sehemu maalum sasa utajadiliana nao nini. Lakini FDLR ni kikundi kinachoeleweka. Hapa ndipo tunapata shauku ya kumpata "kichaa" pale Wizara ya mambo ya ndani ufanyike msako wa makaburi ya babu wa babu yalipo ili tujue kila mmoja asili yake. Hatutozuia mtutsi kuishi nchini lakini ajulikane kuwa mtutsi ili tujue mrengo wake, sio ajifiche nyuma ya pazia na kutuletea dhihaka kwa ushauri wenye kuwafaa wao wenyewe.
 
Kikwete awaombe radhi tu wanyarwanda mambo yaishe, kuliko misuguano inayoanza kuchipuka.

Kikwete karikoroga mwenyewe sasa linamtokea puani. Nafikiri Kikwete alidhani anaongea na wale wazee wa Dar ambao anawapaga pilau na buku tano ali waje kumsikiliza pale Diamond Jubilee akiropoka mashudu yake.

Chezea Kagame wewe!!!
Hakuna kibaya alichoongea Rais wetu. Tuache chuki binafsi. Kagame/ Watutsi si watu wema hata kidogo na wazuri sana kwa propaganda duniani. Jiulize hivi walioua sana kati ya Watutsi na Wahutu ni nani? kuuawa kwa Watutsi kunatangazwa sana kuliko kuuawa kwa Wahutu (second Rwanda genocide). Aliye muua Rais Juvenal Habyarimana ni nani kama sio Vikundi vya Kagame? Huyu ndiye aliye sababisha first Rwanda genocide. Je unajua kuwa serikali ya Rwanda wanawasaidia M23 Kongo? Kwa maana hiyo ni lazima amchukie Rais wetu hata aseme mazuri, kwa kuwa TZ imepeleka majeshi kukabiliana na M23. Jiulize kwanini M23 ni wajeuri sana na wanajiamini?. Kagame ni dikteta na ni adui mkubwa wa Wahutu na usimsifie hata kidogo, anatakiwa rais wa Rwanda atakaye waunganisha Wahutu na Watutsi kwani binadam wote ni sawa
 
mr.president is right...............

ni kweli kuwa alichokisema rais kikwete kipo sawa, wanyarwanda wasikimbie ukweli, mgogoro ndani ya congo ni wanyarwanda waliokimbia makwao.
Wanyarwanda wakae wazungumze na pia uhutu na utusi usiwe kigezo cha majanga ndani ya nchi jirani ya congo drc
 
ni kweli kuwa alichokisema rais kikwete kipo sawa, wanyarwanda wasikimbie ukweli, mgogoro ndani ya congo ni wanyarwanda waliokimbia makwao.
Wanyarwanda wakae wazungumze na pia uhutu na utusi usiwe kigezo cha majanga ndani ya nchi jirani ya congo drc

mitanzania haina akili kabisa..yale yale ya kuomba waalimu jamaica
 
Kikwete awaombe radhi tu wanyarwanda mambo yaishe, kuliko misuguano inayoanza kuchipuka.

Kikwete karikoroga mwenyewe sasa linamtokea puani. Nafikiri Kikwete alidhani anaongea na wale wazee wa Dar ambao anawapaga pilau na buku tano ali waje kumsikiliza pale Diamond Jubilee akiropoka mashudu yake.

Chezea Kagame wewe!!!

Ulevi tu...labda tupe ushauri wako ulitaka aseme nini?
 
Waliwaua tena wengi na mbaya zaidi wakawafuata tena kwenye makambi yao waliyokimbilia DRC mwaka 1997 kipindi kile wanasaidia kumuondoa Mobutu inasemekana watusi waliua wahutu milioni mbili mashariki mwa DRC.Kwa hiyokwa kifupi kama watusi waliokufa kipindi cha genocide mwaka 1994 walikuwa laki 8 then watusi wakarevange kwa kuua wahutu milioni 2 kwenye makambi yao DRC so who is a genocider? haya soma mwenyewe hii link hapa chini
Second Rwanda genocide is revealed in Congo - World news - Africa | NBC News

Hata wale wakimbizi waliohifadhiwa ngara na kigoma ambao aliwazuga kuwa warudi rwanda kuwa vita vimekwisha na hakuna visasi, aliwapiga risasi wote. Jamaa ni chinjachinja ambaye anajifanya mtu mwema.
 
mitanzania haina akili kabisa..yale yale ya kuomba waalimu jamaica

Matusi ni ushahidi wa kukosa hoja. Nadhani umenielewa. Hebu eleza kwa nini kuongea na ndugu yako, ambaye mnagombana, si kitu sahihi katika jitihada ya kutafuta mwisho wa ugomvi.
 
Waliwaua tena wengi na mbaya zaidi wakawafuata tena kwenye makambi yao waliyokimbilia DRC mwaka 1997 kipindi kile wanasaidia kumuondoa Mobutu inasemekana watusi waliua wahutu milioni mbili mashariki mwa DRC.Kwa hiyokwa kifupi kama watusi waliokufa kipindi cha genocide mwaka 1994 walikuwa laki 8 then watusi wakarevange kwa kuua wahutu milioni 2 kwenye makambi yao DRC so who is a genocider? haya soma mwenyewe hii link hapa chini
Second Rwanda genocide is revealed in Congo - World news - Africa | NBC News

Wanyrwanda wanatakiwa kujifunza kusamehe. Mifano iko duniani kote. Tume za maridhiano zimeundwa sehemu zote yalikotokea matatizo na watu wameridhiana na utangamano kurejeshwa. Nimeyaona maoni ya baadhi ya Wanyarwanda yakiwa na mwelekeo wa kumlaani Rais Kikwete na wakimwita genocide sympathizer! Wanakosea kumpa jina hilo Rais Kikwete. Ni vizuri Wanyarwanda waukubali ukweli mchungu kuwa bila maridhiano,kusameheana na kukaa chini na kuzungumza tatizo la Ututsi na Uhutu halitakwisha. Ni kweli Watutsi waliuliwa na Wahutu. Je si kweli pia Watutsi waliwaua Wahutu?
 
Simuungi mkono Rais kwa mambo mengi lakini kwa hili yuko sahihi kwa 100%

Hivi jamani kuna kitu kibaya mtu kutoa ushauri wa maadaui kukaa mezani na watu kumaliza tofauti?

Kwenu Watanzania wenzangu, tunapaswa kufahamu kuwa Urais ni taasisi na alama muhimu ya tiafa letu. Kwenye mambo ya msingi na hasa yahusuyo uhusiano wa kimataifa lazima tumuunge mkono kwa nguvu zote na kusahau tofauti zetu za ndani ya nchi.
 
Back
Top Bottom