Ushauri kwa Wanyarwanda: Sioni kosa la Kikwete!

Ushauri kwa Wanyarwanda: Sioni kosa la Kikwete!

salaama

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2010
Posts
251
Reaction score
325


Alichokisema Rais Jakaya Kikwete kwenye mkutano wa kutafuta amani nchini DRC hakina ubaya wowote. Pengine kwa kuanza nielezee kwa ufupi alichosema Rais Kikwete ambacho kimesababisha Wanyarwanda wanatahamaki kiasi hiki.


Ajenda ya mkutano ilikuwa ni juhudi za kutafuta amani nchini DRC. Inaeleweka kwamba vikundi vingi vya waasi kutoka nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu vinafanya shughuli zake kutokea DRC. Vikundi hivyo kwa miaka mingi vimekuwa viki destabilize DRC kwakuwa muda mwingi vimekuwa vikiendesha mapigano ndani ya Congo. Juhudi za kuvisambaratisha vikundi hivyo kwa njia za mapigano hazijazaa matunda kwa zaidi ya miaka 19 sasa.


Miaka yote, Tanzania imekuwa ni kimbilio la wanyonge Barani Afrika. harakati za ukombozi wa nchi zote kusini mwa Afrika zimefanyikia Tanzania. Aidha, Tanzania kwa miaka mingi imefanya juhudi za kutafuta amani sio nchini Congo peke yake, bali katika eneo lote la ukanda wa maziwa makuu. Mengi yamefanywa ikiwa ni pamoja na:


1) kuwa msuluhishi katika mazungumzo ya kutafuta amani Rwanda, Burundi
2) Kuwa mwenyeji wa wakimbizi kutoka Rwanda, Burundi, DRC
3) Kupeleka majeshi ya kulinda amani


Kitu kumoja ambacho Tanzania imejifunza katika miaka yote hii, ni kwamba mapigano/vita mara nyingi sio suluhu ya kudumu ya kumaliza uhasama. Mazungumzo ndio njia bora yenye kuweza kuleta maridhiano.


Ipo mifano mingi ya matunda ya mazungumzo. Leo hii kikundi kilichokuwa kinajulikana kuwa ni cha kigaidi nchini Burundi FNL, ni sehemu ya Serikali ya Burundi kwasababu, wote walitoa nafasi ya mazungumzo.


Vikundi vingi vya kigaidi vya DRC, viligeuka kuwa vyama vya siasa na kushiriki kwenye uchaguzi, kwasababu vilikubali mazungumzo.


Leo hii DRC inafanya mazungumzo na vikundi vya waasi na vya kigaidi nchini Uganda ili kutafuta suluhu. Mazungumzo haya yametokana na juhudi za wakuu wa nchi za maziwa makuu ambayo Rwanda ni mjumbe. Hivi nani asiyejua jinsi gani vikundi hivyo vilivyofanya vitendo vya unyama na mauaji kwa wananchi wasio na hatia? Wameua, wamebaka, wameiba.....wamefanya kila jambo hovu, lakini bado imeonekana busara ya kukaa mezani kuzungumza.


Ukiachilia mifano ya kwenye ukanda huu, ipo mifano mingine mingi tu nje ya ukanda.


Nothern Ireland
Yaliyotokea Ireland ya kaskazini kila mtu anafahamu. Maelfu ya watu waliuawa kutokana na vitendo vya kigaidi vya IRA. Lakini mwisho wa yote, Serikali ilikaa nao meza moja, matokeo yake ni amani kupatikana Nothern Irrland.


Msumbiji na Angola
Huko Msumbiji nani asiyekumbuka magaidi wa Renamo walivyoua maelfu ya watu nchini humo. Lakini mwishowe walikaa mezani na Frelimo, amani ikapatokana. Hata Angola, nani asiyekumbuka Jonas Savimbi alivyoua mamia ya wananchi wasio na hatia.


ANC na apartheid
Huko Afrika ya kusini nani asiyejua kwamba maelfu ya watu walipoteza maisha yao kutokana na sera za ubaguzi na manyanyaso ya serikali ya makaburu. Lakini baada ya kuitikia wito wa kuzungumza, leo hii wanaendelea kuishi kama taifa moja.


Jews na wajerumani
Pengine mifano niliyoitoa waweza kusema haifanani na Rwanda,kwakuwa nchi zile haziku experience mauaji ya kimbari. Lakini huko Ujerumani, mauaji makubwa yalifanyika dhidi ya wayaudi. Kila mtu anafahamu hilo. Lakini leo hii ndugu wale hawaendelezi uhasama....


Baada ya mifano hiyo, ni dhahiri kabisa kwamba alichoshauri Rais Kikwete ni sahihi kabisa. Nchi zote za maziwa makuu ambazo zina vikundi vinavyohasimiana navyo, watumie njia ya mazungumzo kama njia bora ya kumaliza uhasama na kutoa fursa kwa wahusika waondoke Congo na kurejea nchini mwao.


Kwa kesi ya Rwanda...sio kweli kwamba kila mwanachama wa FDLR alihusika na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994. Wapo wana FDRL ambao walizaliwa baada ya 1994 na wanaishi exile ikiwa ni pamoja na DRC.


Hivi ni haki kuwajumisha hao kwenye kundi la magaidi waliofanya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994?


Je hatuoni kutoa fursa ya mazungumzo itawawezesha wana FDLR ambao hawakuwa na hatia na wala hawakuwepo mwaka 1994 kupata fursa ya kurejea nchini mwao?


Na je Rwanda haioni busara ya kutumia njia ya mazungumzo itawezesha kufikia makubaliano na waasi hao wawatoe waliohusika na mauaji ya kimbari wakashitakiwe?


Kufanya mazungumzo hakumaanishi ni kutoa msamaha, la hasha. Kufanya mazungumzo ni kuweka mazingira ya kutafuta suluhu ikiwa ni pamoja na kuweka misingi ya kuchukua hatua mbalimbali kwa wahusika.


Wanyarwanda wame overreact na kuwa emotional pasipo kuwa na sababu ya msingi. Rais Kikwete na watanzania kwa ujumla, ni watu wa mwisho kuwa sympathiser wa wanachama wa FDLR waliohusika na mauaji ya kimbari mwaka 1994 na wale wanaoendeleza mapigano hivi sasa huko DRC kwani athari za vitendo vyao vilitugharimu sana.... kwani sio tu vilikiuka misingi ya utu ambayo Tanzania inaiheshimu na kuipigania siku zote, bali pia ilitugharimu kwa kupokea wakimbizi katika vipindi tofauti. Vitendo vyao bado vinaendelea kutugharimu hadi leo. Uwepo wa majeshi ya Tz kulinda amani nchini DRC ni matokeo ya vikundi vya aina ya FDLR kuvuruga amani nchini DRC.

ikumbukwe pia Kitendo cha Tanzamia kuwa Mwenyeji wa Mahakama ya Kimataifa ya Kimbari ICTR, ni ushahidi tosha wa namna ambavyo Tanzania haiungi mkono mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda, haina huruma kwa wale wote walooshiriki katika mauaji ya kimbari. Hivyo, hapa kama kuna mtu wa kuomba radhi, ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda na wanyarwanda wengine wote walio over-react na kumshambulia Rais Kikwete.
 
Kikwete awaombe radhi tu wanyarwanda mambo yaishe, kuliko misuguano inayoanza kuchipuka.

Kikwete karikoroga mwenyewe sasa linamtokea puani. Nafikiri Kikwete alidhani anaongea na wale wazee wa Dar ambao anawapaga pilau na buku tano ali waje kumsikiliza pale Diamond Jubilee akiropoka mashudu yake.

Chezea Kagame wewe!!!
 
Kwani huo ushauri alipoutoa alikuwa anaongea na nani? Nadhani hakuwa na nia mbaya ni kwa ujirani mwematu. After all kukichafuka kwao sisi ndo tunaopokea wakimbizi na risasi wanazokuja nazo.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Kikwete awaombe radhi tu wanyarwanda mambo yaishe, kuliko misuguano inayoanza kuchipuka.

Kikwete karikoroga mwenyewe sasa linamtokea puani. Nafikiri Kikwete alidhani anaongea na wale wazee wa Dar ambao anawapaga pilau na buku tano ali waje kumsikiliza pale Diamond Jubilee akiropoka mashudu yake.

Chezea Kagame wewe!!!

Mmeshapata pa kudandia ili kujifariji na hongover ya kufail.
 
Hivi RPF wakati wanateka Rwanda hawakuua wahutu kweli!

Waliwaua tena wengi na mbaya zaidi wakawafuata tena kwenye makambi yao waliyokimbilia DRC mwaka 1997 kipindi kile wanasaidia kumuondoa Mobutu inasemekana watusi waliua wahutu milioni mbili mashariki mwa DRC.Kwa hiyokwa kifupi kama watusi waliokufa kipindi cha genocide mwaka 1994 walikuwa laki 8 then watusi wakarevange kwa kuua wahutu milioni 2 kwenye makambi yao DRC so who is a genocider? haya soma mwenyewe hii link hapa chini
Second Rwanda genocide is revealed in Congo - World news - Africa | NBC News
 
Umeeleza vizuri. Labda kama wana lingine waseme!.

Kwa maneno haya mimi sioni tatizo. Naamini Tanzania kupitia kwa Raisi wetu imetoa ushauri muhimu sana. Ni mtanzania wa ajabu atakaekuwa tofauti na ushauri huu wa watanzania kwa majilani zetu. Tulinde hadhi ya nchi yetu, tuwe wamoja!

Mungu ibariki Tanzania!
 
Mbona hujasema kwanini Marekani hawakai na Al Qaeda meza moja,Never negotiate with terrorists.
 
Jakaya Kikwete yupo sahihi kabisa!
  • Binafsi kuna mambo mengi chini ya uongozi wake siyapendi au hafanyi vizuri au watanzania wengi hawaridhishwi naye...lakini haimaanishi kuwa kwa kasoro hizo, Kikwete hawezi kuwa right!
  • Ndiyo, anazo changamoto nyingi sana nchini mwake za yeye kuchukua hatua...kama vile, kwanini asikae na mtwara meza moja kuliko kutumia jeshi kuhusu mgogoro wa gesi...ili aweze waambia warwanda nao wakae chini waongee na M23....haiondoi ukweli aliousema kuwa; suluhu kwa mgogoro wa DRC, moja wapo ni Rwanda kukaa meza moja M23!...hata shetani kuna wakati yupo sahihi...kwa kumsema shetani mwenzie anayekosea!

Nini Kifanyike;
  • Kwanza ni watanzania kuwa wamoja bila kujali tofauti zetu za kidini na itikadi kwa kuwa nyuma ya rais kimataifa! Kila familia ina matatizo yake so, don't side with anyone against the family.
  • Lazima, kwa kauli moja tulaani kauli za kejeli, kashfa na dharau zilizo tolewa na magazeti ya Rwanda kwa rais wetu! Tukumbuke kuwa kauli yeyote ya Rais wetu nje ya mipaka, ni kauli ya Tanzania na raia wake wote!
  • Kwakuwa kauli hizi za kijinga zimetolewa na magazeti huko Rwanda, kwanini na magazeti yetu yasijibu mapigo ili kueleza alicho maanisha Rais wetu....!? Kwanini yasilaani vyombo vya habari vya Rwanda vyenye kauli chafu kwa viongozi wetu?
 
Watanzania tusichokijuwa ni nia ya Rais kagame na Rais Museven kutaka kuitawala Afrika mashariki na kati. chini ya mission yao ya kuuda HIMA EMPIRE .huu ni mpango wa WATUTSI kuwatawala watu wote wa Afrika mashariki na kati.na mpaka sasa wamefanikiwa sana Wanaogoza nchi za uganda,congo na burundi. Tanzania walianxa kutuma makachelo wao ambai wakati wa mkapa tayari kulikuwa na watutsi jeshini tena wenye vyeo vya juu lkn wilipo gundulika haraka waliondoshwa na kurudishwa Rwanda.
Hata baadhi ya watu waliojifanya wanaharakati kama vile general ulimwengu ni mawakala wa wstutsi wiokuja Tanzania kwa kazi maalum. nae alishtukiwa na kutakiwa kuondoka nchini mara moja na sasa anauraia wa kununua.
Vurugu za Congo ni mipango ya makusudi ya inayoratibiwa na kagame na museven ili waendelee kuvuna rasilimali za huko congi DRC ,wameigeuza kongo kuwa shamba la bibi.na wako tayari mupambana na yeyote atakaetaka Congo patulie.
Kitendo cha Tanzania kupeleka jeshi la kulinda amani kongo ni tatizo kubwa kwa maslahi ya Rwanda na Uganda.maana wanaujua mziki wa jeshi la tanzania na bamna walivyo pania kuimarisha amani nchini congo hivyo hawatakaa kimya mpaka Tanzania iondie majeshi yaje nchini Congo.
Watanzani tuweke vyama pembeni katika hili na tusimame pamoja kama Taifa kuwapinga wote wenye nia mbaya na nchi yetu.wapo watakaochangia hoja hii kwa matusi na kejeli hawa ni miongoni mwa wanamtandao wa Kagane na Museven wala sio Watanzania ila wanajifanya watanzania. tuwapuhze tutetee maslahi wa watu wa congo ambao hawana mtetezi kwa miaka mingi tagu mzalendo wa jweli ws congo alipo uawa PATRICE LUMUMBA.
 
Tanzani ni Taifa kubwa katika diplomasia za kimataifa tangu enzi za Mwl. Nyerere. Rais Jakaya nfie alieumaliza mgogoro wa kenya kati ya Raila odinga na Kibaki. Mgogoro wa CCM na CUF zanziber na sasa wazanziber wamekuwa wamoja. naamini hata mgogoro wa congo akipewa nafasi ataumaliza.
 
Tatizo la uchambuzi wako ni kukosa hisoria ya FDLR na kilichotokea kipindi na hata baada ya mauaji ya 1994. Sio mambo yote yanatatuliwa kwa kukaa chini na kuongea. Mbona hatoi ushauri huu kwa Marekani na kuwaambia wakae chini na Al qaida waongee? Rwanda iongee nini na FDLR? Hata baada ya kupatikana kwa amani Rwanda wakimbizi wakaambiwa warudi, hawa jamaa hawakurudi, kwanini hawakurudi wakati wakimbizi wengine walirudi. Kwanini kama mtu kakosea msimwambie tu kuwa kakosea? Angeongela mambo mengine bwana, alikuwa na mambo mengi ya kuongea hili kachemsha kwa wale ambeo wanajua historia ya Rwanda
 
Watu hawapendi kuambiwa ukweli...kikwete amewaambia ukweli wanaanza mbwembwe...vita sio suluhisho la matatizo
 
Kikwete awaombe radhi tu wanyarwanda mambo yaishe, kuliko misuguano inayoanza kuchipuka.

Kikwete karikoroga mwenyewe sasa linamtokea puani. Nafikiri Kikwete alidhani anaongea na wale wazee wa Dar ambao anawapaga pilau na buku tano ali waje kumsikiliza pale Diamond Jubilee akiropoka mashudu yake.

Chezea Kagame wewe!!!

unajua ktk binadam kuwa wapo wana vichwa vyenye akili na wengine wana uji...sasa napata wasiwasi huenda na wewe nazi yako imejaa uji....msimamo wa tanzania siku zote huwa ni amani kwa njia ya majadiliano sio kwa njia ya vita....kikwete ameegemea kwenye asili ya mtanzania.
 
Mbona hujasema kwanini Marekani hawakai na Al Qaeda meza moja,Never negotiate with terrorists.
hIVI wewe mpaka leo hujui kuwa Al Qaida ni shetani. wao huonesha tape tuu lakini wamejificha sasa marekani itajadiliana na shetani ? D.I Y-do it youself!!
 
Juzi Rwanda ilikasirishwa na ushauri wa Rais wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete, baadhi ya Watanzania walikurupuka kwa kupinga, wengine katoa lugha ya kukashifu kauli ya Rais Kikwete. Lakini tunatakiwa kufikiria kwa upana madhara yanayosababishwa na waasi katika nchiza ukanda huu. Lazima tukumbuke kuwa hawa waasi wa Rwanda wanaishi nchi gani? Je, wapo nchini Rwanda? Jibu ni hapana. Hivyo nchi ambazo zinaumia na mgogoro huu siyo Rwanda pekee bali na nchi jirani kama CONGO DRC, BURUNDI, TANZANIA NA UGANDA. Tutafakari kwa umakini haya:-


  1. Kwa kuwa Rais Kagame hataki waasi walete madhala katika nchi yake hivyo anajitahidi kuwaweka mbali na nchi yake, yaani zero grazing katika nchi jirani. Hivyo hataacha kuvisaidia vikundi mbalimbali kama M23 na vingine huko CONGO ili kuzuia kuingia Rwanda.
  2. Waasi wanapataje huduma zao za kila siku pamoja na siraha? Kama siyo kuingia katika nchi za Tanzania, Uganda na Burundi kwa kusudi la kuuza siraha, kuua na kuiba rasilimali kama tembo ili kupata pembe za ndovu au kuhusika katika matukio mbalimbali ya utekaji wa magari na raia. Kumbuka kila kukicha siraha nzito kama SMG na risasi zake hukamatwa katika mikoa ya pembezone mwa Tanzania.
  3. Kama waasi wa Rwanda wataendelea kuishi nje ya Rwanda ni lini Kagane ataamini kuwa hawataisumbua serikali ya Rwanda?
  4. Baadhi waasi wamekimbilia nchi za jirani kama Tanzania na kujichanganya na raia hivyo ni hatari kwa usalama wa nchi yetu.
  5. Madhala ya wakimbizi ni makubwa, kumbuka kila vita inapotea katika ukanda huu nchi ya kwanza kupokea wakimbizi wengi ni Tanzania.

Rais ni taasisi naamini rais wetu hakukurupuka, wameshafanya utafiti wa kutosha na wakagundua vita ya KONGO haiwezi kuisha kama waasi wa Rwanda wataendelea kuwepo CONGO DRC.
 
Mr.President is right...............
 
Back
Top Bottom