Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 55,030
- 59,683
Hao mafisadi wote ni ccm
bank ya vatican ndo imewafundisha mkombozi bank jinsi ya ku laundry pesa,juu wao wana uzoefu tangu kipindi cha adolf hitler
Hongera sana mkuu endelea kuwashauri waelimike hawa jamaa!wakati taifa likihitaji shule nyingi na vyuo vikuu nyie mnadai kadhi???
Sasa sijui kama chuo cha morogoro waislamu wote,wala si mbaya,mi shuleni mwislamu nilikua mimi tu katika watu karibu 500,kwahiyo siyo ishu.Kwani chuo kikuu cha kiislamu morogoro wanafunzi wanasoma bure??? Pamoja na kwamba wote ni waislamu.
Kadhi...kazi au kadhi?? naogopa nsije zimia mie
Kulikuwepo na east africa muslim welfare society kama sikosei,na ilikuwa imewekeza katika elimu na mashule etc.Mkuu Uko Sahihi! Lakini Kuna Kitu Ambacho Wanadai Kimeua Taasisi Nyingi Za Kiislam Toka Kianzishwe! Nacho Ni BAKWATA Ambayo Wengi Wao Hudai Ni Chombo Kinachosimamiwa Na Sirikali. Dhehebu La AnsarSuna Ambalo Mara Nyingi Hupingana Na BAKWATA Ndilo Sehemu Pekee Ya Uislam Ambayao Ndio Yenye Kuangaza Maendeleo Ya Uislam Tz, Ndio Walioanzisha Chuo Kiku Cha Kislam Morogoro, Ndio Wenye Vyombo Vya Habari Mfano Tv Iman, Radio Iman, Saut Ya Quran,magazeti Ya Alhuda, Anuur Nk. Lakini Bakwata Sijajua Wanamiliki Nini. Hawa Hawa Ansarsuna Ndio Hawaitaki Kabisa Mahakama Ya Kadhi Ila BAKWATA Ndio Wanaoipigania Mahakama Ya Kadhi. Hata Mimi Nashawishika Kuamini Kua BAKWATA Ndio Wanatakiwa Kubebeshwa Lawama Zote.
haa haa suala la ufisadi halina dini mkuu, unawakumbuka kina daudi balali? Kina rostam aziz, jakaya kikwete walivyohusika kwenye Epa? Mkuu sio vizuri matendo ya mtu kuyaingiza moja kwa moja kwenye imani au dini yake. Kwa mfano ikiwa muislamu mmoja amezini, huwezi sema uislamu unapenda uzinifu kamwe! Pia suala la kanisa kupewa fedha na serikali tuwekee uthibitisho hapa!Na mimi kama Muislam nakushauri huu ushauri wako upeleke Kanisani.
Kawaambie hivi toka toka uhuru mpaka sasa wasomi wa Kikirsto wamejazana serikali kila idara wamelisaidiaje taifa letu kutoka kwenye nchi masikini duniani, unajua kuwa Tanzani ipo kwenye nchi 20 masikini wa kutupwa duniani huko serikalini kazi yenu kufanya ufisadi tu.
Halafu nyie Wakirsto ndiyo mnabebwa unajua kama kila mwaka Kanisa linapewa bilioni 61.9.
Ahsante.
haa haa nakushukuru mkuu kwa kusema ukweli, ufisadi ni ufisadi tu.Ufisadi Tanzania hauna dini. Tangu lini Kikwete akawa Mkristo?
mkuu hongera sana kwa ushauri mzuri hawa kama hawataki kusikia yatakuja kuwatokea puaniWanaJF,
Nimefikiria muda mrefu kuhusu sakata hili la kufa na kupona la mahakama ya kadhi. Ni wazi kuwa mahakama ni muhimu katika jamii. Lakini pamoja na umuhimu wake, nadhani tukikaa chini na kutafakari, kuna mengi ya umuhimu zaidi. Jambo la kwanza kwa Nchi kama Tanzania ambayo kwaajili ya uongozi mbovu wa waliokuwa madarakani kwa nyakati tofauti lingepaswa kupewa kipaumbele ni Elimu. Ona jinsi Elimu inavyochezeshwa gwaride, hadi tumefikia hatua ya kuweka div. 5, ili kuficha waliofeli.
Nirudi kwenye mada,
Nasema ushauri kwa waislamu kuwa waongeze nguvu kwenye elimu dunia. Waongeze shule zinazoendeshwa na taasisi za kiislamu, zenye ubora. Waongeze vyuo vikuu vinavyoendeshwa na taasisi za kiislamu, wakitaka wawapokee waislamu tu haidhuru, lakini ni bora wakawapokea wote kama zifanyazo taasisi za kikristu. Elimu bora Tanzania inahitajika. Na Elimu bora Tanzania haiwezi kutolewa na Serikali tu. Ona madhehebu ya kikristo walivyoweka kipaumbele katika elimu. Hesabu tu vyuo vikuu vinavyoendeshwa na madhehebu ya kikristo. Hesabu shule za sekondari zenye ubora wa hali ya juu zinazoendeshwa na taasisi za kikristo. Sijui taasisi za kiislam zinaendesha vyuo vikuu vingapi, lakini nafahamu walau moja ile ya Morogoro, iliyokuwa chuo cha Tanesco, ambayo walipewa na serikali ili kuwatuliza.
Tazama kwenye afya, ona ni vituo vingapi vya afya, hospitali, hadi hospitali za rufaa zinazoendeshwa na taasisi za dini? Nafahamu walau hospitali ya rufaa ya KCMC na Bugando zinaendeshwa na taasisi za kikristo. Hospitali za kawaida ni nyingi. Zinazoendeshwa na taasisi za kiislamu sizifahamu, zinaweza kuwa nyingi kuliko hizo, au la. Kwenye suala la afya ndipo pa kutumia nguvu nyingi. Huko ndipo pa kuwa na hitaji la kuweka kambi Bungeni kama kutakuwa na haja.
Nadhani sio vizuri kusubiri siku zote kubebwa na serikali. Kila madhehebu wana sheria zao, sheria zao ambazo hazipaswi kwenda kinyume na sheria za Nchi. Sioni sababu ya kutumia nguvu kubwa kudai mahakama badala ya kuwekeza kwenye mambo ya maandeleo kama elimu, afya, nk. Kwanini tunadhani maisha yetu lazima kupelekana mahakamani?
Ndiyo maana nasema natoa ushauri kwa waislamu hasa waJF maana ndo watakaosoma ushauri huu, Waislamu wawekeze nguvu nyingi kwenye mambo ya maendeleo zaidi kuliko mahakama. Wawekeze kwenye elimu na afya. Achaneni mambo ya mahakama. Mahakama ya nchi inaweza kumaliza yote, ikiwa kutakuwa na haja. Lakini kwa mtu optimistic hawezi kutumia nguvu nyingi kwenye hilo.
Sio haki kwa wabunge: wawakilishi wa wananchi kupoteza muda kujadili kuwa waislamu wawe na mahakama ya kadhi au la. Ni wazi watajadili, hasa wakati huu tunapokaribia uchaguzi. Ili kila mchangiaji aonekane anawajali waislamu, ataunga mkono mahakama ya kadhi, watafanya funika kombe mwanaharamu apite. Ili tu waislamu wa jimbo lake wasimtose, ili tu waislamu wasikikatae chama chake. Lakini nasema tena sio haki wabunge wapoteze muda katika jambo hili ambalo sio kipaumbele cha taifa. Sio haki lakini litajadiliwa kwaajili wa woga wa kupoteza kura.
Mniwie radhi, kama kuna moja hatapendezwa na ushauri wangu. Ukweli utabaki kuwa kuwekeza kwenye elimu, hasa elimu dunia na afya ni bora kuliko kuwekeza kwenye mahakama.
uislamu wa kikwete sio hoj watendaji wa chini ni WAPAGANI?NDO MAANA DK IDRISA alipigwa vitaUfisadi Tanzania hauna dini. Tangu lini Kikwete akawa Mkristo?
Wakitumia neno la kuudhi dhidi yangu, wala sio tatizo, hata wakindiitukana. Ila ukweli utabaki huu, na ukweli huu utawasuta siku za usoni.
hawa watu wanatakiwa kusoma hata kama ni kwa lazima kwa sabbu kwa kweli, kukosa kwao elimu ndiko kunakopelekea wawe wanaongea wanayoyasema. Jamaa hawanaga uwezo wa kujenga hoja, jamaa hawana uwezo wa kuelewa hata simple phrases, halafu hawajui kama hawaelewi, jamaa hawana uwezo wa kujadili kwa point wala kujibu swali kama linavyoulizwa; jamaa hawa kwa kujua hawana hoja wamejikita zaidi kwenye ubishi wa kila kitu kwa makelele, matusi, fujo na vitisho.
Terror approaches!. Utasikia wanasema "msipotupa hiki mtaona", msipofanya hivi, tutaonyeshana adabu", mara utasikika, "...mkikataa hiki, tutafanya kama boko haramu",.."mahakama ya kadhi ni lazima hata kwa jihadi". Hivi kinachowafanya wawe na approach za kigaidi ni mafundisho ya dini yao au ni ujinga na kukosa uwezo wa kujenga wala kuelewa hoja?
Ninakwenda kazini lakini usishangae watakapokuja hapa,yote niliyoyasema pale utayaona. Matusi, vitisho, nguvu, fujo, vurugu za kijinga tu.
Ni afadhali serikali ilazimish waislam wote waende shule hata kama ikibidi ziwepo za watu wazima ili angalau halmashauri zikae kwenye order badala ya mahakama ya kadhi. Mahakama ya kadhi hawana uwezo wa kuiendesha na itazidisha migogoro miongoni mwao. Hainatija kwa taifa na hata kwa waislam walio wengi. Sana sana itanufaisha wale wanaotafuta kuajiriwa kule, na wanaoume wanaoamini katika ubabe dhidi ya wanawake na watoto wa kike. Hakuna la ziada.
Mahakama za kadhi ziko na zinafanya kazi, kwa nini leo zijadiliwe na bunge? Hizi ni za kidini, kwa nini ziingizwe kwenye katiba hata kama serikali haizihudumii? Wawaachie masuala yao ya kidini wayafanye wenyewe misikitini. Si jukumu la serikali kuweka kwenye katiba masuala ya dini.
haa haa suala la ufisadi halina dini mkuu, unawakumbuka kina daudi balali? Kina rostam aziz, jakaya kikwete walivyohusika kwenye epa? Mkuu sio vizuri matendo ya mtu kuyaingiza moja kwa moja kwenye imani au dini yake. Kwa mfano ikiwa muislamu mmoja amezini, huwezi sema uislamu unapenda uzinifu kamwe! Pia suala la kanisa kupewa fedha na serikali tuwekee uthibitisho hapa!
Sasa kwa taarifa yako chanzo cha madai ya mahakama ya kadhi ni kuwepo kwa hicho chuo cha kiisilamu kilichopewa majengo ya Tanesco. Jamaa walipopewa wakaanzisha shahada nyingi za elimu ya kiisilamu kama vile Bachelor of Laws with Shariah na Bachelor of Islamic Studies with Education. Kinachowaumiza kichwa ni kwamba wahitimu wawapeleke wapi? Ndipo madai ya kuanzisha mahakama za kadhi zinazogharamiwa na serikali yalipoanza kushika kasi....Sijui taasisi za kiislam zinaendesha vyuo vikuu vingapi, lakini nafahamu walau moja ile ya Morogoro, iliyokuwa chuo cha Tanesco, ambayo walipewa na serikali ili kuwatuliza ...