Ushauri kwa wadada ambao ni michepuko ya waume za watu

The only

JF-Expert Member
May 19, 2011
10,433
13,417
Kwanza kabisa nianze kwa kuwapongeza kwa huduma ya penzi lenu mwanana hakika mna mahala penu mbinguni.

Ushauri niliowaitia hapa ni kuwa dada zangu mnajisahau sana:

1. Unapokuwa mchepuko tambua kuwa wewe ni wa mda mfupi kwa msela, hivyo kaa kijanja ,uwezekano wa mchepuko kuzidi miaka mitano huwa mdogo, dada mtumie huyo kujijenga kiuchumi au kimaarifa ukiwa naye, mdada anakusimulia et jamaa ananipa laki 5 za matumizi kila mwezi siwezi muacha, mimi nilidhani uje na mikakati ya kuhakikisha unaweza kuishi bila yeye, yaani save fikilia biashara hizo laki tano ukiingiza kila mwezi laki 3 kwenye duka lako la nguo baada ya 3yrs siku anaondoka unaenda kulilia hotel Zanzibar.

2. Ukiona anakupa thamani kuliko mkewe basi dada jua unadate na muhuni, mama hata akikuoa ww atathamini wengine, hebu epuka dhambi zisizo na lazima plz kuwa mwanamke mwema kataa hizo mambo kumfungia mme wa mtu weekend nzima ni raha kwako ila dada kuna maisha baada ya kufa, amekupenda msaidie akili yako maana yake hana.

3. Usiache kuyapangilia maisha yako nje ya mume wa mtu, waza utaolewa na nani unataka nini kwenye maisha na ujue yeye hayupo kwenye maisha yako ni rafiki tu wa faida

KWANINI NIMEPANIC KUSHAURI?

Mimi mme wa mtu na watoto 3 na naipenda familia yangu kuzidi chochote, katika miaka 12 ya ndoa hii nimebadili michepuko 6 ila mke ni huyu huyu, maishani nimejaliwa kupata michepuko smart yote hakuna asinipigia simu na kunimisi wawili leo ni wake za watu na wanahela kunizidi na mm wanakiri ndo nimewaonesha njia.

Haba juzi kati nlipata ka-single mother nikakaelewa kukala mala mbili tatu nikaomba nijue maisha yake, ni kwamba msela alimzalisha kwa kuzuga anatoa mahali alitoa hadi uchumba akatoka nduki, dada kapanga uswaz ana binti wa miaka 7, basi nikamueleza mm nataka awe mchepuko wangu ila sitaki uzazi nataka tustarehe ila in return nitajenga maisha yake, nikamtoa chumba cha Tshs 25 uswazi huko nikamhamishia eneo nikalipa Tshs 60 miez 6, kwa kuwa alikuwa anafanya mgahawa ni nkamwambia tafuta eneo nikuwekee kabiashara akapata frame nkalipa ths 300k miez 3 na cash700 afungue nkamuahidi kadili tukijaaliwa nataka auze vinywaji etc nshaongea na msela wangu wa mafriji akanambia tafuta rejeta laki kava atampa shemu wake bure.

Cha ajabu? Dada amehamia kuniganda simu hapa na hapa, juzi kaniibukia baa et toyo wamesema wameniona na mtu, nkamwambia mm mbona sijamkataza akipata mtu wa maana wadumu sina FUTURE naye ikawa valangati, anatuma SMS ooh luku imeisha luku yake mwezi 7000 mtu anauza hadi laki, yaani kifupi hana lengo la kujitegemea ili aamue anidate kwa kunipendea hela au independent.

HITIMISHO
Michepuko tunawapenda sana lakini mnapaswa mjue nafasi yenu, hakuna mwanaume anachaguliwa mchepuko, unampenda mwenyewe ukiondoa penzi na support ya kukufanya ujitegemee huna urithi, hata ukisema tuzae unambania mwanao nafasi ya kufurahia penzi la baba kama nalowapa wana wamke wangu halali, MJITAMBUE.
 
Mke wako naye anamegwa kama unavyomeva, kama ume badili 6 yeye kabadili 7
Hilo halinipi shida kabisa , as long as mm ananitreat vizuri inanitosha kabisa , naamini pia ana siri zake ila nampa nafasi ya heshima anatulea vyema mm na wanae , kama ww huchepuki ni kwa faida yako mbinguni haikuhakikishii kutochapiwa mkuu
 
Hongera kwa kubadilisha michepuko 6 mkuu
Jitahidi kuongeza wengine…
Kiongozi kwa wanaume nipo top 10 ya watulivu 12 year sita tuu???na sifanyi masifa i fallen in love with each at her time
 
Huwa naona mwanaume ni mpumbavu hasa yule anajisifia kua na mchepuko wakati teyari yuko katika ndoa.

Inaonesha jinsi gani mtu unaye ishi naye huna hisia, ndio maana hujutii ata kimoja unachofanya kwake. Ila unaogopa kuvunja ndoa kisa jamiii itakuonaje
Nilijalibu kushauri mausiano siku mmoja Nilijuw wanaume tunawatesa sana awa watoto wakik
 
Back
Top Bottom