Karibuni kwa ushauri

mambio

JF-Expert Member
Mar 4, 2017
2,348
2,776
Kipindi linatokea hilo tukio mimi nilikuwa ni mgeni kwenye hiyo mitaa kuna biashara yangu niliihamishia huo mtaa.

Nyumba niliyokodi frem nilikuta yeye akiwa tayari anabiashara hapo,
nilihamia hapo kipindi akiwa na mgogoro na mmewe, kwa maana hiyo mume sikuwahi kukutana nae wala kumfaham, alikuwa kaondoka nyumbani na kumuacha mke na mtoto.

Mke ni mtumishi wa umma mume ni msomi anayemiliki vyeti. Hajabahatika ajira.

Baadae walikuja kusuruhisha.tofauti zao mume akarudi maisha yakaendelea.

Leo nimepata ujumbe wa yule mwanamke akiniomba maongezi anajambo lake anahitaji ushauri.

Sijaweza kukutana naye maana ratiba ilibana, nikamuomba tuongee kwa simu. Akashindwa kuongea akaniomba tuchart.

Anadai mme wake ni dhaifu sana ila yeye ameamua kumvumilia sababu anampenda.

Anasema zamani alikuwa wanaweza kunyanduana kwa week mara 2, ikaenda ikawa kwa week mara 1, ikafika hadi kwa mwezi na sasa wanakaa hadi miezi kadhaa jamaa kazi hakuna.

Mbaya zaidi anadai mwezi ujao wanatakiwa wafunge ndoa na ipo kwenye mchakato michango na mambo mengine.

Anasema amejaribu kushirikisha baadhi ya ndugu wamekuja kuongea na mumewe ila mume anadai ni stress tu zinasumbua.

Closed/ ushauri umetosha
 
Ndugu mwandishi siku ukifumwa ndo utajua yaliomo yamo au hakuna. Tena mshikaji atakunywa supu ya pweza alikasusu na mkongo watakupakia
Kiongozi kuwa serious kidogo.
Huyo binti kaomba ushauri.
Nazani kilichopo hapa ni kushauri tu.
Km umeangalia hizo charting hazina hayo mambo.
Km unaushauri wowote karibu mkuu.
 
Mwambie aolewe,kuhusu kukaza akuachie wewe
Kwangu mimi hapana.
Nna familia bora sitaki kuivuruga.
Km kuna ushauri wowote karibu.
Mimi nimemwambia ajaribu kwenda hospitali mguu kwa mguu na mumewe watashauriwa cha kufanya huko.
 
Na wewe kuna mtu anaambiwa hivyo hivyo na mwanamke wako kua wewe ni dhaifu,usiamini maneno kama hayo,hakuna ukweli wowote hapo,

Namuonea huruma huyo jamaa anataka kuoa malaya,

Alikuuliza wewe kama gia tu ya kutaka umtafune.
 
Hawa ni wanandoa au mahawara?

Unawaitaje mume na mke na bado hawajafunga ndoa?

Acha shobo kwenye mahusiano ya watu
Walifunga ndoa bomani, hivi inarudiwa tena kanisani na wanawatoto tayari.
Sina Shobo mzee nina majukumu yangu ila tu nimeombwa ushauri.
Sana sana nadhani ni ushauri jinsi ya kumrudisha kidume mwenzetu kwenye afya kamili.
Ushauri mwema ntakaopata hapa nitampa aliyeuhitaji.
 
Daaaah. Masikhara ila kweli aisee. Waongee tu na mwenzie. Wakiweza wakatishe mahusiano yao.
 
Walifunga ndoa bomani, hivi inarudiwa tena kanisani na wanawatoto tayari.
Sina Shobo mzee nina majukumu yangu ila tu nimeombwa ushauri.
Sana sana nadhani ni ushauri jinsi ya kumrudisha kidume mwenzetu kwenye afya kamili.
Ushauri mwema ntakaopata hapa nitampa aliyeuhitaji.
Kama walifunga ndoa bomani hiyo tayari ni ndoa sema wanataka kufanya sherehe ya harusi sio kufunga ndoa

Mwombe namba za kidume wake ili uumshauri
 
Back
Top Bottom