Ushauri kwa TCRA kitengo cha Tovuti

Mr Why

JF-Expert Member
Nov 27, 2019
1,117
1,915
TCRA napenda kuwashauri kuhusiana na tovuti hasa zinazo onesha maudhui yasiyo faa. Napenda kuwashauri kuwa hakuna haja ya kufungia tovuti za ngono kwasababu tovuti hizo haziwafuati watumiaji na wala hazilazimishi watumiaji kuzifuata bali ni watumiaji ndio wanaozifuata.

Kitendo cha TCRA kuzifungia hii inaonesha dhahiri kuwa mnamapungufu makubwa sana wala hamfanyi kazi kwa weledi ni sawa na ninyi kuwa waoga.

Badala ya ninyi kuzifungia basi mlipaswa muwasiliane na wamiliki wa tovuti hizo muweke utaratibu wa watumiaji kuingia kwenye tovuti hizo kwa gharama kubwa tofauti na tovuti nyingine.

Kitendo cha watumiaji kuingia katika tovuti hizo kwa gharama kuwa kingewaongezea ninyi mapato makubwa lakini mpaka sasa hamjafikiri hilo mnawaza kufungia na ukizingatia maamuzi kama haya ni maamuzi ya watu washamba ni sawa na maamuzi ya wanyama na sio binadamu.

Nchi zilizoendelea kama Marekani kila tovuti ni huru wa kuwa hewani wao wanazingatia umri kwa watumiaji wake kwa kufanya Verification za umri nakadhalika huku Serikali yao ikiendelea kupata mapato makubwa sana kupitia tovuti hizo.

Acheni fikra za kufungia mitandao na badala yake tizameni jinsi gani mtapata mapato kupitia tovuti hizo kwa kufanya hivyo ni dhahiri kuwa mna utimamu wa akili.

Kitendo cha kufungia tovuti ni upumbavu mkubwa kwasababu watumiaji bado wanaweza kuingia kwa kupitia Virtual Private Network tofauti na mwisho wa siku mnaonekana kama washamba na jambo jingine msilolifahamu ni kuwa binadamu hafai kuzuia hilo wekeni akilini mwenu.
 
Back
Top Bottom