Ushauri kwa Serikali kuhusu Shambulizi na utekaji wa Bandari ya Msumbiji na IS

Hapana, ni huyu mmakonde ni mwenzetu kabisa na ni zao la Nachingwea.

Hivyo kama magaidi wameingia Msumbiji na yeye yupo, wewe waona nisimpe changamoto?
Mkuu, hata Chechnya iliwahi kuwa na makundi kama haya japo ilikuwa chini ya himaya ya Urusi.

Hivyo kuzuka kwa haya makundi haijalishi nani yupo madarakani.
 
Nimeone Nyusi leo alikuwa mtaani anatembelea wahanga wa mashambulizi wa hao magaidi. Problem sisi waafrika ni rahisi kugawanyishwa kwa propaganda uchwara tu bila kufanya critical analysis. Msumbiji ni kama imeiweka Tz nje ya equation kwenye kupambana na hao maharamia, ni kama vile wanatunyooshea kidole na sisi. Na mbaya zaidi ndio kachukua kiti cha SADC sasa sijui hali itakuwa vipi..

JW iweke buffer zone na kupiga doria kali ukanda huo. Kama hakuna kuaminiana na kunyoosheana vidole kwa kuwa hapo jirani tunapajua vizuri coverts ops ku pre empty na ku paralysis hicho kikundi ni muhimu. Hadi pale kutakapokuwa na common understanding ya kukabiliana na hili tatizo kwa pamoja.
 
Mkuu, hata Chechnya iliwahi kuwa na makundi kama haya japo ilikuwa chini ya himaya ya Urusi.

Hivyo kuzuka kwa haya makundi haijalishi nani yupo madarakani.

Mkuu, hili kundi halizazuka tu ghafla.

Kudorora kwa ulinzi na usalama ndio chimbuko la kikundi hiki, kupewa silaha na vifaa vyote vya vita.

Inawezekana kabisa masalia ya RENAMO yamejikita humo au watoto wa "vetarans".

Sasa haya yote yanahitaji kuwa macho kama serikali na vyombo vyake vya ulinzi.
 

Nadhani pia ile operesheni ya kwanza ilikuwa ni kuhusu kulinda "parameters".

Sasa hivi kuwe na mipango thabiti ya kupiga kambi ndani kabisa kwa ushirikiano wa ki-SADC.
 
Fact
 
Nadhani pia ile operesheni ya kwanza ilikuwa ni kuhusu kulinda "parameters".

Sasa hivi kuwe na mipango thabiti ya kupiga kambi ndani kabisa kwa ushirikiano wa ki-SADC.

Yes, nadhani saiv eneo lote kwa upande wa mpakani huko liko mikono salama. Ila ndio kuwa macho muda wote.

Naona ni mapema sana kuingia huko ndani kukiwa na mwanga mkali mchana. Hawatuamini hao watu maana washaaminishwa vibaya hivyo sidhani kama watapokelewa vizuri hao JW. Tukabie kwenye mstari tu.
 
Ni lazima pia tujiandae na gharama zitakazoambatana na kuipa msaada wowote Mozambique dhidi ya hili kundi. Huenda hatuna tofauti kubwa sana nao kiusalama ni mapema sana kuwaita wazembe. Kinachoendelea kule tumekiona kikianza, kustawi na kukomaa kule Nigeria. Tumeona harakati za Kenya na Uganda kule Somalia na gharama zake. Tunawazidi nini?
 

Kabisa, na cha muhimu kwa sasa ni mkutano wa pamoja wa wakuu wa SADC.

Kama AU iko kimya kwenye masuala kama haya baso SADC ionyeshe mfano kwa kuanza kushughulikia regional issues.

Uko rght unaposema sisi waafrika tuna shida.

Yaani kule Magharibi wameshindwa kuisaidia Nigeria na Boko Haram.

AU ndio wamelala usingizi wa pono hakuna hata kauli kuhusu hali hii.

Waafrika tuna safari ndefu sana.
 

Afrika ni kila mtu apambane na hali yake style. Na hii ni kwasababu tunategemea nchi za nje sana kibiashara kuliko sisi wenyewe kwa wenyewe ndio maana hakuna anejali nchi ya mwingine. Na tukiwa wamoja tutawakosesha maslahi hao wakubwa wanaotuletea silaha na kupora rasilimali zetu.

Kungekua na intra-trade ya kueleweka hapa Afrika huu upuuzi usingekuwepo maana nchi zingeshirikiana kwa pamoja kuhakikisha kuna usalama wa kutosha ili kurahisisha movement za watu, huduma na biashara zingine.

Changamoto hizi za kiulinzi zingetatuliwa kwa pamoja na kwa kushirikiana. AU ni toothless dog haina msaada wowote. Kweli hiki ni kipimo kikubwa kwa SADC. Inatakiwa block hii iwe mfano kwa kutatua hali ya msumbiji kwa haraka.
 
Tukijitoa kimbele mbele kuingia Msumbiji kusaidia Serikali dhidi ya waasi, yatatukuta ya Garissa.
 
Uko sahihi kabisa mkuu, makundi kama haya hayamaliziki kwa operation ya kijeshi ya usiku mmoja ila ni suala linalohitaji muda (Nigeria mpaka sasa inapambana na Bokoharam) na ina gharama zake kirasilimali (fedha,vifaa,mafunzo) na hata kiusalama (mfano Kenya na Uganda baada ya kuingia Somalia).
 

Hizi Ishu inabidi uzijadiri kila moja peke yake,hao wengine inawezekana sio legelege,lakini,Kuna sababu zingine zinazofanya washindwe,ila huyu wa msumbiji,kwa viwango vyovyote vile ni legelege

Dawa ya magaidi ni a bullet in the back of the head,hiyo ndio lugha pekee wanayoielewa

Na hivi vikundi huwa havizuki tu

Unakumbuka misafara ya kikundi Cha ISS,ilikuwa inajaa landcruiser mkonge tupu,Tena mpya!jiulize zilikuwa zinanunuliwa wapi,na zinawafikiaje?
 
Sikia hao ISIS hawapigani kwa manati, so sisi tujizatiti kulinda ardhi yetu tu isiguswe na hao panya wajiitao isis..bila shaka wa Sasa bado hatuna uwezo wa kupambana na makundi Kama haya yenye silaha,,kushambulia na kukimbua ndo njia yao.. walaaniwe

,
 
Mpaka hata leo Syria, Iraq, Nigeria
 

We jamaa, wafahamu manati yananikumbusha mbali sana?

Kuwinda njiwa au tetere.
 
Tukijitoa kimbele mbele kuingia Msumbiji kusaidia Serikali dhidi ya waasi, yatatukuta ya Garissa.

Kimbele mbele ndio suluhisho.... Hadi Sasa serikali ya Mozambique ipo kimya na haijafanya operesheni zaidi ya Ile waliyosema wameua Viongozi wa ilo kundi ambao wakadai Ni watz.

Cha msingi Ni kuingiza tu jeshi Hadi ktk hiyo bandari na kuikomboa. Kama hao msumbiji hawawezi kujipanga kwa mashambulizi.

Pia kuomba kibali Cha kufanya shambulio, hao magaidi watapenyezewa taarifa na baadhi ya Viongozi wanaoshirikiana nao wa serikali ya Mozambique...
 
ni kawaida kupigwa hata wairaeli walipigwa. Na wafilisti saana japo walikua imara ila ukilemaa kidogo. Ndio adui anashika. Hatamu
 
We jamaa, wafahamu manati yananikumbusha mbali sana?

Kuwinda njiwa au tetere.
Nazijua nilikua natumia kupigia mbuzi na ndege wakati nachunga.. lakini pia nimewahi pigwa na manati karibu kabisa na jicho na dogo mmoja mkorofi huko machungani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…