Ushauri kwa M-Pesa tawi la Vodashop Mlimani City

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,455
29,133
Leo nilipita kwenye hili tawi la M-pesa kujaza akaunti yangu, baada ya kuhesabiwa kwenye kimashine chao ambacho mteja hukioni nikaambiwa eti zimepungua alfu 10 wakati hela nimetoa benki,
Sitaki niingie kwa gia ya kuwakandia moja kwa moja kua ni wezi, kwani inawezekana ni kosa langu pia labda wakati natoka benki nliingiza hela pungufu mfukoni.
But ushauri wangu hizo mashine zenu mziweke kwa namna ambayo tutaziona na sisi wateja kama benki wanavyofanya.
 
Ujumbe utakuwa umefika....maana najua nao wanapita pita humu jamvini!!!
 
kawaida unapohesabu fedha za mteja, mteja anatakiwa aone, inawezekana ni kweli zimepungua au uhuni wa watumishi wa hilo duka, kama ndivyo wanavyofanya inabidi wajirekebishe
 
Nitakusaidia kuufikisha sasa hivi kuna mtu niko nae hapa wa VODA. Wasilete mambo ya wizi hela yenyewe mgogoro kuipata.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom