Ushauri kwa kipindi cha Clouds TV kiitwacho Clouds 360

Ushauri kwa kipindi cha Clouds TV kiitwacho Clouds 360

Niliwahi kuo-comment juu ya kipindi hicho,kwa kweli kinaboa sana,mi naangalia asubuhi kwa vile AZAM haina star TV ambayo ni the best kwa TV zote kwa kipindi chao cha yaliyomo magazetini,uwa wanatoa summary nzuri sana tofauti na TV nyingine yoyote Tanzania,uwa naanzia ITV ambao wao wanasoma tu vichwa vya habari na hakuna cha ziada,kisha nahamia clouds kuangalia kama kuna la ziada kabla siajenda kwenye mizunguko yangu.Tatizo clouds wanatumia muda mwingi kujadili nonsense na vitu vingi ambavyo hawana uelewa navyo pia wanaingiliana ingiliana pal aliyena unafuu ni yule dogo anayetangaza mpira,uwa wananiboa tena ku quote ma-philosophers mara alistotle,mara Einsten etc
 
Kama Clouds wanataka kupendwa na wasikilizaji ni dhahiri wanakiwa kubadilika. Kweli hakuna kitu perfect duniani, lakin basi wajifunze kutokana na maoni ya watazamaji/wasikilizaji. TV sio chombo cha kuuzia sura, ni chombo cha umma cha habari na biashara! Mbadilike!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Pia waache political biaseness,mfano mtangazaji mmoja anaweza kusema kitu kinachohusu mbunge fulani,mwingine anadakia kwa kuuliza, kwani yule mbunge ni wa chama gani? kama ni CHADEMA au CUF watakitaja hicho chama lakini kama ni CCM utasikia mmoja wao anajibu kuwa SI NI KILE CHAMA CHETU, sasa mimi uwa napata wakati mgumu sana kuwaelewa na hasa ukizingatia maadili ya taaluma zao,je ni sahii kwa watangazaji kuonyesha ukereketwa wa waziwazi? Mbona hata TBC ambao tunawajua inclination yao hawaonyeshi ukeleketwa wa wazi? Au hiyo clouds ni TV ya CCM?

Nadhani wale ambao mmewahi kufuatilia comments za hao watangazaji wa 360 kuhusiana na mada mfano Bunge la katiba, Ukawa etc mtakubaliana na mimi kuhusu ilo.

Hata leo asubuhi walikuwa wanashabikia waandishi kupigwa na polisi kuwa eti walifuata nini na kwanini hawakuwa na vitambulisho, kwa hiyo polisi walishindwa kuwatofautisha na mashabiki wa CHADEMA hivyo ni sahihi kupata kipondo,mimi kwa ilo sikuwaelewa kabisa ukizingatia kuwa nao ni waandishi wa habari, pale issue ilikuwa ni matumizi ya nguvu na sio matumizi ya nguvu kwa nani?

Wajirekebishe, wanaowakosoa wanapenda wandelee kuonekana runingani.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums[/QUOTE]
 
Kuna huyo Jamaa anaitwa Sasala(?)...Sikumbuki jina lake....hana haiba ya utangazaji kabisa...hata kusoma magazeti kama ana kimuemue...Yule demu ndio kabisaaaaaaa..Uelewa wa mambo 000....Hawajui kupangilia mada na jinsi ya kujadili...Niliwangalia Mara kadhaa sijarudia tenaaa
Huyo jamaa ni Hr pale nashangaa kahamia kwenye kusoma magazeti halafu heading za UKAWA na magazeti kama mwananchi na Tanzania Daima hasomi kazi kufagilia CCM
 
Kija arudi kwenye vipindi vya muziki. Kama alivyokuwa eatv .

Hawezi kuhoji wala kutoa point kwenye masuala ya siasa , uchumi na nchi.

Mara nyingi huwa anainama na kuona aibu tu.

Yule kaka nae anamwonekano wa kuuza kwenye luninga ila hana hoja Anakuwa hajiamini.

Wabadilishe jinsi wanavyokaa (set up ya kipindi).
 
Yule dem kimeo kanifanya niache kuangalia kile kipindi. Hata yule jamaa anayesoma vichwa vya magazeti hafai kabisa. Kwa ufupi kile kipindi hawajajipanga kabisa.

Karibuni morning trumpet ya Azam tv ndo habari ya mjini..
 
Hao clouds Tv kweli wachanga bado,maana mpaka leo hawana kipindi kizuri.

Wajipange upya wafikie level flan za Eatv afu yule kijakazi Yunus kafuata nini kule??

Angalau cha afya check na mchezo wa mahusiano namkubali Clinton..vingine hakuna kitu
 
Niliwahi kuo-comment juu ya kipindi hicho,kwa kweli kinaboa sana,mi naangalia asubuhi kwa vile AZAM haina star TV ambayo ni the best kwa TV zote kwa kipindi chao cha yaliyomo magazetini,uwa wanatoa summary nzuri sana tofauti na TV nyingine yoyote Tanzania,uwa naanzia ITV ambao wao wanasoma tu vichwa vya habari na hakuna cha ziada,kisha nahamia clouds kuangalia kama kuna la ziada kabla siajenda kwenye mizunguko yangu.Tatizo clouds wanatumia muda mwingi kujadili nonsense na vitu vingi ambavyo hawana uelewa navyo pia wanaingiliana ingiliana pal aliyena unafuu ni yule dogo anayetangaza mpira,uwa wananiboa tena ku quote ma-philosophers mara alistotle,mara Einsten etc

Km unataka uchambuzi wa magazeti Azam tv wanachambua vizuri sana kipindi morning trumpet
 
Kile kipindi producer wake researchers wake wote hovyoo. Setup ya kipindi hovyo.

Kusoma hamjui hata kujifunza kwa TV zingine hamuoni?? Huyo dada anakula kucha anatazama chini muda wote, story zao nyepesi mnoo hazina nyama, nyingi ni copy & paste ya BBC.
 
yule binti asingeruhusiwa kucommment hana uelewa wa mambo leo nlikuwa naangalia ni vituko..hajui tofauti ya hoja mbalimbali..
 
Umeshindwa kutumia akili yako na muda wako kushauri vitu vya msingi kwenye maisha yako. Unashauri clouds? Stop worrying about the wrong people.

ungeanza wewe kujishauri juu ya maisha yako kuliko kuchangia vitu ambavyo wewe unajua havina msingi kwa maisha yako....kunyamaza kimya ni busara pia
 
Mimi huwa nasubiri wamalize ili niangalie kakipande ka 'JE WAJUA?mengine kwa watu wa huku kusini hatuwaelewi kabisa.
 
jmn mi mwenzenu nkijickia nimeboreka nakiweka ili nicheke bs c Mana huwa wananifurahisha tu mambo yao.
 
huyu dada Kija anafanya nini pale kwenye kipindi, bora yule kaka Hudson Kamoga ana unafuu. Huyo dada ni janga, leo walikuwa na ugeni toka OSHA hajui hata OSHA nini. Hii ni taasisi ya usalama na afya kazini yeye akajua ni kuosha vyombo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom