Ushauri kuhusu mke wangu kutokubadilika

Rukie

Member
Sep 27, 2022
78
123
Habari za Leo

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 35 nimeoa na kubahatika kupata watoto wawili.

Nimeoa takribani miaka 6 iliyopita na mke wangu nilimtoa kijijini kutokana na hali yangu ya uchumi haikua sawa.

Changamoto iliyofanya kuandika huu uzi ni kwamba mke wangu habadiliki kabisa, ule ushamba wa kijijini bado anao. Nimejitahidi sana kumjali, kumpa pesa lakini habadiliki kabisa kuanzia uvaaji na hata kupendeza kitu ambacho hupelekea mimi kupata aibu kwa sababu inaonekana kama natesa familia.

Nimejitahidi kumpatia sehemu biashara zangu ili apate pesa na kununua baadhi ya mahitaji ya kujipendezesha lakini hakuna kitu.

Binafsi nampenda sana mke wangu, ni mpole na siyo msaliti ila nataka apendeze zaidi. Naombeni ushauri kama kuna njia naweza tumia ili mke wangu awe mzuri, bora na hadhi na apendeze. Inafika mpaka anazidiwa na wafanyakazi wangu tuliowaweka katika biashara.
 
Habari za Leo

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 35 nimeoa na kubahatika kupata watoto wawili.

Nimeoa takribani miaka 6 iliopita na mke wangu nilimtoa kijijini kutokana na Hali yangu ya uchumi haikua sawa.

Changamoto iliyofanya kuandika huu Uzi ni kwamba mke wangu habadiliki kabisa ule ushamba wa kijijini Bado anao. Nimejitahidi sana kumjali kumpa pesa lakini habadiliki kabisa kuanzia uvaaji na hata kupendeza kitu ambacho hupelekea Mimi kupata aibu Kwa sababu inaonekana kama natesa familia.

Nimejitahidi kumpatia sehemu biashara zangu ili apate pesa na kununua baadhi ya mahitaji ya kujipendezesha lakini hakuna kitu.

Binafsi nampenda sana mke wangu ni mpole na sio msaliti ila nataka apendeze zaidi. Naombeni ushauri kama Kuna njia naweza tumia ili mke wangu awe mzuri Bora na hadhi na apendeze inafika mpaka anazidiwa na staff wangu tuliowaweka katika biashara.
Na akibadirika tu, unaibiwa niamini hapa
 
Apendeze kwenye sehemu gani?????

Arembe uso na kusuka? ama mavazi?

kwa hayo ni rahis sana.

kasheshe ipo kwenye kunenepa na kupungua, mke akinenepa sna na ukitaman apungue hapo ndie kuna mbinde ya hatar 😃😂
 
Habari za Leo

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 35 nimeoa na kubahatika kupata watoto wawili.

Nimeoa takribani miaka 6 iliyopita na mke wangu nilimtoa kijijini kutokana na hali yangu ya uchumi haikua sawa.

Changamoto iliyofanya kuandika huu uzi ni kwamba mke wangu habadiliki kabisa, ule ushamba wa kijijini bado anao. Nimejitahidi sana kumjali, kumpa pesa lakini habadiliki kabisa kuanzia uvaaji na hata kupendeza kitu ambacho hupelekea mimi kupata aibu kwa sababu inaonekana kama natesa familia.

Nimejitahidi kumpatia sehemu biashara zangu ili apate pesa na kununua baadhi ya mahitaji ya kujipendezesha lakini hakuna kitu.

Binafsi nampenda sana mke wangu, ni mpole na siyo msaliti ila nataka apendeze zaidi. Naombeni ushauri kama kuna njia naweza tumia ili mke wangu awe mzuri, bora na hadhi na apendeze. Inafika mpaka anazidiwa na wafanyakazi wangu tuliowaweka katika biashara.
Mkuu mshukuru mungu aisee, ukihitaji abadilike zaidi wajuba wataanza kukugongea mkeo na kisha utakuja kulia tena humu .

Kama anatimiza majukum yake Kama mama Wa familia kikamilifu basi we muache hivyo hivyo , usije ukaanza kujuta bure
 
Mnunulie nguo ambazo binafs akivaa unaona utavutiwa kuhusu kusuka kama unapenda mpelekee saluni mchagulie nywele nzuri au ongea na msusi amsuke msifie sana Yani msifie Kila baada ya dakika akiona ndo kitu unapenda atabadilika huenda hajui nn afanye
Piga show za uhakika

Achana na Hao et atabadilika Malaya Malaya tu hata huko vijijin wanawake Malaya wapo na watu wameoa wanawake walioona sio washamba na Bado wamepigwa na vitu vizito
 
Mkeo wewe ndio unamjua unajua nini akivaa atapendeza na nini hakitampendeza .Mpaka hapo ninrahisi sana nguo mnunulie wewe zile za hadhi unayoitaka na unazojua zitampendeza kutokana na alivyo na saloon mpeleke au unamwambia nenda saloon kasuke hapo tayari ushalipia na kumwambia msusi amtengeneze vizuri apendeze.

Viatu unamnunulia na urembo pamoja na kumtafutia mafuta mazuri.

Ukishafanya yote hayo lazima tu atabadilika mana atavaa vile ulivyomnunulia wewe na akishazoea na kujiona anapendeza hata taka tena kurudia vya zamani.

NB ila kuna watu hawabadilikagi hata umnunulie nini bado tu atachemka. Ukiwa na wa hivi wewe ndio unampangia kabisa mfano Kuna shughuli au Kuna sehemu mnaenda pamoja unamchagulia cha kuvaa yaani wewe ndio unamuandaa ili asije kukutia aibu mana wao wanaonaga wapo sawa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom