Ushauri katika hili-yamenikuta!

blauzi

Member
Aug 28, 2008
24
5
Mimi ni mvulana niko masomoni kwa sasa.(Nasoma Degree ya pili) Nina mpenzi wangu tuliyedumu nae kwa miaka 3 sasa. Nimeshamtambulisha nyumbani kwetu, na pia nafahamika kwao japo sijaenda kujitambulisha rasmi. Nikiwa kwenye harakati za kwenda kutoa posa kwao, yeye alipata ajira na hivyo kwenda kazini.Akiwa huko mawasiliano yamekuwa ni mazuri tu na sikupata shida wala wasiwasi juu ya penzi letu. Miezi miwili baada ya kulipoti kazini, alinipigia simu huku akilia na kuogopa kilichotokea,ambacho anadai ni shetani amemtokea. Ana mimba, anayodai shetani alimfanya amkubalie mwanaume mmoja walieshinda nae huko siku ya kuriporti kazini. Msababishaji bado hajapata taarifa za mimba hiyo.Anadai bado ananipenda na ANAOMBA RADHI. Mimi bado sijampa msimamo wangu kuhusu hilo.

Naombeni ushauri wenu wanajamvi, natafakari sana kabla sijatoa maamuzi magumu.
 
Jaribu kupitia thread flan ipo humu humu MMU ina title "NIOE ALIYEZAA?" unaweza kupata mawili matatu manake kisa kinakaribia kufanana na chako.
By then, kama mmependana kwa dhati na kama binti ana tabia njema, usiumize kichwa. Tanangaza kikao cha kwanza fasta!
 
sidhani kama kisa hiki kinafanana na kile per se.

Kile kisa Tegemea kakutana na mwanamke ana mtoto kampenda anataka avute ndani, na yeye ana mtoto aliyeachiwa na mkewe.

Hapa jamaa ana mchumba, ambaye kajazwa na shetani wakiwa kati kati ya uchumba wao.
Kwa kifupi, kapigwa tawi tena kavu kavu.

Jaribu kupitia thread flan ipo humu humu MMU ina title "NIOE ALIYEZAA?" unaweza kupata mawili matatu manake kisa kinakaribia kufanana na chako.
By then, kama mmependana kwa dhati na kama binti ana tabia njema, usiumize kichwa. Tanangaza kikao cha kwanza fasta!
 
Mmmh! Haya mambo haya Sijui kwa nini watu c waaminifu jamani! Pole bwana endelea kusubiri maushauri toka kwa wapendwa! ila hiyo ID yako sasa!
 
wewe nazani ni msichana-hii stori inaweza kuwa yako-so unataka kujua reaction ya jamaa wako itakuwaje
huwezi jiita "blauzi" kama wewe si mwanamke
 
mwambie huyo mwanamke kama 'shetani alimpitia' amshike mkono huyo'shetani' waendelee na safari....

Miezi miwili tu kakusaliti ingekua mwaka?
 
mi siamini kuwa kuna kitu kama shetaki mumpitia mtu...siku hizi naona shetani anasingiziwa kila kitu hata kile ambacho hausiki... huyo aliamua kufanya na itabaki kua hivyo!! nisingependa kutumia maneno mazuri ya kukupa moyo kuwa kila kitu kipo sawa na kaza moyo songa mbele!! ki ukweli kuna tatizo hapo... juilize vipi ukipata nafasi ya masomo nje ya nchi kwa miaka mitano kwa mfano... si utakuta kaolewa na anaishi na mwanaume nyumbani kwako?
mimi sidhani kama anakufaa maana kama "asubuhi tu imekuwa hivyo...jioni itakuwaje?"
All in all wewe ndo mwamuzi wa mwisho...sisi tunashauri tu..
 
Acha masihara blauzi, yaani apo unatafuta ushauri? Kusoma hujui hata picha huoni?
 
yaani mtu na digrii mbili anajiita mvulana lo! nadhan huyu ni darasa la pili sio digrii 2
 
mungu wangu mbavu zangu jamani.kongosho jamaniiiiiiii
huu niushauri wangu bila kigugumizi. Hakufaiiiiiiii na mshukuru mungu hukufikia kumuoa achana nae mwambie alale mbele na mume wake mpya tena wakafunge ndoa fasta tu. Piga chini leoleo tena kama unahitaji ushauri. Tena inaonekana unaongozwa na mungu kweli kwasababu umefunguliwa macho uone sasa kama ni kipofu sawa tu. Dunia ya sasa jamani inaenda mwisho imefika hapa? Duh mimi ndiyo hayo tu
 
Jaribu kupitia thread flan ipo humu humu MMU ina title "NIOE ALIYEZAA?" unaweza kupata mawili matatu manake kisa kinakaribia kufanana na chako.
By then, kama mmependana kwa dhati na kama binti ana tabia njema, usiumize kichwa. Tanangaza kikao cha kwanza fasta!
hakuna mapenzi ya dhati hapo mkuu, mzembe mwandamizi huyo, ningekuwa mimi ningesitisha mipango ya ndoa na kujenga uhusiano wa kaka na dada.
 
hakuna shetan wala nn!hapo chukulia asngepata mimba,ungeoa,afu jamaa angendelea makamuz kama kawa!au angepata ngoma na wewe ungekua umeukwaa!cha msingi piga chini angalia mbele!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom