Ushauri katika kadhia hii ya kifamilia

biasharaTz

Senior Member
Apr 14, 2016
154
225
Habari zenu
Baada ya salamu tupeane pole wote kwa kuisoma namba hasa pasina matarajio ya lini hali za kiuchumi zitaka sawa
Ama baada ya hilo, ndugu zangu naombeni ushauri muhimu sana katika kadhia ambayo imetokea katika ndoa yangu
Kwa kifupi ni kuwa kuna binti tulioana kwa muda kama miaka mitatu hivi na kidogo katika muda huo wote tulijaaliwa kupata mtoto mmoja kwanza ila ukawepo utata kuhusiana na baba halisi wa huyu mtoto kwani mienendo ya huyu aliekuwa mke wangu ilibadilika sana kabla ya kupata mimba hasa baada ya kupata kazi shirika moja hivi la hifadhi jina kapuni na kwa bahati nzuri alipata cheo. Kielimu yeye ana shahada na mimi vile vile ni shahada tofauti zetu ni kuwa mimi niliachana na masuala ya kuajiriwa na kujikita katika kujiajiri. Alhamdulillaah biashara hazikunitupa mkono kwani kama kula, nyumba na usafiri havikuwa tatizo kwangu
Na vilevile japo mshahara wake alikuwa anapata mkubwa tu lakini hata siku moja sikuwahi kumwambia anisaidie katika majukumu kama mume ila akijisikia alikuwa anasaidia. Na hili nililifanya hasa kwa misingi ya dini yetu.
Turejee katika suala la mtoto. Huyu mtoto alivyozaliwa wazazi na ndugu walipomuona walisema kuwa makini mtoto huyu sio asili yetu kwa watu wa Visiwani hasa mnatujua. Hakuwa kabisa na uasilia wowote na kinasaba na jamaa yoyote na kwetu lakini nikajipa matumaini huenda anafanana na upande wa kwao. Ila kuna siku nikamweleza mwenzangu kuwa kuna haja ya kumpima DNA mtoto yule mwanzo alikataa lakini baadae akakubali kwa shingo upande. Kabla ya kwenda kumpima nilipata safari ya dharula kwenda nje ya nchi basi nilivyorejea kumkumbusha tu suala la DNA ikawa shida. Maana alimwaga matusi na maneno vibaya sana na mwisho akanitamkia kua yule mtoto mimi sio baba yake. Baba yake yupo bosi aliempa nafasi kule kazini. Mwanzo niliona mas'khara. Lakini aliendelea kushikilia msimamo huo na kurudia zaidi ya mara 5.
Kiukweli niliumia sana na pamoja na maneno na kero zoote sikuwahi hata siku moja kumjibu vibaya. Kuificha aibu ile ilibidi niende kwa mama yake mzazi yaani mkwe wangu wa kike. Nikamweleza a to z ya yote. Ajabu yule mama kwa lugha lainiii kabisa akaniambia sawa kama ishatokea sasa tatizo lako ni nini. Ulitaka mtoto wetu akose kazi sehemu nzuri? Daah nikakubali matokeo na kusema alhamdulillaah na kuondoka zangu. Basi baada ya hapo nikaamua niachane nae. Nikampa talaka na kuendelea na maisha yangu
Sasa wiki kama mbili zilizopita alinipigia simu kuniambia kuwa amejifungua na huyu mtoto ni wa kwangu. Yaani kanishangaza sana na bahati mbaya sikumbuki lini tulishirikiana tendo la ndoa wakati ule wa sekeseke la talaka kwani sikuwa na hamu kabisaaa na mapenzi tena. Na mbaya zaidi ananisistiza kuwa hata yule mtoto wa kwanza ni wangu pia kwani zile zilikuwa hasira tu kuniambia maneno yale na pamoja kuwa alinihakikishia mbele ya mama yake kuwa yule mtoto si wangu
Wanajamii hebu nipeni ushauri huyu mwanamke ni mkweli kweli au ni muongo? Maana navyojua ukweli wa baba wa mtoto anaujua mama mwenyewe! Na pili, moyo wangu kimahabba kwake na mtoto ulishakufa kabisaaaaa sina hata chembe ya upendo nao japo sina chuki nao. Hivyo ukisema tukapime DNA naona hata kama itaonyesha nina uhusiano nao lakini siwezi tena kuwa na upendo kama wa mwanzo
Pili, kule ofisini kazi hajaacha je uhusiano na huyo bosi aliemuweka hautakuwa unaendelea?
Tatu, nini hasaa kinachomrudisha kwangu na kujiliza usiku na mchana kubembeleza turudiane au tuendelee na maisha kama zamani? Kwa sababu kwa mtazamo wangu aliamini ukiwa na pesa basi ndo maisha umeyaweza?
Naishia hapa labda na wenzangu mna neno la ushauri
 

Nokia83

JF-Expert Member
Jan 16, 2014
24,627
2,000
Sasa kama huna chembe ya upendo ushauri wa nn?!

Umeshamwacha basi hamna kurudiana nae tena.
 

Madame S

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
15,289
2,000
kama ulimshampa talaka yatosha cha kukusaidia kapimeni DNA hua haidanganyi
 

Mbushuu

JF-Expert Member
Aug 3, 2011
1,947
2,000
Kweli tuishi nao kwa akili, kapime DNA ili kujiridhisha kwanza mambo mengine yatafata
 

Daudi1

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
6,815
2,000
Ulishaenda mpaka kwa mama yake bado akawa upande wake, na aliona kazi ni muhimu kuliko mume wa nini sasa, hata vipimo vikionyesha mtoto ni wako huyo mwanamke hakufaiii uzuri wake umempa talaka chapa lapa endelea mbele
 

Namge

JF-Expert Member
Oct 9, 2016
1,231
2,000
Kapime DNA... Kama ni wako.. Tunza wanao/mwanao..

Endelea mbele.. Tena wew unaonekana Ustadhi una nafasi karbu nne..relax bhana..
 

jichopevu

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
404
250
Nenda kapime DNA, kama watoto ni wako, walee wakuze, wape malezi mema na mazuri. Dini inakutaka hivyo, utakuwa mas'ul juu yao

Kuhusu mke wako sina cha kukushauri. Ila ameshaonyesha uvunjaji wa uaminifu....maamuzi ni juu yako
 

Cute shy

JF-Expert Member
Apr 27, 2015
1,135
2,000
Piga hesabu ulivyorudi ulifanya naye mapenzi, ukikumbuka hilo ndo dna yako, kuhusu kupima mkisema mna ndoa hata majibu yakiwa mabaya upande wako, dr. Atamlinda mtoto au watoto wasije kukosa baba wakawa wa mitaani
 

biasharaTz

Senior Member
Apr 14, 2016
154
225
Asanteni kwa ushauri wakuu. Naona suala la DNA ni soundable ntalifanyia kazi ila suala la kurudiana hakika nakiri hili hapana. Japo suala la hawa watoto nakiri ntahitaji physchiological counselation maana unajua ukishaambiwa hawa watoto si wako then baadae uambiwe wako. Kidogo kuukubali ukweli inachukua muda hasa ukizingatia tayari ulishakubali matokeo na kusonga mbele kimaisha
Asanteni sana
 

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
26,668
2,000
Kumbe mimi nipo tofauti sana aiseee........
Nikisha acha, hua sirudi.
Na kuomba ushauri kwenye mambo kama haya ni moja ya dalili za kwamba ulimuacha kwa kukwepa aibu, lakini moyoni bado una huba na mtalaka wako.
 

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
26,668
2,000
Watoto kama ni wako ama si wakwako, hilo ni jambo lingine. Na kimsingi watoto hawapaswi kubebeshwa adhabu kwa makosa ya mama yao.
Mkuu... Mbona watu tuna lea watoto wasio wetu, na maisha yanasonga..!!?
Kikubwa jipime na usikilize nini haja y moyo wako. Kisha fanya maamuzi ambayo hautakuja kuyajutia maishani mwako.
 

miss chagga

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
57,919
2,000
humpendi .. chukua watoto kapime DNA kama ni wako hudumia huko alipo kama si wako ka kimya fanya maisha yako.. hiyo familia hawana busara kabisa .. si anakazi nzuri akaolewe na kazi.. wanawake huwa tunakosea hesabu ndogo sana ukiwa mchepuko very rare utakuwa njia kuu badala utunze goma lako unalitawanya na kulichafua kwa jeuri ya mchepuko.... haya kianchomrudisha kwako ni kwamba anatafuta pakutulia nadhani alitarajia makubwa huko kayakosa sasa anarudi kwa danga lake teh .. kama huna upendo usirudiane nae na wala usirudiane kwa sababu ya huruma..
 

biasharaTz

Senior Member
Apr 14, 2016
154
225
Kumbe mimi nipo tofauti sana aiseee........
Nikisha acha, hua sirudi.
Na kuomba ushauri kwenye mambo kama haya ni moja ya dalili za kwamba ulimuacha kwa kukwepa aibu, lakini moyoni bado una huba na mtalaka wako.
Mkuu hata mimi nikiacha huwa sirudi nyuma lakini kutokana na usumbufu wa simu zake za mara kwa mara ndiyo maana nikaona vema labda niangalie hili jambo kwa jicho la pili.
Vilevile suala la kulea mtoto asie wangu naweza sana lakini sio kwa mwanamke aliekuwa mke wangu azae nje angali yupo ndani ya ndoa na mimi then nilee. Hili halipo NEVER. Bora basi angekuwa labda 'single mother' ila sio.
 

pantaloo

JF-Expert Member
Mar 28, 2015
375
225
Kuna wanawake wana maudhi hawafai hata kulumangia na kachumbali
Nikirudi kwenye point
1 Pima DNA
2 angalia haja ya Moyo wako kaka
3. Ukiona VP nyoosha mwendo kaka. Ila kama dam yako Lea wa toto ila usiowe huyoo mwanamke
 

Lihakanga

JF-Expert Member
Dec 17, 2016
1,969
2,000
Sikiliza bro, watoto siyo wako(katamka mmoja lkn hata huyo jua si wako). Kwao wanajua watoto ni wa bosi alompa kazi nzuri. Unabembeleza nini? Huyo kaona dalili ya kuachwa na bosi. Anajihami asibaki hewani. Sasa na wewe mwonyeshe kuwa siyo "bushoke" Nina hasira kama kesi yangu vile.
 

biasharaTz

Senior Member
Apr 14, 2016
154
225
Sikiliza bro, watoto siyo wako(katamka mmoja lkn hata huyo jua si wako). Kwao wanajua watoto ni wa bosi alompa kazi nzuri. Unabembeleza nini? Huyo kaona dalili ya kuachwa na bosi. Anajihami asibaki hewani. Sasa na wewe mwonyeshe kuwa siyo "bushoke" Nina hasira kama kesi yangu vile.
Nimekuelewa sana mkuu Lihakanga. Nashukuru hisia zangu nawe umezivaa. Kiukweli jinsi alivyonipigisha kwata wakati ule nina moyo wa kubembeleza na kuipigania ndoa sidhani kama itatokea tena kwake au kwa wanawake wengine.
Suala la kupima DNA, nashuku nalo hasa ukizingatia madaktari khofu ya kuchezewa mchezo mchafu wa kubambikizwa nakugeuzwa majibu kuwa siyo ndiyo. Nimekuja gundua sasa watoto wanaotelekezwa na wazazi hasa wa kiume wasiwe na jazba na baba zao bali wajitahidi kuujua ukweli kwani mapenzi ya baba kwa watoto huweza kufishwa na kauli na vitendo vya mama yao
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom