Nyati hebu tupe taarifa ya maamuzi yako ulinunua wapi (duka gani)? Za size gani? Aina gani (ceramic, porcelain, granite9? Na kwa bei gani kwa square metre?
Wakuu leteni habari mpya kwa wale mnaondelea na ujenzi hasa wale waliofikia hatua ya kuweka floor tiles
nyumba yako bado hujaweka tiles tu!!!
Wakuu leteni habari mpya kwa wale mnaondelea na ujenzi hasa wale waliofikia hatua ya kuweka floor tiles
Mkuu, mimi nimetumia tiles grade 1 wenyewe wanaziita granite za China ni nzuri sana na quality yake haina tofauti na hizo za Spain na bei yake ni TShs. 16,500 tu kwa sqm. Hizi ni za floor za ukutani ziko za 7,800 na za 18000 kwa sqm.
Mkuu rmashauri, ulinunua wapi hizo? na je una picha kadhaa? hili suala linaniumiza kichwa sasahivi nipo kwenye zoezi la kuweka tiles mjengo wangu ila nipo mbali...
Dada Belinda, ilikuwa nizinunue kutoka GoodOne, hawa ni wachina wako pale mtaa wa Swahili Kariakoo. Tulipofika pale na fundi wangu tukakosa ile rangi niliyoipenda pale kwenye display yao lakini kwenye stock yao haikuwepo. Fundi akaniambia twende duka lingine analoliamini kwa bei ileile, tukaenda kununua kwa watoto wa Mtei duka lao linaitwa Mony Tiles liko pale makutano ya mtaa wa Swahili na Kipata, ng'ambo tu kidogo ya mtaa wa Uhuru ukitokea kariakoo sokoni. Picha nilipiga kwa simu ya Nokia Lumia 600 ambayo naona ina matatizo ya sofware inagoma kutransfer picha kwa bluetooth hata kwa cable ya USB. Nitaenda site kwangu kesho na kamera nikapige picha niziweke hapa. Ila Kuna rangi nyingi sana pale dukani, kwahiyo chaguo letu (mimi na mke wangu) linaweza kuwa tofauti na matakwa yako. Ila kwa ubora hata fundi wangu alizisifia ni nzuri sana.
Useful thread kwa kweli!
Nimejifunza mengi.. But natamani kujua ni zipi hasa hazitelezi! Na nimeona baadhi ya wadau wanasema za Monalisa zinapauka.. Je kuna yeyote ameshanunua hapo na kukaa nazo vip zinapauka??
Nataka kufanya maamuzi kati ya Godone na Monalisa wapendwa!
Nauhifadhi uzi kwa ajili ya matumizi ya June.
vp jamani kuhusu hii brand ya TWYFORD?? nona ipo kwenye maduka mengi ,kuna aliyewahi kutumia aina hii ya tiles
vp jamani kuhusu hii brand ya TWYFORD?? nona ipo kwenye maduka mengi ,kuna aliyewahi kutumia aina hii ya tiles
Wakuu hizi ni tiles za Kichina grade 1, ni nzuri Kwa sana tu. Nimeziweka zinakaribia miaka 2 sawa utafikiri nimeziweka jana. Ila kama upo Dar bora kazinunulie pale GoodOne bei zao ni nzuri sana tofauti na sehemu zingine.Nami nasubiri majibu.
Wakuu hizi ni tiles za Kichina grade 1, ni nzuri Kwa sana tu. Nimeziweka zinakaribia miaka 2 sawa utafikiri nimeziweka jana. Ila kama upo Dar bora kazinunulie pale GoodOne bei zao ni nzuri sana tofauti na sehemu zingine.
asante mkuu....unamaanisha hawa GoodOne wanauza na hizo TWYFORD???....na wewe uliweka goodone au twyford
msaad wako please....maana bado sijajua tofauiti zake.
asante mkuu....unamaanisha hawa GoodOne wanauza na hizo TWYFORD???....na wewe uliweka goodone au twyford
msaad wako please....maana bado sijajua tofauiti zake.
Mkuu TWYFORD ndo zenyewe hizo wanazouza GoodOne. Zina ubora wa juu sana tu huna haja ya kutumia haja kubwa Kwa hizo za Spain bila sababu.asante kiongozi maana ss wengine spanish zimeshatushinda bei ni kali sana
Tiles za Granite za china zinapauka muda siyo mrefu. Ikiwekwa sehemu ambayo watu wanapitapita sana kama sebuleni, kwenye corridor na jikoni hazitachukua muda bila kabla hazijapauka. Porcelain ndiyo nzuri kwa nyumba zetu za kiswahili na pia bei ni nafuu sana.
Usitumie tiles za Ceremics chini (jikoni, sebuleni au chooni) kwa sababu zinanyonya maji na hivyo zitajaza uvundo sehemu hizo.