Ushauri juu ya marumaru (tiles )

Ushauri juu ya marumaru (tiles )

Nyati hebu tupe taarifa ya maamuzi yako ulinunua wapi (duka gani)? Za size gani? Aina gani (ceramic, porcelain, granite9? Na kwa bei gani kwa square metre?

Mimi nilinunua pale Mwenge karibu na kituo cha daladala cha ITV, kuna duka linaitwa CTM kama sikosei, waliniuzia za Brazil, kwa kweli kwa viwango vyangu zile ni nzuri. Bei 48,000/= per 1.44. Siyo Granite (Hazitelezi) lakini inawezekana ni kati ya hizo mbili zilizobaki. Size kwa tile moja ni kama vile 40 X 40
 
Wakuu leteni habari mpya kwa wale mnaondelea na ujenzi hasa wale waliofikia hatua ya kuweka floor tiles
 
Mkuu, mimi nimetumia tiles grade 1 wenyewe wanaziita granite za China ni nzuri sana na quality yake haina tofauti na hizo za Spain na bei yake ni TShs. 16,500 tu kwa sqm. Hizi ni za floor za ukutani ziko za 7,800 na za 18000 kwa sqm.
 
Mkuu rmashauri, ulinunua wapi hizo? na je una picha kadhaa? hili suala linaniumiza kichwa sasahivi nipo kwenye zoezi la kuweka tiles mjengo wangu ila nipo mbali...
 
Dada Belinda, ilikuwa nizinunue kutoka GoodOne, hawa ni wachina wako pale mtaa wa Swahili Kariakoo. Tulipofika pale na fundi wangu tukakosa ile rangi niliyoipenda pale kwenye display yao lakini kwenye stock yao haikuwepo. Fundi akaniambia twende duka lingine analoliamini kwa bei ileile, tukaenda kununua kwa watoto wa Mtei duka lao linaitwa Mony Tiles liko pale makutano ya mtaa wa Swahili na Kipata, ng'ambo tu kidogo ya mtaa wa Uhuru ukitokea kariakoo sokoni. Picha nilipiga kwa simu ya Nokia Lumia 600 ambayo naona ina matatizo ya sofware inagoma kutransfer picha kwa bluetooth hata kwa cable ya USB. Nitaenda site kwangu kesho na kamera nikapige picha niziweke hapa. Ila Kuna rangi nyingi sana pale dukani, kwahiyo chaguo letu (mimi na mke wangu) linaweza kuwa tofauti na matakwa yako. Ila kwa ubora hata fundi wangu alizisifia ni nzuri sana.
 
Mkuu asante sana kwa maelezo yako..ni kweli taste inaweza kutofautiana kama ulivyosema, kwa ulivyonielekeza ndani ya miezi 2 fulani nitapatembelea hapo. Pia najaribu kuangalia kama wana mtandao nione taarifa zao zaidi na laa picha kama zipo.
Asante sana na ujenzi mwema...!!
 
Useful thread kwa kweli!

Nimejifunza mengi.. But natamani kujua ni zipi hasa hazitelezi! Na nimeona baadhi ya wadau wanasema za Monalisa zinapauka.. Je kuna yeyote ameshanunua hapo na kukaa nazo vip zinapauka??

Nataka kufanya maamuzi kati ya Godone na Monalisa wapendwa!
 
Dada GoodOne na Monalisa ni two sister companies na bidhaa zao ni zilezile ila Monalisa pale kamata wanaongeza bei kidogo. Kwahiyo nenda tu pale GoodOne Kariakoo utapata za kuteleza kidogo na zisizoteleza. Ukikosa hapo nenda Mony tiles wako pale mtaa wa Sikukuu na Kipata (Kariakoo) wana tiles (malumalu) za ubora huo huo na bei ni zilezile.
 
vp jamani kuhusu hii brand ya TWYFORD?? nona ipo kwenye maduka mengi ,kuna aliyewahi kutumia aina hii ya tiles
 
Nami nasubiri majibu.
Wakuu hizi ni tiles za Kichina grade 1, ni nzuri Kwa sana tu. Nimeziweka zinakaribia miaka 2 sawa utafikiri nimeziweka jana. Ila kama upo Dar bora kazinunulie pale GoodOne bei zao ni nzuri sana tofauti na sehemu zingine.
 
asante mkuu....unamaanisha hawa GoodOne wanauza na hizo TWYFORD???....na wewe uliweka goodone au twyford
msaad wako please....maana bado sijajua tofauiti zake.
 
Mkuu ninachojua hata hao GoodOne tiles wanazouza ni hizo za TWYFORD
 
asante kiongozi maana ss wengine spanish zimeshatushinda bei ni kali sana
 
asante mkuu....unamaanisha hawa GoodOne wanauza na hizo TWYFORD???....na wewe uliweka goodone au twyford
msaad wako please....maana bado sijajua tofauiti zake.
asante kiongozi maana ss wengine spanish zimeshatushinda bei ni kali sana
Mkuu TWYFORD ndo zenyewe hizo wanazouza GoodOne. Zina ubora wa juu sana tu huna haja ya kutumia haja kubwa Kwa hizo za Spain bila sababu.
 
Tiles za Granite za china zinapauka muda siyo mrefu. Ikiwekwa sehemu ambayo watu wanapitapita sana kama sebuleni, kwenye corridor na jikoni hazitachukua muda bila kabla hazijapauka. Porcelain ndiyo nzuri kwa nyumba zetu za kiswahili na pia bei ni nafuu sana.
Usitumie tiles za Ceremics chini (jikoni, sebuleni au chooni) kwa sababu zinanyonya maji na hivyo zitajaza uvundo sehemu hizo.

Niatajuaje kama ni Porcelain, au zinakuwa zimeandikwa kwenye BOX
 
Back
Top Bottom