Revocatus James Ngoja
Member
- Aug 15, 2023
- 11
- 19
NINI KIFANYIKE KUPUNGUZA MFUMUKO WA BEI YA MAFUTA NCHINI?
Na ;Revocatus James Ng'oja
Soma kwa utulivu huu ni Uchambuzi wa Kiuchumi, Kitakwimu na Sera Mbadala.
Ndugu Watanzania,Mafuta ya petroli na dizeli ni uti wa mgongo wa uchumi wa nchi nyingi zinazoendelea kama ilivyo nchi yetu. Bei ya mafuta inapopanda, gharama za usafiri hupanda, bei za chakula hupanda, gharama za uzalishaji huongezeka, na hatimaye mfumuko wa bei huathiri maisha ya wananchi.
Kwa miaka ya hivi karibuni, nchi nyingi za Afrika Mashariki zimekuwa zikikumbwa na kupanda kwa bei za mafuta mara kwa mara. Hali hii inaleta swali muhimu na tafakuri pana ya nini kifanyike kupunguza mfumuko wa bei ya mafuta nchini?
Makala hii inachambua suala hili kwa kutumia takwimu, mifano ya sera kutoka nchi nyingine, na mapendekezo ya kimkakati kwa taifa lakini ni vena umma utambue mwandishi wa makala haya sio mchumi bali ni Mwanasiasa chipukizi, Mwanaharakati na Mtetezi wa haki za binadamu.
1. Athari za Kupanda kwa Bei ya Mafuta Kiuchumi
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za uchumi wa maendeleo, wastani wa 30% hadi 40% ya gharama za usafiri na usambazaji wa bidhaa hutegemea mafuta.
Hii ina maana kwamba:
Mafuta yakipanda kwa 10%, gharama za usafirishaji zinaweza kupanda kwa 3% hadi 5%.
Hali hiyo huathiri moja kwa moja bei za chakula, bidhaa za viwandani na huduma katika nchi nyingi zinazoagiza mafuta kutoka nje.
Tatizo linaongezeka kwa sababu:
1-Mabadiliko ya bei ya mafuta duniani
2-Kushuka kwa thamani ya sarafu ya ndani
3-Kodi nyingi kwenye mafuta
4-Kukosekana kwa akiba ya mafuta ya muda mrefu
Hivyo suluhisho la kudumu linahitaji sera za ndani na mipango ya kimkakati ya kitaifa.
2. Umuhimu wa Taifa Kuwa na Akiba ya Mafuta kwa Walau Mwaka Mmoja.
Moja ya sababu kubwa inayofanya bei ya mafuta kuyumba ni kutegemea sana soko la kimataifa bila kuwa na akiba ya kutosha.
Nchi zilizoendelea mara nyingi huwa na Strategic Petroleum Reserves (SPR) ambazo zinaweza kuhifadhi mafuta kwa miezi kadhaa au hata mwaka.
Faida za kuwa na akiba ya mafuta ni pamoja na:
1. Kudhibiti mishtuko ya soko
Ikiwa bei ya mafuta duniani inapanda ghafla kwani serikali inaweza kutumia akiba yake kupunguza athari kwa wananchi.
2. Kuzuia upandishaji wa bei holela
Wafanyabiashara hawawezi kupandisha bei kwa haraka ikiwa serikali ina uwezo wa kuingiza mafuta kutoka kwenye akiba.
3. Kulinda uchumi wakati wa migogoro ya kimataifa
Migogoro ya kimataifa kama vita au vikwazo vya kiuchumi mara nyingi husababisha uhaba wa mafuta.
Mfano mzuri ni baada ya vita vya urusi na Ukraine na Sasa America na Israel dhidi ya Iran ambapo bei ya mafuta duniani imepanda sana kwa sababu ya kuvurugika kwa usambazaji wa nishati hasa baada ya mlango bahati wa Hormuz kufungwa na Iran.
Kwa hiyo kwa Mtizamo wangu taifa linalojali uchumi wake linapaswa kuwa na akiba ya mafuta ya angalau miezi 6 hadi mwaka mmoja na sio miezi miwili kama tunavyoshudia kwa Sasa.
3. Utitiri wa Kodi kwenye Mafuta
Katika nchi nyingi za Afrika, sehemu kubwa ya bei ya mafuta hutokana na kodi na tozo mbalimbali.
Kwa mfano, katika baadhi ya nchi za Afrika Mashariki Kuna vitu vifuatavyo weka mzigo kwenye hii bidhaa.
1-Kodi za serikali
2-Tozo za miundombinu
3-Kodi za barabara
4-Kodi ya ongezeko la thamani (VAT)
5-Tozo za mamlaka za udhibiti
Kwa wastani, kodi zinaweza kuchangia kati ya 35% hadi 45% ya bei ya mwisho ya mafuta.
Hii ina maana kuwa,Ikiwa lita ya mafuta inauzwa kwa shilingi 3,000 takribani 1,000 hadi 1,300 ni kodi.Hivyo, hata kama bei ya mafuta duniani itashuka, wananchi hawataona tofauti kubwa kwa sababu kodi bado ni nyingi.
Kwa muono wangu suluhisho la kwanza ni serikali kupunguza baadhi ya kodi au kuzifanyia mapitio hasa wakati wa kupanda kwa bei za kimataifa.
4. Mfano wa sera mbadala unaweza kuonekana kuttoka Zambia.
Katika jitihada za kupunguza mzigo wa bei ya mafuta kwa wananchi, serikali ya Zambia ilifanya hatua muhimu ya kuondoa kodi ya VAT kwenye mafuta na badala yake kuweka mfumo tofauti wa kodi.
Hatua hiyo ilikuwa na malengo yafuatayo:
1-Kupunguza bei ya mafuta kwa watumiaji
2-Kusaidia sekta ya usafiri
3-Kudhibiti mfumuko wa bei
Ingawa sera hiyo inaweza kuwa na changamoto za mapato kwa serikali, itaonesha wazi kuwa sera za kodi zinaweza kubadilishwa ili kulinda wananchi wakati wa mshtuko wa kiuchumi.
5. Usafiri wa Umma wa Umeme: Suluhisho la Muda Mrefu
Mbali na sera za mafuta, suluhisho la kudumu ni kupunguza utegemezi wa mafuta kabisa.Hapa ndipo wazo la mapinduzi ya usafiri wa umma wa umeme linapokuwa muhimu.
Katika makala yangu ya hivi majuzi yenye kichwa “USHAURI KWA TAIFA: Mapinduzi ya Usafiri wa Umma Yanawezekana”, (unaweza kubofya hapa kusoma 👇 👇
Nilisisitiza umuhimu wa kubadilisha mfumo wa usafiri.
Naomba kunukuu niliyosema:
“Nchi inayotegemea mafuta kwa kila safari fupi inajifunga kwenye minyororo ya bei za soko la dunia.”
Hoja yangu kuu ilikuwa mabasi ya umeme ni suluhisho bora kwa safari fupi chini ya kilomita 200 kwa sababu:
1. Gharama ya uendeshaji ni ndogo,kwani umeme ni nafuu kuliko mafuta kwa kila kilomita.
2. Hakuna utegemezi wa soko la mafuta
Nchi inaweza kuzalisha umeme wake ndani.
3. Hupunguza uchafuzi wa mazingira
Mabasi ya umeme hayatoi hewa chafu kama dizeli.
4. Hupunguza matumizi ya fedha za kigeni
Nchi nyingi hutumia mabilioni ya dola kuagiza mafuta kila mwaka.
Kwa hiyo, kuwekeza katika usafiri wa umma wa umeme ni mkakati wa kiuchumi, si tu suala la mazingira.
6. Ushauri kwa Taifa
Ndugu watanzania ili kupunguza mfumuko wa bei ya mafuta kwa muda mfupi na mrefu, taifa linaweza kufanya yafuatayo:
1-Kuanzisha akiba ya mafuta ya kimkakati kwa walau mwaka mmoja.
2-Kupunguza au kusitisha baadhi ya kodi kwenye mafuta wakati wa kupanda kwa bei za dunia.
3-Kujenga miundombinu ya kuhifadhi mafuta kwa wingi.
4-Kuwekeza katika usafiri wa umma wa umeme.
5-Kupunguza utegemezi wa magari binafsi kwa kuimarisha usafiri wa umma.
6-Kuweka sera za muda mrefu za nishati mbadala.
Hitimisho:
Maswali Magumu kwa Viongozi.
Ikiwa taifa linaendelea kukumbwa na mfumuko wa bei ya mafuta kila mwaka, ni wakati wa kuulizana maswali magumu:
1-Kwa nini taifa bado halina akiba ya mafuta ya mwaka mzima?
2-Kwa nini kodi kwenye mafuta ni nyingi kuliko gharama halisi ya mafuta yenyewe?
3-Kwa nini hatujaanza mapinduzi ya usafiri wa umma wa umeme?
4-Kwa nini kila kupanda kwa bei ya mafuta duniani lazima wananchi ndio wabebe mzigo?
5-Je, tunajenga uchumi unaojitegemea au tunaendelea kuutegemea mafuta kutoka nje?
Maswali haya yanahitaji majibu ya kweli, sera thabiti, na uamuzi wa kisiasa kwa sababu bila kufanya mabadiliko ya kimkakati, bei ya mafuta itaendelea kuwa mzigo mkubwa kwa wananchi na kikwazo kwa maendeleo ya taifa.
Nimewasilisha.
Ni Mimi Mdogo wenu kutoka
Reha-Rombo-Kilimanjaro
Revocatus James Ng'oja