Hukustahili kuchukua mzigo pasipo kuwa na risiti halali yenye kuonyesha TRA wamepata chao, otherwise nawe ulikwepa kodi au uliwafaidisha wao.Mkuu ulipotaja Monalisa kuna kitu umenikumbusha. Hivi hawa jamaa wako katika kundi gani? Ni wafanyabiashara wa kawaida au ni wawekezaji? Je wawekezaji wanapashwa kuweka hesabu sahihi za transaction zao? Nauliza hivyo kwa kuwa nilielekezwa kwenda hapo Monalisa na jamaa yangu kwenda kununua board fulani kwa ajili ya ujenzi. Tulikubaliana bei na nililipa pale. Walinipa kikaratasi kimeandikwa kwa lugha ya kichina na kunielekeza kwenda Chang'ombe kwenye godown lao kupakia mzigo. Nilipofika Godown, niliwaonyesha hicho kikaratasi na wao walinipa huo mzigo. Delivery note waliyoniandikia pale godown, ilionyesha kwamba nimenunua huo mzigo katika duka fulani la hardware kariakoo. Pesa nilizolipa karibu 15M sikupewa receipt wala nini.
Kwa mtindo huu hawa jamaa si wanakwepa ushuru? Hata VAT hawalipi kwani malipo yangu hayakuwa na receipt.
Je kuna mwingine hapa JF aliyewahi kukutana na ujanja wa hawa wachina?
Tiba
Nenda Hugo Tiles wapo Nyerere Road ilipokuwa ofisi ya exide those days. Next to Tansoma Hotel. Hapa nimewahi nunua tiles kwajili ya ujenzi wa kibanda cha wazazi kijijini, so far niko happy na tiles zao. Kwanza ubora ni mzuri, gharama ni ya kati, hazitelezi kama za kina huhaaaaaaaaaaaaaaaaa
Hii topic nimeipenda sana. Binafsi nigependa kupata ushauri wa kubaki na terazo ama kuweka tiles, kipi ni afadhali, aesthetically zaidi. Naambiwa terazo ni ya zamani ila ni ya milele, je tiles?
Wakuu tiles za Spain naa Italia bei haikamatiki, lol! Naanza kushawishika kwenda kwa za kichina sasa
GTesha mwezi wa tisa ndio huu. Shime shime amka...Nahifadhi hu uzi naomba na mimi nikumbushwe Mwezi wa tisa please
Zipo za uarabuni nzuri na bei poa.
Mkuu bei ikoje kwa hizi za Uarabuni kwa square metre e.g za ukubwa wa 40x40 cm au 45x45cm?
Mkuu bei ikoje kwa hizi za Uarabuni kwa square metre e.g za ukubwa wa 40x40 cm au 45x45cm?
25,000 unapata vizuri sana. Ongea na Seif 0713296353 ni supplier, wana goddown Chang'ombe, yeye ndio yuko hapo, unaweza kwenda kukagua kama uko Dar.
25,000 unapata vizuri sana. Ongea na Seif 0713296353 ni supplier, wana goddown Chang'ombe, yeye ndio yuko hapo, unaweza kwenda kukagua kama uko Dar.
Asante kubwa mkuu. Nitamtafuta
Asante sana
kaka nashukuru aisee nilijua ntakuwa nimeshafikia stegi ya kuweka tiles ndo kwanza nahangaika na issue ya mbao za kazi sana ila soon ntafika.GTesha mwezi wa tisa ndio huu. Shime shime amka...
kaka nashukuru aisee nilijua ntakuwa nimeshafikia stegi ya kuweka tiles ndo kwanza nahangaika na issue ya mbao za kazi sana ila soon ntafika.
Marejesho, Angalia usichukue zenye maua, chukua plain kwani zenye Nakshi sometimes zinapauka na maua yanapoteza mvuto wake.