Kiongozi nakushauri usiache Ualimu. Kazi yeyote ile ya Uaskari...either Police au Jeshi(JWTZ) sio kazi ndugu yangu. Hao unao waona askari nao wanatamani watoke huku but wanashindwa coz they do not have other options za ajira .....nikiwa na maana hawana elimu ya kutosha (professional) au hata kama wanazo basi wamechelewa kufanya maamuzi magumu ya kutoka huko and they are late now to make hard decision hivyo wanaendelea kuwa watumwa huko jeshini/police.
MFANO:
Mimi nilijiunga na jeshi mwaka 2001 by then nikiwa form 6 leaver, kutokana na elimu yangu na uelewa wangu nilikuwa naumia sana kuona askari ....koplo au sajenti akiwa na mbavu za mbwa kutuburuza atakavyo na kutaka waheshimiwe as miungu kisa cheo.
Mwaka 2002 nika-join UDSM nikiwa bado askari nikasomea B.Ed na 2006 nilipomaliza nikapiga chini faster jeshi. Ukiwa uraiani unafaidi sana maisha na unakuwa huru. Jeshini amri za kufa mtu, kulinda guard, kufagia fagia kama mtoto wa primary na we hali ukiwa home unajidai baba wa familia...hahaha...acha hiyo makitu bana.
Leo hii am so happy na maisha ya Ualimu na nikikutana na askari wenzangu wananipongeza kwa maamuzi magumu niliyoyafanya na wananionea wivu sana.
USHAURI WA MWISHO:
1. Leo hii kama una degree ina maana utakuja kustaafu ukiwa na daraja H la mshahara! na kama ingekuwa leo hii unastaafu ualimu basi ungepata mafao yako kama Milioni 120 plus, je ni askari gani awe wa JWT au police ambae hana cheo kikubwa .....askari wa kawaida anaweza lipwa hiyo pesa???
2. Ualimu unakuwa free sana na mambo yako...fungua miradi ..ufugaji au biashara itakuongezea kipato kizuri sana but kazi ya uaskari ni utumwa.
NB: Mtoto wangu kamwe hata akose kazi lakini hawezi kufanya kazi ya utumwa ya Police au jeshi....NEVER!
Mtoa Mada Tuambie Maamuzi Yako, Maana Ushauri Umetolewa Sana Hapa!
Nadhani umeelewa
jeshi jkt miaka 2,huku huna uhakika wa kazi,then miezi 6 monduli,wewee nenda jeshini wewee, angalia posho 300,000/, salary 500,000/= ,jumla 700,000 HAYO MAPATO NI KWA ASIYE NA CHEO AMBAYE HANA SHAHADA, MWALIMU WA DEGREE 534,000/=, toa kodi,cwt na makato ya heslb, inabak 390,000/=,
private! ajira mikononi mwa wanafunzi wakikugomea tu umefunga mabegimshahara wa cheti na degree yako? Bora utafute private unapiga laki 8-9 na mazingira mazuri ya kazi after 5 yrz utakuwa mbali xna bt usisahau kupiga biashara au kilimo na ufugaji! Bt kama afya nzuri pia ukitimba polisi au jeshi unapiga ela zaidi
Mimi ni mwalimu mwenye shahada ya elimu baada ya kujiendeleza toka ualimu ngazi ya cheti,miaka 7 kazini,
baada ya kuona mambo hayaendi kabisa hapa kwenye ualimu kuna ndugu yangu kanishauri nihamie kwenye jeshi la polisi (uaskari), kwani maisha ni magumu na pamoja na kujiendeleza kielimu hakuna badiliko lolote nnlilolipata hadi sasa kuanzia mshahara uko palepale tu,
zaidi ya kupelekwa kibabe sekondari ya jirani na shule yangu ya awali bila hata kupewa stahili zangu za uhamisho,
naomba ushauri wa dhati kuhusu wapi penye unafuu,
Mimi naona police wana unafuu kwasababu police wengi wana vitambi.
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
E-bwana sikiliza Elimu uliyonayo inatosha sana kilichobaki ,angalia sehemu yenye kipato,usiogope ugumu wa kazi,angalia ANKARA.NAKUSHAURI UKIPATA JESHI WE NENDA,UALIMU MSHAHARA KIDOGO,BADO KUBURUZWA PALE PALE,UNATUPWA PORI,KUFUATA MSHAHARA MJINI UNATUMIA ROBO YA MSHAHARA WAKO,UALIMU MWANANGU SIO INSHU,MAAFISA ELIMU WENYEWE AMBAO MNALINGANA ELIMU,MACHOKO TU,WANABANA HAKI YA MNYONGE,MVUJA JASHO,PIGA UALIMU CHINI MZEE,"NI BORA NUSU SHARI KULIKO SHARI KAMILI"
ahsante sana mkuu,
umefunguka kwa uzoefu kitu ambacho kinanisaidia kupata picha halisi ya jeshi la polisi ilivyo,
jeshi jkt miaka 2,huku huna uhakika wa kazi,then miezi 6 monduli,
kazi ya ualimu ni nafuu na inampa mtu mda wa kufanya shughuli nyingine za kiuchumi pale anapo kuwa amemaliza mda wa kaz kwa maoni yangu, vilevile inampatia mhusika wakati mzuri wa kuwa karibu na familia kutokana anapata mda mwingi anapotoka kazini